Precision|Exactness|Empiricism - Uthabiti|Usahihi|Uhakika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision|Exactness|Empiricism - Uthabiti|Usahihi|Uhakika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Aug 8, 2012.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Precision/Exactness/Empiricism - The Only Solution to Tanzania's Problems (Uthabiti/Usahihi/Uhakika - Suluhisho Pekee la Matatizo ya Tanzania)

  Companero's Precision/Exactness/Empiricism model
  provides a solution to all that ails Tanzania. Whether in the political, economic, social or cultural plane the solution is the same: be precise/exact/empirical. In other words, allow for a very minute/small if not negligible margin of error. This way there will be very few accidents, very limited avenues for corruption and so forth. A bus scheduled to leave at 7 am and arrive at 7 pm should leave at 7 am and arrive at 7pm. Yes, a politician who is supposed to declare all his wealth and how s/he got it should do so precisely/exactly/empirically.

  Modeli ya Kompanero ya Uthabiti/Usahihi/Uhakika inatoa suluhisho la yote yanayoitatiza Tanzania. Iwe katika medani ya kisiasa, kiuchumi, kijamii ama kiutamaduni suluhisho ni hilo hilo: kuwa thabiti/sahihi/hakika. Kwa maneno mengine, ruhusu tu wigo finyu/mdogo sana wa kufanya makosa. Tukifanya hivi kutakuwa na ajali chache, mianya michache ya rushwa na kadhalika. Basi lililopangiwa kuondoka saa 1 asubuhi na kufika saa 1 usiku linapaswa kuondoka saa 1 asubuhi na kufika saa 1 usiku. Ndio, mwanasiasa anayetakiwa kutaja mali zake zote na jinsi alivyozipata anatakiwa kufanya hivyo kwa uthabiti/usahihi/uhakika.

  THIS IS THE PANACEA - HUU NDIO MWAROBAINI!
   
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  - kama mabomba ya maji hotelini yanapaswa kutoa maji ya moto kwa dakika 45 na yawe yanayatoa kwa dakika 45
  - kama shilingi trilioni 25 zimepangiwa kutengeneza miundombinu basi shilingi trilioni 25 zitengeneze miundombinu
  - kama mtafiti anapaswa kusema asilimia 95 zilizofanya hiki ama kile na aseme asilimia 95 zilifanya hiki ama kile
  - kama umeme unatakiwa kukatwa ama kutolewa kwa masaa 15 tu basi na ukatwe ama utolewe kwa masaa 15 tu
  - kama kifaa cha meno kinaweza kusafisha inchi 5 basi daktari wa meno anapaswa kujua hilo na kusema ni inchi 5
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Una uhakika?
   
 4. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kiranga, tuchukulie ni ya uhakika of not less than asilimia 90% hapo unakubali?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndio/Haswa
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tija ya uhakika katika jambo lolote, iwe ni kupanga kupanda mahindi yatakayozalisha magunia 75 ya mahindi na kuvuna mahindi magunia 75 ama kupanga kutoa mshahara tarehe 25 na kuutoa tarehe 25, haiwezi kupatikana bila kutumia hii modeli!
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Uhakika ni ndoto ya wasioelewa na laana ya wanaoelewa.
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  fafanua, kwa uhakika/uthabiti/usahihi
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Dude please, you can't be serious.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Halafu precision na exactness kimsingi maana yake ni moja.

  Bwa'mdogo rudi ujipange upya.
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kwani nani kasema/kadai inatofautiana?
   
 12. Companero

  Companero Platinum Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  mitanzania bwana, badala ya kujadili modeli muhimu ya kuisadia isiwe 'miafrika ndivyo ilivyo' kazi kunanga tu!
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe mwenyewe mtoa mada umechemka kwenye exactitude ya diction unategemea nini? Upigiwe makofi?
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Naweza kufafanua, lakini si kwa uhakika kwa sababu nimeshasema uhakika ni ndoto.

  Hata maneno yanayotumika kuelezea vitu katika lugha hayana uhakika ( Bertrand Russell), uhakika utatoka wapi?

  Ninaposema "hii ni rangi ya hudhurungi" na wewe ukakubali, "naam, hii ni rangi hudhurungi".

  Utajua vipi wote tunaona kitu kimoja kwa uhakika?
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Umeyaweka kwa kuyatenganisha na hivyo kumfanya msomaji aone kuwa umeyatenganisha. Ungetumia precision halafu exactness uiweke kwenye mabano hapo ungeeleweka zaidi.
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  wapi nimechemka?matumizi ya "/" na "|" ni kuweka msisitizo tu, kumbuka tulishawa kuijadili kidogo hii modeli ya precision (hayo maneno ya exactness na empiricism) ni kuweka msisitizo tu kwa msomaji kuwa tunapoongelea dhana ya precision tunaamanisha watu wawe precise/exact/empirical/factual na visawe(sinonyms) zote zinazowakilisha hayo!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Yours is a three pronged panacea. But, it's not really a three pronged panacea for precision and exactness have, in essence, the same meaning.

  So go back to the drawing board and start all over, since we are talking about preciseness.
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  hizi metafizikia ndio zinatuleta matatizo, ndio maana rushwa mmeipa majina mengi yanayoifanya isiwe presaisi, mara eti kuzunguka mbuyu, kupewa chai, kulainisha koo, kula mlungula ilhali rushwa ni rushwa tu!
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  hii michezo ya semantics ndio inalipotezea muda na tija taifa, yaani inatulostisha tu - rejea jibu kwa kiranga hapo juu!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ukija hapa na mambo ya preciseness, exactness, au sijui exactitude basi you might as well be that.
   
Loading...