Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 27, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,597
  Trophy Points: 280
  Spika Sitta,Waziri MKuu Pinda watofautiana kuhusu TAKUKURU


  [​IMG]

  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mbunge Silaju Kaboyonga na Spika Samweli Sitta wakijadili jambo nje ya Bunge jana Mjini Dodoma.

  Na Mwandishi Wetu,Dodoma
  Mwananchi
  10/27/2009

  MSUGUANO kati ya mihimili miwili, Bunge na Serikali umejitokeza baada ya Spika Samuel Sitta na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutofautiana kuhusu hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwahoji wabunge kuhusu tuhuma za watunga sheria hao kulipwa posho mara mbili.

  Wakati tofauti hizo zikijidhihirisha kwenye kikao cha faragha cha wabunge kilichofanyika ukumbi wa zamani wa Bunge unaojulikana kama Pius Msekwa, mmoja wa vinara wa vita dhidi ya ufisadi, Dk Harrison Mwakyembe aliongea na waandishi wa habari na kushutuma vikali kitendo hicho cha Takukuru akikielezea kuwa ni cha kisasi na kusema kamwe hatakubali kuhojiwa.

  Hatua ya Takukuru kuhoji wabunge hao imetokana na malalamiko kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kulalamikia mwenendo wa Kamati za Bunge kudai posho mara mbili kwenye idara na taasisi za serikali. Bunge hugharimia posho kwa ajili ya shughuli za kamati zao zinazosimamia vyombo hivyo, lakini baadhi ya wabunge walidaiwa kuendelea kupokea posho mara mbili, hali ambayo iliilazimisha Takukuru kuanza kuwahoji wanaotuhumiwa kufanya hivyo.

  Lakini wabunge, akiwemo Spika Sitta, wamekuwa wakipinga kitendo hicho na jana serikali ilionekana kuunga mkono wabunge kuhojiwa huku Bunge likiendelea kupinga.

  Tofauti za watendaji hao wawili wa serikali na Bunge zilizijitokeza jana mchana wakati wabunge walipokutana kwa faragha kupokea taarifa ya agenda zilizopitishwa na Kamati ya Uongozi kwa ajili ya kujadiliwa kwenye mkutano unaoendelea mjini hapa.

  Suala la kuhojiwa kwa wabunge lilizua mjadala mkali kiasi kwamba mkutano huo, ambao awali ulikadiriwa kuwa ungechukua takriban saa moja kuanzia saa 5:15 asubuhi, ulimalizika karibu saa 8:00 alasiri.

  Katika mjadala huo, mbunge wa Dole, Juma Suleiman N’hunga (CCM) alienda mbali na kusema chombo kilichopaswa kuwahoji wabunge ni Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge na sio Takukuru ambao ni mhimili mwingine wa dola.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo, kitendo cha Takukuru kuwahoji wabunge ambao ni mhimili wa Bunge ni ukiukwaji wa katiba na akapendekeza Takukuru ikatazwe kuendelea na zoezi lake la kuwahoji wabunge.

  Mbunge mwingine aliyechangia mjadala huo mzito alipendekeza Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani na mkurugenzi wa Takukuru, Dk.Edward Hoseah kama ilivyotokea kwa taasisi kama hiyo nchini Kenya.

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge walitofautiana katika suala hilo, huku baadhi wakihoji sababu za chombo hicho kukaa kimpya wakati Basil Mramba alipohojiwa na kushitakiwa mahakamani.

  Mramba, aliyekuwa waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya tatu na baadaye waziri wa miundombinu katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi iliyoiingizia serikali hasara ya mamilioni.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho zimedokeza kuwa Mramba alitumia mkutano huo kuelezea kwa kirefu namna alivyohojiwa na Takukuru katika mazingira ya kudhalilisha tena na vijana wadogo ambao hawakustahili kumhoji.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo naye alitumia kikao hicho kuelezea masaibu yaliyomkuta wakati alipoitwa na Takukuru kutoka jimboni kwake hadi Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa nne.

