Posho za wabunge zapanda kimyakimya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tindikalikali, Nov 28, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Nimekubali hakuna biashara inayolipa vizuri kwa sasa kama ubunge. 200,000 kwa siku? Enough is enough!

  [​IMG]
  Kikao cha Bunge kikiendelea mjini Dodoma


  ZAPANDA KUTOKA SH70, 000 HADI 200,000, NI ZAIDI YA ASILIMIA 150
  Fredy Azzah

  HUKU mjadala wa kufutwa au kwa posho za wabunge na watumishi wengine wa Serikali ukiwa umefifia, posho za vikao (sitting allowance) za wabunge zimepanda kutoka Sh70,000 kwa siku hadi Sh200,000, imefahamika.

  "Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya Ofisi za Bunge.

  Kutoka na ongezeko hilo, kwa sasa kila mbunge atakuwa akilipwa Sh80,000 ikiwa ni posho ya kujikimu (perdiem) anapokuwa nje jimbo lake, posho ya vikao (sitting allowance) Sh200,000 na mafuta ya gari Sh50,000 kila siku, ambazo jumla yake ni Sh330,000 kwa siku.

  Kutokana na ongezeko hilo, Bajeti ya Bunge kwa ajili ya posho za vikao vya wabunge imepanda na kufikia Sh28 bilioni kwa mwaka.

  Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu siyo msemaji wa wabunge, bali Ofisi ya Bunge.

  "Ni nani kawapa hizo taarifa bwana, au ni vyanzo vyenu vya habari?" alihoji Dk Kashililah.

  Baada ya kuelezwa kuwa taarifa hizo zimetoka kwenye vyanzo vyetu vya kuaminika alisema "Hao wana utaratibu wao bwana, labda mtafute Spika ndiye msemaji wa Wabunge."

  Juhudi za kumpata Spika, Anne Makinda kutoa ufafanuzi wa suala hili, hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita wakati wote bila kupokewa hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakujibu. Hata simu zote za Naibu wake, Job Ndugai hazikupatikana.

  Hata hivyo, Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe alisema kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na wabunge kuwa wanalipwa mishahara midogo kulingana na kazi wanayofanya.

  Alisema endapo wawakilishi hao wa wananchi wangekuwa wanalipwa mishahara inayolingana na kazi wanayofanya, kusingekuwa na sababu ya kuongezeka kwa posho hizo.

  "Ninachosema mimi, siyo wabunge peke yao, lakini watumishi wote wa umma wanalipwa mishahara midogo sana mimi binafsi sitegemei posho za Bunge, kabla ya kuingia bungeni nilikuwa nimefanya kazi kwa miaka 14 na nilikuwa napata mshahara mzuri tu," alisema Filikunjombe.

  Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema amezisikia taarifa hizo za kuongezeka kwa posho lakini siyo kwa undani. Hata hivyo alisema hakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza suala hilo.

  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema walivyokuwa wakipinga posho hizo wakati zilivyokuwa Sh70,000 waandishi wa habari walichukua suala hilo kama ajenda ya Chadema, hivyo kupandishwa kwa posho hizo ni matokeo ya watu kuwapuuza walivyokuwa wakizipinga.

  "Msimamo wetu sisi tulishautoa tangu wakati posho zikiwa Sh70,000 wakati sisi tukipinga hizi posho waandishi wa habari na Watanzania mlichukulia suala hili kama ajenda ya Chadema, sisi wenyewe tupo wachache bungeni, tulichotaka ni kuonyesha jinsi fedha za Watanzania zinavyotumika vibaya," alisema na kuongeza:

  "Achilia mbali hizo 200,000 za wabunge kuna watu huko serikalini wanalipwa mpaka Sh400,000 au Sh1 milioni kwa siku nyie ulizeni."

  Alipoulizwa kama amechukua posho hiyo ya Sh200,000 alisema hajafanya hivyo kwa sababu hazifuatilii.

  "Sijui hata kama zimeanza kulipwa au la kwa sababu huwa sizifuatilii na haka kama suala la posho hilo zilijadiliwa wakati wa vikao vya mwanzo mimi sikuwepo kwa sababu tulikuwa kwenye kesi yetu Arusha na bungeni tulikuja mwishoni wakati wa Muswada wa Katiba," alisema Mbowe.

  Ongezeko hili la posho za wabunge limekuja wakati Watanzania wakiendelea kuishi kwenye maisha magumu yanayochangiwa na mfumuko wa bei ambao mpaka mwisho mwa Oktoba ulikuwa umefikia asilimia 17.9.

  Pia ongezeko hili limekuja wakati Watanzania wakiwa na matumaini ya posho hizi kupunguzwa baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza bungeni kuwa Serikali imekubali pendekezo la kutafakari na kuziangalia upya posho mbalimbali wanazolipwa wabunge na watumishi wote umma.

  Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali alisema kuwa hawezi kuzungumza chochote juu ya posho hizo kwa kuwa hajapata barua rasmi juu ya kupanda kwake.

  "Sijapata barua yoyote, nikiuliza na kupata majibu kwa wahusika nitakuwa na uhakika na nitakupa maoni yangu na msimamo wangu vizuri kabisa, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote," alisema Mkosamali.

