Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Ajizi nyumba ya njaa, wakati baadhi ya watu ndani ya chadema wakifikiri mashambulizi yanatoka nje ni wakati waelewe sasa misuguano ya kimadaraka miongoni mwa 'makamanda' inaendelea na wengi watapotezwa au wakiona mbali waachane na siasa.
Tulio na kumbukumbu tunakumbuka yaliyomtokea Chacha Wangwe (RIP) na yaliyotaka kuwatokea Zitto Kabwe na wenzake na mwaka jana Dr.Slaa ni dhahiri kama wasingeshitukia mchezo mchafu wangepotezwa kwa kigezo kuwa ni 'wasaliti'. Lazima ieleweke sasa ndani ya chadema kuna makundi yanayosuguana,yanapigania 'tonge' na 'ufalme'. Kuna wakuja ambao kimsingi wana ukwasi na wanaona wao ndio wamesababisha ongezeko la wabunge na madiwani na kuna kundi la 'bakulutu' hawa wanaamini jasho lao ndilo limeifikisha chadema ilipo sasa.
Hii ni dhambi,damu zilizopotea bila hatia zinalia,zitalia na wahusika watacharazana bila kujua. Ni wakati wa kama chama wakae chini wajue ya kwamba hila hazifikishi mtu mbali. Umafia huu ndani ya chadema lazima udhibitiwe,kwa nje tunadanganywa kuna maelewano lakini si kweli kuna shida kubwa.