Powertiller & tractor Kubota

sassy girl

Senior Member
Sep 19, 2020
112
172
Wale wanaohitaji kuzielewa power tiller karibuni.

Uzi huu utatumika kujibu maswali na majibu ya wadau ambao wamekua wakiniuliza mara kwa mara.

Kuna aina kuu mbili za power tiller yaani Long hand power tiller na Short hand power tiller.

LONG HAND POWER TILLER
Long hand power tiller ni zile zenye mikono mirefu ya kuendeshea kama ville Siam Kubota, Boar, Toyo, Myanmar(hazipo nchini), Swami, N.k

Power tiller hizi zote huwa ni 14 HP, 4 gear na magurudumu ya mbele makubwa kiasi. Powetiller hutoka ikiwa na cage wheel, disc plough na leki kwaajiri ya kupigia level na kuokota.

Bei zake nchini ni million 5 au pungufu kwa aina nyingine zote( India and chinese) bila tera na 7.5 million ikiwa complete. Hazidumu sana kwani huanza kusumbua gear box na engine ndani ya mwaka mmoja au miwili toka kununuliwa. Zinadumu kwa miaka 7 - 10 zikitunzwa vizuri.

Zinafaa kwenye kilimo cha mahindi na kilimo kingine kinachofanana na hicho.

Bei ni 9.5- 10 Million kwa Siam Kubota (Japan) bila tera na 12-14 million complete. Hudumu kwa muda mrefu up to 15 years na inaweza kufanya kazi miaka 3 bila serious service ya engine wala gear box. Shida ya hizi mashine ni ghalama kubwa zaa spea.

Hizi hukimbia sana na hufanya kazi kwa uharaka zaidi. Vile vile ni nyepesi kuopoa kama zikikwama kwenye tope wakati wa kuvuruga. Zinafaa kwa matumizi yoyote ya kilimo na katika mazingira yoyoye isipokuwa Yale yenye visiki kwani jembe lake si imara sana.

SHORT HAND POWER TILLER
Short hand power tiller ni zile zenye mikono mifupi ya kuendeshea kama vile Amec, Kubota(ndogo), Toyo, Greeves, Jiang Dong (JD), Zhong Hou (ZH) n.k.

Power tiller hizi huwa na 13 HP mpaka 20 HP kutegemeana na uhitaji wa mteja. Bei zake huanzia million 3.5 bila tera mpaka million 7 ikiwa full.

Power tiller hizi hutoka ikiwa na disc plough,Rotavator na cage wheel za kwenye maji.

Machine hizi huwa na gia 8 na hazikimbii sana lakini zinanguvu kubwa. Zinafaa kwenye kilimo cha aina yoyote. Tatizo kubwa la hizi machine ni kufa haraka yaani hazikai zaidi ya miaka 7 kama zinafanya kazi kweli kweli kweli picha na mawasiliano email+91 9990874397

somethingealspecial8@gmail.com



JamiiForums-211493954_408x230.jpg
IMG-20200928-WA0000.jpg
Screenshot_20200928-181910~2.jpg
Screenshot_20200928-182026~2.jpg
Screenshot_20200928-182009~2.jpg
Screenshot_20200928-182053~2.jpg
Screenshot_20200928-202815.jpg
Screenshot_20200928-181858~2.jpg
 
Back
Top Bottom