PPRA Inaisimamia Public Procurement Act kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PPRA Inaisimamia Public Procurement Act kweli?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Katikomile, Jan 11, 2010.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Baada ya utafiti kuonesha kwamba rushwa nyingi/kubwa kubwa zilikuwa kwenye manunuzi(Procurement of public goods and services) ya umma, serikali iliamua kuanzisha sheria ya Manunuzi, Public Procurement Act ikifuatiwa na Regulator wake ambaye ni Public Procurement Regulatory Authorities. Nionavyo mimi hii PPRA wanaingiliana kikazi zaidi na ofisi ya Controller and Auditor General (CAG) na Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB).

  Je ni kweli Rushwa imepungua kwenye manunuzi au ndio imeongezeka zaidi, What are PPRA exactly doing?
   
 2. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  PPRA nadhani inasimamia PPA vizuri ila tatizo ninaloliona ni rushwa bado haijaisha na wazawa bado hawapewi kipaumbele.

  Hizo anti bribery policy za kuandika tu hazisaidii inatakiwa hatua za kimkakati ambazo hata kwenye tender document si lazima zitajwe. rushwa badi ipo pale pale, tena nene zaidi.

  wazawa pia wameachwa kabisa, kipengele cha kupendelea wazawa kinaachwa na maslahi binafsi yanatawala. unakuta mzawa yuko juu kidogo eg 100m kwa 102m, hapo mzawalazima afikiriwe tofauti maana kwanza unamuwezesha na pili hela yake inabaki hapa ila hicho sijakiona bado.

  PPA yenyewe ukiisoma ni nzuri ila bado sijaona kama inasaidia
   
 3. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  PPRA inaelekeza kuunda kwa Procurement Management Unit (PMU) katika kila ofisi/idara ya umma, na ninafikiri hii PMU inakuwa na members wa kudumu! Sasa je, si ni rahisi kuwaonga hao watu make wanajulikana.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu kwanza hata uwepo wa PPRA bado hautiliwi maanani sana na baadhi ya taasisi za umma. Kwa mfano PPRA wamekuwa wakifanya kitu kinaitwa procurement audit katika hizi taasisi na kugundua mapungufu mengi tu ikiwemo manunuzi yasiyofuata sheria (Public Procurement Act of 2004 and regulations of 2005). Lakini kwa uzoefu wangu sijaona any disciplinary actions zikichukuliwa.

  Na hata suala la kuundwa kwa PMU kwenye hizi taasisi za umma ni kama kiini macho kwani huenda hata hizo PMU hazijifanyi kazi zake kama sheria inavyotaka mwisho wa siku watu wanajinunulia kwa jinsi wajuavyo maana wanajua kabisa kuwa kama wakifata sheria inavyotaka hawatapata 10%. So rushwa is there to stay unless wale wanaopindisha sheria wanabanwa ili kuwa mfano kwa wengine.
   
 5. E

  Edo JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwa maoni yangu, PPRA wamefanya mengi mema na wanastahili pongezi kwani kabla ya hapo, hali ilikuwa mbaya zaidi. Sheria inakipengele cha local preference na kinatumika vizuri, japo kinatugharimu maana kwenye miradi mikubwa pale tunapotumia hii sheria kumpa "mzawa". Lakini ni bora tukubali hiyo gharama tujenge uwezo wa watu wetu. PPRA wamewezesha tenders kuwa wazi kwa kila mtu-tatizo letu sisi ni uvivu wa kujaza yale madocument makubwa ila nasi tuhsindane na wenzetu-tunaishia kulipua mataokeo yako tunakuwa-non -responsive-kisha tuaanza mjaungu! Ni vema tupongeze pale panapostahili na tuwaelekeze wapi wakaze buti kuboresha, tuache kulalamika tu kila siku jamani.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Mkuu; PPRA is good lakini nadhani ma;pungufu hapa kwetu yako sehemu tatu

  1. supply chain management systems kwa ujumla - ukichunguza hata rushwa, na mambo mengine yanachangiwa na uwezo mdogo wa wataalam wetu kwenye planning, monitoring and operationalization ya mambo. an effective scms huondoa sana possibilities za corruption na disputes
  2. PMUs nyingi hazina auditing matokeo yake zinafanya kazi kama miungu watu
  3. tunahitaji procurement audit board na iwe na relevant technical people kutoka kada zote na si ma-engineers pekee

  PPRA inaweza kufanya makubwa zaidi kama hayo hapo juu yatakuwa acknowledged
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,182
  Trophy Points: 280
  Tujiulize
   
Loading...