Precision Air wanatia huruma

Labda wamrudishe Kioko.........huyu mama aliyepo PW imemshinda kabisa. Hata bia aliziondoa inflight kwa sababu ya imani yake!
Alphonse Kioko na Moses aliekua CFO ndio walioua hili shirika, hata suffering ya hili shirika sasa ni matokeo ya mengi waliofanya kipindi Chao. Kwa sasa Moses ni mmoja ya matajiri wakubwa tu Kenya kwa hela walizomuibia Mzee Ngaleku Michael Shirima. Mikataba mingi waliingia ya kifisadi ukiwemo wa ukopeshaji wa hizi ATR Turboprop.

Kimsingi hili shirika lilishindwa kuendana na rapid growth yao likafikia hapa chini ya management yao. Pengine labda aliekua CEO msaidizi Bw. Allan Shara angeweza kua mtu muafaka ila ndio hivyo tena wakenya walitakiwa washike zile top na crucial managerial posts!
 
Fastjet lete ndege ndogo ukatue na Mtwara, Kigoma na Tabora.
 

Angalau umewapa ukweli. Serikali ilibidi iisaidie kampuni hiyo ya kizalendo ambayo ilibeba bendera ya TZ wakati Atc ikiwa hoi na kabla fastjet haijaja na bei zake za kuizika precision. Subiri imalize kazi ya kuizika precision uone nauli zake zitakavyo paa.
 
hawa PRECISION kiukweli wanatia huruma majuzi nilisafiri nao toka KIA-DAR kupitia ZNZ daah kwanza mkiingia ndege imezimwa (AC hazifanyi kaz) FULL JOTO mpaka saa ya kuondoka ndo PILOT akawasha AC tukapaa siku ya kurudi hivyo hivyo mkiingia ndegeni jotooo mkitua znz kusubiria/kushuka ndege inazimwa. sasa kwenye PROMOTION zao ndo kituko cha mwaka wanadai nauli ni 5,000/= kumbe nauli inafika 150,000 (ONE WAY) wenzao FASTJET 6,600 (Promotion ONE WAY LOCAL FLIGHTS) ukiweka na KODI ni 19200
 
Hahhahahhahahahahah hizi bussiness ngoja tuisubiri community airline maana kama mapacha vile na fastjet
 

Hiyo nauli inakaribia nauli ya kutoka Dar to Istanbul kwenda na kurudi kwa Turkish airline
 
Presisheni sidhani kama wanajielewa kwa kweli sasa wanadai ya promosheni 195,000/= ONE WAY (Domestic Flights) wakati mpinzani ao fastjet 79,000 (one way) route hizo hizo za babu CHIRIMA
 
Waswahili mkipata chungu kipya cha zamani kinabezwa...hata kama kilifanya mchango wake vya kutosha.

FIESTA VS WASAFI.
Hivi hatuwez kum-"poach" CEO wa Qatar au Emirates akaja kutufanyia kazi hapa nchin kulirudisha ShirikA kwenye anga za kimataifa.
 
Viongozi wa serikari ndio wateja wazuri wa airplane wote ni air tz lazima wachoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…