  Juni 7, mwaka huu Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Zitto Kabwe, aliwasilisha barua Ofisi ya Bunge akikataa posho akisema watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.

  Zitto alisema posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.

  Alisema kitendo cha Waziri Mkuu kueleza kuwa watatafakari na kuangalia upya na kwamba suala la posho ni sera ya taifa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ni ishara ya kiongozi huyo wa juu kukubali wazo la Chadema na safari ya kufuta posho hizo.

  Awali, mara baada ya Chadema kutangaza msimamo huo, Spika Makinda alipinga uamuzi wa kususia posho akisema suala hilo lipo kisheria na kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuamua kuliondoa.

  Alisema wabunge wa Chadema wataendelea kulipwa posho za vikao kupitia akaunti zao za benki na watatakiwa kusaini fomu ya mahudhurio ya Bunge, vinginevyo watajiweka katika wakati mbaya.

  Hata hivyo, akihitimisha hoja za wabunge katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi ya ofisi yake na zilizo chini yake juzi, Pinda alisema suala la posho lipo kwenye mchakato wa kuangaliwa upya.
   
 2. mwl frank

  mwl frank Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  kwa wabunge ni sawa kwa sababu wao wananunua 'hewa'ya peponi!watumishi,wakulima wanapata ya bure yaani ya Mungu! INATISHA SANA.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  watatoana roho, ndo maana hawataki wenye nchi waandike katiba yao! wanajua hiyo kitu itapunguzwa ilingane na posho ya waalim.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  kwenye hili hakuna chama tawala au cha upinzani........wote wanashabikia kulipora taifa..................huku hakuna vigezo vya kulinganisha mapato ya wabunge na watendaji wengine serikalini..................................kama ni kubana mkanda si tubane wote lakini wabunge hawataki kwa sababu bunge lao wamelitukuza mithali ya Mwenyezi Mungu pale walipoliita bunge tukufu na wao ni waheshimiwa na sisi wengine hatuna hiyo taswira......ni walalahoi ila muhimu sana katika kuhalalisha ulaji wao kila baada ya miaka mitano
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Ubunge raha
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Wizi mtupu huu!! Nadhani tulifute Bunge, kwanza halina tija yeyote zaidi ya kufuja fedha zetu...
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ila ukiangalia in total ni kama 28mil kama watafanya kazi tuliowatuma si hela nyingi sana ukichukulia ughali wa maisha uko juu.

  Ila nao ilo ongezeko dah kubwa sana.

  Inaponiuma ni pale ata wale ambao wamekuja bungeni kuuza sura nao wanapata wakati output yao ni zero kwa Taifa kupitia bungeni.

  Kuna haja ya kuadjust kidogo
   
 8. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  teh teh teh waliohojiwa hapo juu wote wanababaisha katika kujibu kuhusu ongezeko la posho.Ama kweli pesa ndo kila kitu.Hapana shaka ndo maana wafanyakazi hawajalipwa mishahara yao ili kufidia kwanza ongezeko hilo la posho kwa kuwa hata kwenye bajeti 2011/2012 hakukuwemo na ongezeko hilo
   
 9. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Ni 28bilioni si 28mil na hii ni pesa nyingi.
   
 10. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Bunge la Tanzania limejaa majambazi wa mchana kweupe wanakwiba huku wakilindwa na obsolete laws.
   
 11. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  HII NI HATARI.....KATIBA IJAYO IELEZA NAMNA WABUNGE WATAKAVYOLIPWA MISHAHARA NA POSHO , C KUJIPANGIA KAMA WANAVYOFANYA SASA'''':lol::lol:
   
 12. S

  Smarty JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  duh hii nchi noma sana ...hakuna usawa kabisa viongozi wetu wabinafsi sana..yaani unachukua 330 kwa siku wakati mwenzio hiyo anaipata kwa mwezi au mwaka mzima.. viongozi wote ni wezi tu. Suruhu ni kuingia barabarani tu. Hivi hii nchi haiwezi kuwepo bila bunge kuwepo??? Bila wabunge tunaishi bana ...hawa jamaa vipi?
   
 13. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,371
  Trophy Points: 280
  Tutakutana nao 2015, ole wao! Watanikoma!
   
 14. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwenye red ni 28 bilion
   
 15. S

  Smarty JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  kote huko?? We niaje?? Watakuwa wameishakwiba shilingi ngapi??
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nilitegemea wabunge wa Magwanda wangepinga ongezeko hili la kutisha lakini kimya sioni tofauti kati ya magwanda na Magamba wote sawa.
   
 17. w

  wakupita Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Hawa jamaa wana uhalali gani wa kumhukumu jairo kwamba analiibia taifa ?,they have got no moral obligations to judge others of moral decay!
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vyama vyote vya siasa vimekubaliana posho zipande kutoka Sh70,000 hadi 200,000, kwa siku?
   
 19. Bongo Pix Blog

  Bongo Pix Blog JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamna noma 2015 waongeze nafasi za wabunge zifike hadi 10,000 au kila watu 3000 mbunge mmoja alafu unakaa vipindi viwili tu kwa mtindo huo tutakuwa tunagawana keki ya taifa. Maana huko ndiko kwa kuchumia au kutajirikia kwa wabongo.
   
 20. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,371
  Trophy Points: 280
  sasa unafikiri tutafanyaje? Vita au?
   
Loading...