  Shelukindo alihoji inakuwaje Takukuru ianzishe uchunguzi huo sasa wakati ambao Bunge linatakiwa kupokea utekelezaji wa maazimio yake ambayo baadhi yanataka DK Hosea awajibishwe.

  Pamoja na Spika kueleza kuwa tayari ameandaa mazingira mazuri yatakayotumika kuwahoji wabunge hao ikiwamo kuipatia Takukuru ofisi kwenye jengo la Bunge mjini Dodoma na Dar es Salaam Salaam, bado baadhi ya wabunge walipinga.

  Kutokana na michango ya wabunge wengi kuonyesha dhahiri kukerwa na kitendo cha Takukuru, Spika Sitta alitangaza katika kikao hicho kuwa kuanzia hiyo jana mahojiano hayo yamesimamishwa.

  Lakini Waziri Mkuu akaonyesha kutokubaliana na maamuzi hayo ya spika na kueleza kuwa uchunguzi huo wa Takukuru utaendelea kwa kuwa ofisi ya Rais Ikulu ndio ambayo imeagiza ufanyike.

  Waziri Mkuu Pinda alisisitiza kuwa kinachotakiwa kufanywa si kusitishwa kwa uchunguzi huo bali ufanyike katika maeneo yenye staha na katika mazingira ambayo hayawadhalilishi wabunge.

  Mkutano huo haukuelezwa pia kama ni lini ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge itawasilishwa bungeni katika mkutano huu wa 17 hali ambayo inazidisha usiri na uzito wa mjadala kuhusu kashfa ya Richmond.

  Wakati hayo yakiendelea, mbunge wa Kyela, Dk Mwakyembe aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo la Takukuru kuendesha uchunguzi huo ni kuwafunga midomo wabunge wasishikie bango kashfa ya Richmond.

  Dk. Mwakyembe, ambaye aliiongoza kamati teuli iliyochunguza kashfa ya Richmond, alisema binafsi hawezi kukubali kile alichodai ni upuuzi wa taasisi hiyo kutaka kuwahoji wabunge katika kipindi hiki tete cha Richmond.

  Dk Mwakyembe aliishangaa taasisi hiyo akiitaka ijichunguze kwanza kabla ya kuamua kuwachunguza wabunge kuhusu malipo ya posho mbalimbali, huhusan posho za chakula.

  "Takukuru waliponipigia simu kunihitaji, nilikataa kwa sababu kwa mazingira yenyewe hili zoezi linaendeshwa kwa malengo ya kuwafunga midomo wabunge kuhusu sakata la Richmond mimi nilikataa," alisema.

  Alisema kuwa malipo hayo ya posho yamekuwepo miaka mingi na yamekuwa yakitengewa bajeti katika fungu la kuwakirimu wageni na haoni chembe yoyote ya rushwa katika suala la malipo hayo.

  Dk.Mwakyembe alisema alikataa wito huo wa Takukuru kwa kuwa ulikuwa unakwenda kinyume na haki na madaraka ya Bunge na pia ni kinyume cha vifungu 100 na 101 vya katiba ya nchi vinavyotoa uhuru kwa Bunge.

  Sisi wabunge tunasubiri utekelezaji wa maazimio ya Bunge na moja ya maazimio hayo yanataka mtendaji mkuu wa Takukuru awajibishwe kwa kutofanya vizuri kazi yake katika uchunguzi wa Richmond," alisisitiza Mwakyembe.

  "Alisema mchakato bado haujakamilika na wewe unaenda kuwahoji wale wanaokuhoji... hilo halikubaliki na ni kinyume cha utawala wa sheria mimi ni mwanasheria mwalimu wa sheria siwezi kukubali upuuzi huu."

  Dk. Mwakyembe aliitaka Takukuru kumpeleka mahakamani kama ana makosa na kutamba kuwa hata ikifanya hivyo ataibwaga mahakamani na kusisitiza mafisadi wasitumie vyombo vya habari kumchafua.

  Tukiaanza kuongelea mambo ya posho Takukuru wenyewe ndio vinara wa kutoa posho…wametufanyia semina mara mbili mimi; naishi Dar es salaam, wanatulipa posho ya kulala wajichunguze wao wenyewe kwanza, alisema.

