Pres. Mugabe falls down steps, photographers forced to delete images

Pres. Mugabe falls down steps, photographers forced to delete images

Wamemchoka tuu, hivi kama umri umeenda kwa nini mtu usipumzike na kuachia wengine? Kwa kawaida ukifikisha umri ambao unaanguka huku unatembea mwenyewe ujue hata akili pia imechoka.
 
Amezeeka sasa angewaachia vijana madaraka halafu yy abaki kama mshauri tu.
 
Wazimbabwe sijui kwanin bado wanamchagua
 
Watu wanachangia hili tukio kishabiki zaidi tena kwa kutegemea picha za mnato!!!

Hivi kati yetu kuna mtu hajawahi kujikwaa akaanguka kwenye steps. Inachukua sekunde ngapi kuanguka mpaka useme wamemuacha anaanguka mpaka chini? Je,umeona video ya tukio zima? Je,tumeona ya kuwa alikuwa anashuka hizo ngazi kwa kasi gani?! Sasa kama hayo yote hatuna majibu yake iweje tuanze kuhukumu walinzi na wapambe wake kwa kutegemea tu ushahidi wa picha za mnato?!! Guys please...
 
Huyu mzee haambiliki wala hashauriki wa muache aendelee kuchana misamba mbele ya wajukuu.
 
Ipo siku itamkuta aibu zaidi ya hiyo.

Umri umeenda aachie na wengine.
 
Kwanini wapigapicha walazimishwe kufuta picha? mbona za JK kuanguka Jangwani bado zipo hadi U-tube.
 
Huyu ni kivuli tu kuna watu nyuma yake wanaoitawala Zimbabwe. Na hawawezi kamwe kuruhusu apumzike mpaka hapo atakapovuta. Kwa umri huo nina uhakika hata ukimuuliza leo ni siku gani anaweza asikumbuke.
 
Waingereza wabaya wakaona waiweke kwenye sky news...[video]http://news.sky.com/story/1421604/robert-mugabe-falls-down-steps-in-video[/video]
 
Teh teh teh.... the only true son of Africa we have..... very intelligent. Pole sana.
 
Ni aibu kwa viongozi wa Africa kung'ang'ania madaraka, ni hivi punde tu Rais wa Zimbabwe ameanguka ktk ngazi za jukwaa akiwa anashuka, amekuwa akiiongoza nchi ya Zimbambwe tangu 1980 hadi sasa, Reported by Aljazeera
 
kwa hiyo kikwete alipokuwa anaanguka majukwaan alikuwa king'anganiz wa madaraka?

nonsense with your topic.
 
AngeRIP kabisa.viongozi mbumbumbu na madikteta ndiyo waliotufikisha waafrika hapa tulipo.yeye na museveni ni watu hatari kwa maendeleo ya demokrasia afrika.
 
Back
Top Bottom