Precision Air wamshusha Dr. Azaveli Rwaitama kwenye ndege kisa Lugha

Precision wamzalilisha Dr Azaveli Rwaitama mwanza baada ya kumutia polisi ndani ya ndege na kumshitaki kwa kosa la kukataa kutii amri za wahudumu. Kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Alikuwa ameketi kwenye kiti cha emergence exit na kuwataka wahudumu wampe maelezo kwa Kiswahili kwani ndege za Precision ni za kitanzania na zinaoparate nchini. Wahudumu walikataa na kumwamuru ahame kama yeye hajui kingereza- Kwa kuanzia hapo polisi waliitwa na kumtia mbaroni.

Ninachojua mimi ni kwamba ndege nyingi hutumia Lugha kuu za kimataifa na Lugha za nchi husika. Ukipanda Ethiopia line au Turkish na zingine nyingi watakupa maelezo kwa Lugha yao ya Taifa na zingine za kimataifa. Inakuwaje leo Tanzania tushindwe kutoa flight instrusctions kwa kiswahili?

Precision mmemkosea Dr Rwaitama mwombeni radhi na mlipeni gharama zote za kusimamisha safari yake ya Bukoba.

Fast Jet wanatumia Lugha zote mbili
 
Yeye tu na kiburi chake
 
Nafikiri huyu mzee atakua anatafuta umaarufu uzeeni. nijuavyo mimi unaponunua ticket lazima ina namba ya kiti utakachokaa. na kama alikiuka utaratibu wa kwenye ndege iweje useme amedhalilishwa. nimesafri na PW zaidi ya mara 10 na sijawahi kusika hata mara moja lugha ya Kiswahili kutotumika. wahuduu ni watanzania sitegemei hilo kutokea. naona mtoa mada anapaswa kuhakiki mada kabla ya kuiweka hapa jamvini
 
Wahaya bwana kwa masifa! Eti hajui kingereza aelezewe kwa kiswahili
 
Bora Kama kiingereza chenywe wangekimudu! Huwa wananiboa Kwa matabmshi na lafudhi ya kuigiza. Sitasahau hii, we wish you ' pilizant' flight!
 
Mods- Nimeposti maelezo ya Lwaitama tafadhali unganisheni kwenye mada kuu.

Nimesoma maelezo yako lakini kuna mahali kama hayaeleweki hivi kama yanarudiarudia. Back to the topic kuna baadhi ya mabinti wa Precision ambao kwa kufanya kazi ya kuhudumu kwenye ndege wanajiona kama miungu watu hivi. Kuna mmoja wakati natoka Nairobi mwaka 2012 alinikera sana, kisa niliomba bia ya pili aliniangalia kwa dharau juu hadi chini na ingawa hakusonya lkn nilijisikia vibaya, kwa kifupi sikupewa. Mwenzangu niliyekaa naye (mhindi / mwarabu) alipewa bia 3 za kopo ambazo baada ya huyo binti kuondoka alinipa moja na akamponda sana yule binti, baadaye pia alimletea nyingine mbili ambazo tulishea pia lkn baada ya yule binti kuondoka. Hivyo kuna baadhi ambao kwa kweli wana matatizo kidogo tena sasa hivi wamepunguza nyodo baada ya ushindani.

Lkn kama walivyosema wenzangu sometimes Dr. uwa mtata, tumesikia pande moja ya habari, ngoja tusubiri nyingine hasa yule aliyekaa 2A, na nafikiri huyu ndiye aliyekaa dirishani ambaye alitakiwa kupewa maelezo husika
 
Bora Kama kiingereza chenywe wangekimudu! Huwa wananiboa Kwa matabmshi na lafudhi ya kuigiza. Sitasahau hii, we wish you ' pilizant' flight!

Siku moja nikasikia kutoka kwa wahudumu, "On behalf of presicion air and the rest of it screw", nilichoka kabisa
 
Kama ni kweli, basi naye kachemka.

Kwa nini ang'ang'anie kuambiwa kwa Kiswahili ilhali Kiingereza anakielewa?
hayo ni mawazo yako.... si lazima kufanya utakavyo

prof is right... hatukatazwi kuomba lugha unayokua comfortable nayo... yawezekana huyo binti english yake was far worse than anything mule kwenye ndege

kama umewahi kupanda precision utajua kwamba mabinti zetu mule ndani english yao ni mbaya kuliko "i come to bukoba"
 
Na wewe haya ni maoni yako na haimaanishi uko sahishi.

kama umewahi kupanda precision utajua kwamba mabinti zetu mule ndani english yao ni mbaya kuliko "i come to bukoba"

Precision ina flight attendants wengi tu na mara zote (na nimeipanda mara nyingi sana) kuitumia hiyo airline sijawahi sikia attendant yeyote yule akiongea Kiingereza kibovu. Na nadhani huwa niko makini sana katika kubaini makosa ya ki-lugha.
 
anyway... wahudumu wengine hupata kiburi kutokana na mahusiano yao na pilots au mabosi precision...

pia kuna korosho mule ndanihazina nembo ya TBS miaka nenda miaka rudi, na ukiuliza unaambiwa mwenye hiki kiwanda ni mkuu fulani wala usihangaike tumesharipoti sana tu... anakuala na wakubwa

percision is killing itself
 
Na wewe haya ni maoni yako na haimaanishi uko sahishi.

Precision ina flight attendants wengi tu na mara zote (na nimeipanda mara nyingi sana) kuitumia hiyo airline sijawahi sikia attendant yeyote yule akiongea Kiingereza kibovu. Na nadhani huwa niko makini sana katika kubaini makosa ya ki-lugha.
anyway... typists are always right so youa re right

kwikwikwikwkwikwi
 
Mkuu, Domestic Airlines(Precision ikiwemo) zote wanatumia lugha zote mbili, nadhani shida ni kwa huyu hostess tu!

Kama inabaki kama ilivyoripotiwa ni kuwa kiswahili hakikutumika siku hiyo katika ndege hiyo kwa route husika ndio maana yote hayo yakatokea mkuu!!!!!

Litabaki kuwa tatizo la Airline mpaka wao wataposema kuwa huyo hostess alikiuka taratibu za kazi yake
 
Hawa hawana akili. Wanadhani kweli Dr Lwaitama hawezi kweli kuongeza Kiingereza? Kwa hiyo watu wote wasioweza kuongea kiingereza ni marufuku kupanda ndege zao?
Haha, kwani unadhani wanamfahamu hata kumfahamu? Watakuwa wamejua ni mnywa gongo fulani ambaye ameamua tu kuwaletea fujo. Hii nchi yetu zinaendeshwa mechanically sana, tangu Rais hadi mabalozi wa nyumba kumi style yao ni hiyo hiyo. Hawana muda wa kuupoteza kujadiliana na kuelewa hoja, wenyewe wanakimbilia kwenye matumizi ya nguvu. Kumbe wangemsikiliza Lwaitama, angewashauri ni nini cha kufanya, lakini kwa kuwa ni wana wa nyoka, hawakujishughulisha na hilo.
 
Tanzania imelala sana wakuu,sidhani kama kuna mtu anajua tz inatakiwa kuwaje baadae.nchi haieleweki,lugha tunayoijua vizuri hatuwezi kuilinda.mfano,FACEBOOK wanatoa tafsiri kwa kiswahili cha kenya ambacho hakieleweki na sio cha kweli.
 
Back
Top Bottom