Precision Air- Dala Dala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision Air- Dala Dala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mTZ_halisi, Mar 10, 2010.

 1. m

  mTZ_halisi Member

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habarini za mchana

  Jamani mimi kuna kitu kinanitatiza, nashindwa hata kuelewa. Kwa kawaida mtu unapokata ticket ya ndege as RETURN TICKET si huwa inaandika unaondoka lini na kurejea lini?

  Sasa nimekuwa nashangazwa na baadhi ya ndege eti unapofika huko uendako say unatoka DAR umekwenda MWZ ukitaka kurudi lazima ufanye confirmation. Nijuavyo mimi baada ya kusafiri ndani na nje ya nchi kama sikupiga simu kwa airline nina maana kuwa nitarudi as per schedule. Nways, nimeshaona hata ndege za nje zinazotaka confirmation uwe unarudi on the day au unabadili schedule yako... SIIKUBALI ila ndio hivo tena.

  Sasa tatizo lililonifanya niandike ni kuwa baada ya kufika MWZ kwa shuguli za kikazi, nimekaa kule nikapeleka ticket siku 3 kabla ya safari kuconfirm kuwa narudi siku hiyo iliyoandikwa. Tulikuwa group wakatupa OK kuwa tutaondoka na ndege ya Precision Air ya saa 2.35 asubuhi.

  Tunafika airport kucheck IN eti wanasema kati yetu kuna watu kadhaa hawakutakiwa kuondoka na ndege ya asubuhi wataondoka saa 8 mchana. Kwa kweli habari hiyo haikukaa vizuri masikioni. Baada ya kubishana kwa muda kwamba kwa nini watupe OK tulipoconfirm na kutupa hata ticket kuonyesha tutaondoka asubuhi kisha siku ya safari tuwe tumekatwa?

  Ati wakasema ilikuwa ije ndege ya watu 72, tumebadilisha kwa hiyo inabidi mwende mchana. Hivi unawezaje kuamua tu kubadili ndege gafla wakati unajua una wasafiri zaidi ya idadi ya hiyo ndege uliyoileta? Tukaja kugundua kuwa kuna wazungu walikuja kuconfirm baadae wakaamua kuwaweka wao kama 20 hivi na kuamua randomly kukata waswahili oh wana connection Dar... aliyekwambia hao uliowakata hawana commitment huko waendako ni nani?

  Kwa kweli Precision hiki mfanyacho si sawa. Ticket mnatutoza karibia laki 4 return kisha mnatunyanyasa kama tunapanda dala dala haiko sawa. Hapo hapo mnafika Dar mizigo imebaki Mwz hivi kwa nini mnashindwa kufanya kazi zenu sawa sawa

  HALAFU TUNASHANGAA KWA NINI HATUENDELEI TANZANIA. hivi vitu vidogo vidogo vinatufanya tuonekane hopeless na tunaendeleza upuuzi ktk maamuzi yetu ya kila siku.

  Jamani samahanini kwa habari ndefu ila iliniuma sana, na wenyewe niliwambia MWZ na hata hapa Dar. Na for me I guess I will never waste my time with your airline again.
   
 2. m

  mTZ_halisi Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  I dont know where you come from but you dont me and my preference in politics; so your comment is not relevant... AT LEAST NOT TO ME

  ATCL bado haijafa, na hata on the day ilikuwepo.
   
 3. m

  mTZ_halisi Member

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  I dont know where you come from but you dont know me and my preference in politics; so your comment is not relevant... AT LEAST NOT TO ME

  ATCL bado haijafa, na hata on the day ilikuwepo.
   
 4. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  nakumbuka nilisafiri na ATC miaka ya nyuma ya 91-96 hv,ATC walikuwa safi kupita ya leo na walikuwa wako commitment na kazi zao hadi unajisikia raha saaana!

  Lakini hv leo kwa kweli naona kuanzia Serikalini huko mpka Management ya ATC ni mbovu tu hakuna lingine zaidi ya hilo.Utawala na Management ni mbovu mbovu mbovu tu!

  Viongozi wa leo hawako long minded!
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Read me between the line and don't take this personal.

