PPF acheni kutapeli wafanyakazi

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,542
Kama siyo kunipigia simu ndugu yangu jana alikuwa anaingia mkenge wa kujiunga na PPF. Bahati nzuri alinipigia simu ili kuniomba ushauri maana kulikuwa na form mbili ya NSSF na PPF, nikamwambia kuwa kama anataka kulia basi ajiunge PPF.

Akaniuliza kwanini nikamwambia kuwa sikuwahi kumsimulia ukatili niliofanyiwa na PPF wa kudhulumiwa mil 10 eti hadi nifikishe miaka 55 ndo nichukue, akaniambia kuwa kuna wenzake wanne walilaghaiwa na staff wa PPF kisha wakajiunga na mfuko huo wa hovyo kabisa.

Kupitia jukwaa hili nataka niwaambie PPF kuwa lenye mwanzo halikosi mwisho, mnajiona wajanja Sana sasa hivi kwa kuendelea kula jasho la wanyonge. Lakini nawahakikishia kuwa shirika lenu litafirisika kabisa, hakuna mjinga wa kukubali kujiunga na nyie.

Endeleeni tu kula hayo mamilioni mliotudhulumu ila nguvu ya karma lazima itawashukia tu.Mtabaki historia kuwa na nyie mlipata kuwepo. Acheni kuwatapeli wafanyakazi wapya kuwa mnatoa fao la kujitoa wakati ni uongo.
Mtauza hadi majengo kwa kukosa wateja, siku yaja, dunia haihitaji base haraka.
 
Back
Top Bottom