  Mwanasiasa huyo aliitaka Takukuru kuacha kukimbilia vitu vidogovidogo na badala yake ishughulikie mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwa kasi hii ya jamaa kukabana koo basi lazima nyumba iungue kwa maji ya moto .Sina comments ila naangalia sarakasi hizi .Ikulu imeamuru kama alivyosema Pinda kuhusu posho ila imeshindwa kuamuru kwenye mambo mengine ?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hawakustahili kumhoji kwa sababu gani? Kwa sababu wadogo? Kwa sababu rank yao haiwaruhusu kumhoji mtu wa rank ya Mramba? Kwa sababu hawana security clearing? Kwa sababu wamezaliwa baada ya Azimio la Arusha?

  Waandishi wa habari wa bongo ovyo!
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we will know it all huyu Mwakyembe ni another generation ya mafisadi hana lolote makelele tu ..anapayuka kuhusu Richmond kumbe na yeye alikuwa na kampuni yake kwenye dili hizo hizo za umeme wa dharura..aaaahgggggg .asihojiwe yeye nani kwani?
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  sinema hazishi siasa za bongo.
   
 6. t

  tk JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wezi wakubwa. Statement zote hizo ni za kifisadi. Sasa inaonyesha wazi kuwa hawa wabunge wapambanaji ni waongo wakubwa. Malalamiko yao hayatokani na uchungu wa nchi bali ni kuwa wao hawakupata nafasi ya kula kama hao wanaowatuhumu. Ushahidi ni huu kuwa walipopata nafasi ndogo tu ya kudhibiti mashirika, hapo hapo wakaanza kula bila kunawa. Jee ingekuwaje kama wangekuwa mawaziri au wakuu wa mashirika. Siwangewazidi hata hao akina Chenge etc?

  Hivi kwa akili yao ilivyokuwa fupi walidhani kinga ya mambo yao ni kuanza wao kuwachunguza wengine? Hii ni urgument ya ajabu ambayo hitegemei toka kwa wanaojiita wasomi.

  Solution ni waburuzwe tu mahakamani. Hakuna kuoneana haya.
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  In a perfect world, PM na Spika kugongana ni suala jema sana kwa maendeleo ya nchi, lakini kwa bunge letu kupitisha kila maamuzi ya serikali ndiyo kumepelekea hapa tulipo leo, labda tunahitaji migongano hii zaidi.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Oct 27, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Waheshimiwa Mramba na Yona walihojiwa na hatimaye wamefikishwa Mahakamani, hakukuwa na vikao vya kuwatetea maskini! Hawa "wapambanaji" wameguswa eti wanadai ni vitu vidogo na vimeanza siku nyingi! Wakumbuke kuwa 'two wrongs can not make a right!' Hivi kama ujambazi umeanza siku nyingi kwa hiyo sio tatizo kama ukifanywa sasa hivi? Kwani kosa la jinai lina expiry date jamani? Huyo Mwakyembe anahofia nini kuhojiwa kama anaheshimu sheria? Amesahau kwamba kinga haimhusu mhalifu? Hongera sana Pinda, wahojiwe hawa "wapambanaji!"
   
 9. b

  bambumbile Senior Member

  #9
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Porojo za Dk. Mwakyembe
  • Atamba anajua sheria, ataibwaga TAKUKURU