  Sihitaji kukufahamu wewe kwani ni mwiko wa JF.

  Kama una imani kuwa ATCL haijafa, basi naona unasikiliza sana Wanasiasa.

  Mwisho usishangae nikisema na mie ni mtumiaji mzuri wa Precision Air kutoka na kurudi Tabora kwani natokea Sikonge...................
   
 6. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Pole sana Mtz...ATCL ndo full kuchemsha kila siku.Ni kweli Precision air kwa kukata bogi ni wataalamu sana na mara zote kisingizio chao huwa ni kwamba "ndege tuliyoitarajia kuja haikuja hivyo imekuja ndege ndogo"Mi pia nimeshawahi kupigwa usanii huwa twice hapo KIA.

  Hatuna kimbilio kwa huduma za ndege humu nchini
   
 7. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Presicion Air ni kero na hilo halina mjadala, hyo kesi iliyokutokea mTZ_Halisi ni kesi za kawaida kabisa na hawa jamaa!

  Yaani wateja wao wa kila siku huwa hawana thamani pindi wanapokuja watu wa ngozi nyeupe!
  Inasikitisha sana!
   
 8. m

  mTZ_halisi Member

  #8
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  No insults taken Sikonge, no hard feelings from my end

  Lakini concern yangu ni kuwa vitu vingi sana tunafanya kienyeji Tanzania ndio maana kutwa maendeleo yetu duni. I must tell you ktk hiyo process ya kuounguza watu mimi sikubaki but I couldnt fight for everyone who was left.

  Ila kwa nini tushindane kwa kitu ambacho kiko wazi. Yani hadi uwe mkorofi ndio usikilizwe... Tanzania tuna kazi.. na sijui tutafika lini.
   
 9. B

  Bobby JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  mTZ, I hate to be the one telling you this. We are all political animals whether we agree or not, this is the fact and will always be. Precision ni wazembe kwa kuwa tuna serikali ya kizembe iliyozaa wizara ya infrastructures ya kizembe iliyozaa mamlaka za kizembe zisizoweza kudhibiti uzembe wa mashirika ya ndege period.

  By the way, kwa wale wasiojuwa president ni kama CEO wa Kampuni. Hivyo kama ukiwa na serious president u will also have serious central government, local government mpaka vijijini huko Namtumbo village leaders nao watakuwa serious and of course serious ATCL and the like. If the opposite is the case then same rule will apply-everything will be hopeless. I guess the second ndio kinachotokea hapa kwetu at the moment na ndio cause ya our plight.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mtz,

  Hii si makala ya kwanza kuhusu hili swala. Kuna jamaa aliandika hapa kuwa walishushwa Arusha (wakiwa tayari ndani ya ndege wamekaa kwenye viti) na Wazungu wakaingizwa kwenye ndege. Hapa lazima ufahamu kuwa huyo travel agent wa hilo kampuni lililokuwa libebe Wazungu, atakuwa mtu mmoja mzito sana ambaye hata Precion Air wanamuogopa. Hilo wala usitilie shaka na kama mtu haamini, afuatilie ajue Wazungu walikuwa wanashughilikiwa na nani safari yao. Sidhani kama Wazungu walipata wazo la kuhonga au kutumia vitisho ili wasafiri siku hiyo na nyie mbaki.

  Miaka kadhaa nyuma, nasikia meli ilichelewa kuondoka Bukoba. Watu ndani wameshonana kama magunia. Wamekaa zaidi ya saa moja na mwisho wanaona Benzi linaingia na anashuka Waziri Rwegasira??? na mizigo yake. Walipoingia tu ndani ya meli, meli ikaondoka..........

  Kuna watu ile Tanzania ni nchi yao na watafanya wanachokitaka bila kujali wala kuogopa. Sasa hata akina Precion Air wanakuwa wanawaogopa wenye nchi. Wakija na kutoa amri, basi hawana cha kusema. Sidhani kama wanafanya hivyo bila kujali kuharibu jina la Kampuni nakukimbiza wateja.
   
