Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Tabia ya BUNGE letu kujigeuza bodi ya wakurugenzi ya serikali inaudhi sana. Wabunge wanakimbizana na posho wanazolipwa wajumbe wa bodi za taasisi na mashirika ya UMMA! Tutafika kweli? Ni vema wakakaa wakaamua ni mshahara kiasi gani wanataka walipwe kuliko kuendelea kukwapua pesa za umma kwa mtindo huu huku wakikwepa kodi.
 
hivi ungekuwa wewe je?
obvious the answer sitoweza kuchukua
and after all haitaweza kutokea kwa sababu ninapenda career yangu regardless of what, sitakimbilia ubunge kwa sababu ya posho ... Ila ni wajibu wangu kulizungumizia hili kwa sababu linatokana na paye yangu na vyanzo vingine vya kodi ya serikali yetu wakati kuna mambo mengi tu ya maendeleo yanaretard..
Nipe sababu ya msingi ya mbunge kuongezewa posho na kumuacha mwalimu akinyanyasika na tgs c,d huko
 
vipi mkuu hufatilii bunge mbona chadema walisha piga tangu ikiwa tzs 70,000...

mkuu ruta,
tuache unafiki chadema walipiga kelele watu tukawa tunawabeza vipi leo tena tuwalaumu...
Je wewe kama mwananchi mlala hoi ulichukua jukumu gani kupiga au kuwaunga mkono chadema...
umenena vyema mkuu lakini waliziacha hizo posho na wana mikakati gani yakuigomea posho pamoja na kuwa zinaingia benki moja kwa moja
 
Naona katibu wa mbunge hapa karagwe akiona watu wengine anatema makohozi. Posho hizi bwana
 
Wangelipwa hivyo na wao wakafanya walichotumwa na wananchi ingekua bora
ila vilazaaaaaaaaaaa
wanalipwa na kula rushwa na wizi hawaachi
katiba tu ndio dawa yao
 
I reckon they deserve such handsome emoluments (given) the tremendous work they perform as part of their parliament stints. For instance, they have recently debated and endorsed a Constitutional Bill pending President's sanction. Additionally, they have carried out inquiry into Jairo's scandal and boldly proposed on stern measures to be taken against the accused which might include losing him a job. All these remarkable jobs need to be appreciated and anything less than Tshs 200,000 a day may not suffice.
 
Tz kuendelea itakuwa ngumu.Itakuwa ni nchi yenye watu wenye mapesa lakini isiyo na maendeleo.
 
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.

Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.

Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.

Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?

Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.

Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.

Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao


source: Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu taarifa ya kupandishwa posho za Wabunge kimyakimya - Wavuti
 
Bado naamini kuwa wafanyakazi wangeweka mgomo wa kweli kuhusu kima cha chini wangepewa.Serikali ina pesa bana.Wabunge wakidai wanaongezewa fasta bila mikinzano hasi.Wafanyakazi wakidai mkuu wa nchi anakimbilia kwa wazee wa CCM dar kuponda.HOVYO KABISA
 
I reckon they deserve such handsome emoluments (given) the tremendous work they perform as part of their parliament stints. For instance, they have recently debated and endorsed a Constitutional Bill pending President's sanction. Additionally, they have carried out inquiry into Jairo's scandal and boldly proposed on stern measures to be taken against the accused which might include losing him a job. All these remarkable jobs need to be appreciated and anything less than Tshs 200,000 a day may not suffice.

Sasa huo si niwajibu wao kama wabunge?!Inahusiana vipi nakujiongezea posho kubwa kiasi hicho tena kimyakimya.
 
mbona kama takwimu haziko sawa? Mi napata ongezeko la %185 ukichukua posho ya zamani via-a- vis posho hii mpya
 
mbona kama takwimu haziko sawa? Mi napata ongezeko la %185 ukichukua posho ya zamani via-a- vis posho hii mpya

Mi mwenyewe anko anasema ameongezewa kwa asilimia 185. Sasa hizi za hapa sijui zimepatikana wapi.
 
Naona hesabu ni janga la kitaifa!

"Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya Ofisi za Bunge.

Hizo hesabu si sahihi .........200,000/70,000x100%=286% na sio 154%

Ongezeko hapa ni shilingi 130,000 (yaani 200,000 ukitoa 70,000). Ongezeko hili ni asilimia 186 (i.e. 185.7 = 130,000x100/70,000). Hiyo 154% sijui mwandishi anaipataje!

Kama lengo ni kusema kiwango kipya ni mara ngapi ya kiwango cha awali....basi angeweza kusema "kiwango kipya cha posho ni zaidi ya mara mbili (au karibia mara tatu) ya kiwango cha awali" na kama ni katika muktadha rasmi sana au ule wa kitaaluma zaidi angesema "kiwango kipya cha posho ni mara 2.86 ya kiwango cha awali"
 
Back
Top Bottom