  na Sauli Giliard, Dodoma

  MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, jana aliwashangaza waandishi wa habari wanaohudhuria mkutano wa 17 wa Bunge mjini Dodoma, baada ya kuitisha mkutano nao na kuhoji kwanini wanakunywa chai ya wabunge wakati wamelipwa posho na vyombo wanavyofanyia kazi pasipo kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), badala ya kutoa ufafanuzi wa kama alipokea posho mara mbili au la.
  Dk. Mwakyembe alihoji hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, wakati akitoa ufafanuzi wa kukataa kuhojiwa na TAKUKURU kuhusu kuchukua posho mara mbili kwa kufanya kazi moja.
  Akizungumza kwa ghadhabu, Dk. Mwakyembe alisema kitendo cha kuhojiwa na TAKUKURU wakati huu ambapo wajumbe wa kamati iliyochunguza suala la Richmond wakitaka Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah, ahojiwe, ni mbinu za kutaka kuwanyamazisha.
  Dk. Mwakyembe alisema kupokea posho ni utaratibu wa siku nyingi na wa kawaida, hivyo kuhojiwa sasa ni mbinu tu ya TAKUKURU kutaka wabunge wasimhoji Dk. Hoseah.
  Alisema kwa uelewa wake wa kisheria, ikizingatiwa kuwa yeye ni mwalimu wa sheria, pamoja na kubaini mchezo huo, hakukubali kuhojiwa kama alichukua posho mara ya pili katika kikao cha kamati ya Bunge kilichofanyika mjini hapa na alitamba kuwa hata kama TAKUKURU itaamua kumpeleka mahakamani, ataibwaga vibaya.
  "Lunch allowances ni utaratibu wa siku nyingi na wa kawaida. Hata waziri akitembelea mikoani huwa anaandaliwa vizuri, licha ya kwamba amepewa posho. Kwani inawezekana kutomwandalia kwa sababu amekwishapewa posho?" alihoji Dk. Mwakyembe.
  Aliwashangaza waandishi wa habari alipowahoji kwanini hawajawahi kuhojiwa na TAKUKURU kwa kunywa chai ya wabunge huku ikijulikana kuwa wametumwa na vyombo vyao wanavyovifanyia kazi, huku akidai kushangazwa na hatua ya wabunge kufanyiwa hivyo sasa.
  Huku akilifananisha gazeti lililochapisha habari yake ya kukataa na kuomba msaada wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta ili asihojiwe na TAKUKURU kuhusu madai ya kupokea posho mara mbili, alisema kama hilo ni kosa, TAKUKURU ndio vinara wa kutoa posho.
  Alitoa mfano wa hivi karibuni katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo, ambapo licha ya kufahamu kuwa anaishi jijini Dar es Salaam, ilimpa posho ya malazi.
  "Hawa TAKUKURU ndio vinara wa kutoa posho. Inafahamika mimi naishi Dar es Salaam, wananipatia posho, leo hii pamoja na mambo mengi yanayotaka majibu wanataka kutuhoji, kama hii si kuwadhalilisha wabunge ni nini?" alihoji huku akionekana kukasirika.
  Mbunge huyo mara kwa mara akihusisha kitendo hicho na mchezo mchafu unaofanywa na aliowaita mafisadi. Alisema TAKUKURU imewaita wabunge kwa kutaka kuwahoji huku wao wakitaka serikali imchukulie hatua Dk. Hoseah na kwamba hilo ni lengo mahususi la kukwamisha juhudi za wabunge.
  "Sisi tunataka utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge, mojawapo ni lile la kuhojiwa kwa viongozi wa TAKUKURU," alisisitiza.
  Dk. Mwakyembe alibainisha kwamba, kukaidi wito wa TAKUKURU wa kuhojiwa juu ya suala hilo kunatokana na kinga aliyonayo kama ilivyobainishwa katika kanuni za Bunge sehemu ile ya 100 pamoja na 101, ambayo inamlinda kama mtumishi wa chombo hicho cha kutunga sheria.
  Aliendelea kujigamba kuwa kamwe hakuna mtu wa kumng'oa jimboni mwake na aliwataka wale aliowaita mafisadi waelewe kuwa hawawezi kumng'oa, labda wapige kambi kwa miaka mitano wakiwa pamoja na wake zao.
  "Mafisadi kuning'oa Kyela ni kazi ngumu, labda washinde Kyela kwa miaka mitano pamoja na wake zao, ndiyo wanaweza kufanya hivyo," alijigamba.
  Alisema wakati TAKUKURU inaendelea kung'ang'ania kuwahoji, zipo hoja za msingi zinazotakiwa kujadiliwa, ikiwa ni pamoja na ile ya nani mmiliki wa Kagoda na Richmond.