 11. N

  Nanu JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa tuangalie Precision na tabia ya kukata watu walio-confirm safari na wala tusiunganishe na itikadi zetu za kisiasa. Let zero in in the issue. I also encountered the same problem with Precision and I have to spent a night in Mwanza. I was distressed and disturbed by that as I couldn't make to my commitments. It was really bad and didn't reflect good on me given the matter which was ahead of me!!!! It was bad!!!!! It is a terrible experience!!
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Bobby, lazima nikiri kuwa ujumbe wangu wa kwanza nilimaanisha hayo juu. Umepakua ubongo wangu wote na kuuweka hapa vizuri sana.
   
 13. m

  mTZ_halisi Member

  #13
  Mar 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2007
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni wazembe tu kama wanakubali kuendeshwa instead of being professionals in their area. Ofcoz kama umesoma vizuri hapo juu mimi sikuweza kukubaliana na their proposal kuwa wale wana haraka kuliko mimi... Vurugu lililotokea hapo, waliniachia nisafiri but sadly kuna waliobakishwa hadi jioni.

  Nways, nimekuwa ON and OFF the forum due to some commitments na nimesoma kiasi hizo views za nyuma ila donge nililokuwa nalo lilibidi litoke...

  na baada ya kuwaeleza pale MWZ my stand, nikaja ktk ofc zao na kuwalalamikia as well kwa sababu kama walikuwa hawana nafasi wasingenipa OK ya that flight.... wewe mie nimetoka ninakotoka unizuie airport... sikubakia MWZ that day

  halafu jamani mbona thanks yangu haiko active?
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jana tu KIA yametokea haya haya watu wameconfirm safari zao kuja Dar wanafika airport wanaambiwa ndege imejaa ikatokea pata shika pale hadi ikabidi wasafirishwe hadi nairobi ambao walipakiwa kwenye ndege ya PW 719 ambayo ilikuwa inatumika na KQ. Yaani Tanzania tunasikitisha!!
   
 15. JS

  JS JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Shame!!!!!!!!!!!!
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hawa PrecisionAir jeuri yao shauri ya monopoly, wakipata ushindani kidogo tu KWISHEN!
  Mwaka juzi ilipoanza Community Airlines zile siku chache waliyumba sana, kama siyo fitna labda wangjirekebisha.

  Ndoto yangu ni pale ATCL watakapoamka usingizini angalau kuwe na ushindani kidogo kwenye eneo hili.
   
 17. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakili kuwa kuna tatizo precision air na tumepiga kelele sana juu ya suala hili lakini hakuna mabadiliko. Hatuwezi kuacha kusafiri kwa matatizo haya yanayozuilika. Nakumbuka na mimi mwaka jana tulichelewa kutoka Dsm kwenda nairobi kwa sababu abiria walikuwa wengi kuliko viti vya kwenye ndege. Ilishangaza sana kwani tuli check in, na tuliingia kwenye ndege wote na hapo ndo abiria mmoja akakosa kiti. Wakamshusha dada mmoja mtanzania badala ya mzungu aliyekuwa na makosa. Mzozo ulituchelewesha na nilichelewa ndege ya kuunganisha pale nairobi. Niwaombe wadau wa forum hii tufanye mkakati wa kuwasiliana na uongozi wa shirika hili la ndege ili wajirekebishe. Sijui mkakati huo utatekelezwa vipi ila ndo wazo langu ... kufikisha kilio chetu kwa uongozi moja kwa moja.
   
 18. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya matatizo ya kukata pax waliokuwa confirmed ni la siku nyingi sana na halitakwisha kwa PRESICION AIR. Kuna ndugu yangu alifiwa na jamaa yake, alipofika airport akaambiwa ndege imejaa. Lakini akaitwa kwa nyuma na kuambiwa atoe kitu kidogo kusudi asafiri. Na alipotoa, abiria aliyekuwa right kusafiri muda huo, alikatwa na huyu jamaa akasafiri.. Je huu upuuzi utakwisha?
   
 19. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  this is not just with Precision air alone..even the so called Pride of Africa KQ ni washenzi sana..kuna siku niliwapa zao hamsini mpaka they had to book me on another flight watake wasitake useless kabisa!!!
   
 20. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Pole mtoa mada
   
Loading...