Predecessor curse is for everyone

Predecessor curse is for everyone

mshamba mchangamfu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
338
Reaction score
91
Kuna tukio huwa nakumbuka tukiwa wanafunzi wa sekondari tuliwah badirishiwa walimu wa 3 kwa muda wa kipindi kifupi cha ajab mwl.wa kwanza alipokuja tukamwambia tuliishia topic flan ila hatukuilewa vzuri

Yule mwl mpya namba moja akaifundisha tena maana ilikuwa ni msingi muhimu kwa topic inayofata ila kwa sababu ambazo sisi kama wanafunzi hatukuweza kuzijua akaondolewa pia tukaletewa mwl mwingine

Mwl mpya namba mbili nae alipokuja tukamwambia pia tumeishia topic ile ile ila haijaeleweka wapo walisema mwl alikuwa mkali wapo waliosema matamshi yake ya kingereza yalikuwa yanatamkwa kwa lafudhi ya kikabila sana ngumu kuyaelewa mwl mpya namba mbili nae akaona ni vyema kuirudia hii topic ila kwa kasi zaidi maana tulikuwa nyuma ya muda kumaliza mtaala ila nae kuna baadhi ya wanafunz walilaum anakasi sana kwenye ufundishaji wake hvyo tukabirishiwa

Ikabid mmoja wa walimu viongoz kwenye idara ya taalum aje ashike usukani huyu akawa mkali sanaa maana akupendezwa na tabia ya darasa letu la kumuona kila mwl mtangulizi ni mwenye mapungufu kupitiliza

Nilikuja liona hilI pia maofisini maboss wengi watangulizi wamekuwa wakiongelewa vibaya sana kiasi kwamba hata yale mazuri waliyosimamia kusahaulika

Kuna tendency inaendelea hv sasa namba one wetu wengi wanaonekana ofisini walikuwa wanakula bata kuna watu wanadiriki kulinganisha mafanikio ya awamu zote ni sawa na miaka kazaa ya awamu hii (kuna mambo makubwa yamefanyika na nakiri kuna mengi yanakuja) ila hata hawa wa, awamu hii lana ya kuzungumzwa vibaya itawakuta
 
Back
Top Bottom