  Taarifa zilizotufikia kutoka ndani ya kikao cha ndani ya kamati ya wabunge wa CCM, muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kuwa wabunge hao wamegawanyika kuhusu suala la kuhojiwa na TAKUKURU, baadhi wakikubaliana na hatua hiyo na wengine wakipinga na kutaka isitishwe mara moja.
  Taarifa hizo zilieleza kuwa kundi la kwanza linaloungwa mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, linaunga mkono hatua hiyo ya TAKUKURU, kwa hoja kwamba fedha nyingi za serikali zimepotea kwa kuwalipa posho mara mbili wabunge.
  Kundi la pili linalodaiwa kuungwa mkono na Spika Sitta linadaiwa kuipinga hatua hiyo ya TAKUKURU, kwa madai kuwa inawadhalilisha wabunge.
  Hata hivyo habari hizo zilidai kuwa, licha ya Spika kutaka hatua hiyo isitishwe, Pinda alitangaza msimamo wake kuwa ni lazima kazi ya kuwahoji wabunge wote wanaotuhumiwa kuchukua posho mara mbili iendelee.
  Wakati huo huo, hatima ya kujadiliwa kwa hoja ya Richmond bungeni bado ni tete, hadi sasa hakuna taarifa zozote za iwapo wabunge watafanya hivyo.
  Pamoja na sakata hilo la Richmond, mambo mengine ambayo bado haijabainika iwapo nayo yatajadiliwa ni pamoja na Kampuni ya Reli (TRL), TICTS na mgodi wa makaa ya mawe, Kiwira.
  Kwa mujibu wa Ofisa Habari Mkuu wa Bunge, Ernest Zulu, alisema masuala hayo yaliyopewa kipaumbele kuwa yatajadiliwa katika mkutano wa 17 wa Bunge unaoendelea mjini hapa, kwa sasa yapo chini ya kamati husika hadi hapo watakapowasilisha taarifa zake kwa Spika.
  "Kwa sasa kamati hizo bado zinapitia taarifa zao, wakishawasilisha bungeni ndipo itajulikana kama watajadili au hawatajadili," alisema Zulu.
  Hata hivyo alisema kuna uwezekano wa Bunge kuongezwa siku mbili zaidi badala ya kumalizika Novemba 6, likaisha Novemba 8.
  Zulu alisema katika kikao hicho kutawasilishwa hoja tatu.
  Watakaowasilisha hoja hizo ni Mbunge wa Longido, Saning'o ole Telele (CCM) anayelalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wafugaji waliohamishwa kwenye maeneo yao na wawekezaji. Mbunge mwingine atakaetoa hoja binafsi ni Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Halima Mdee, ambaye anataka ufafanuzi wa jinsi Kiwanda cha Tanganyika Packers kilivyobinafsishwa. Mwingine ni Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), ambaye hoja yake binafsi ni kutaka masuala ya dini yasijadiliwe bungeni.


  [​IMG]


  juu[​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 10. b

  bambumbile Senior Member

  #10
  Oct 28, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika Sitta kigeugeu
  • Akana kauli zake, barua rasmi ya ofisi yake

  na Charles Mullinda  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, sasa ameanza kutoa kauli tatanishi baada ya jana kuzungumza na Tanzania Daima Jumatano na kueleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekiuka taratibu kwa kuwaita na kuwahoji baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kuchukua posho mara mbili, baada ya kufanya kazi moja.
  Sitta ambaye yuko mjini Dodoma anakoongoza mkutano wa 17 wa Bunge, alihojiwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu msimamo wake dhidi ya TAKUKURU kuwahoji wabunge na kutoa ufafanuzi wa barua iliyoandikwa na Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah, ambayo gazeti hili limeiona, kwenda kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah, ikimtaka alitafutie ufumbuzi suala la wabunge kulipwa posho mara mbili. Katika majibu yake Spika Sitta alikana kuifahamu barua hiyo na kueleza kuwa si jambo la ajabu kwa ukarimu wa Kitanzania wabunge kulipwa posho mara mbili na aliwashutumu baadhi ya viongozi wa juu wa serikali bila kuwataja majina kwa kulitisha Bunge ili lisitekeleze majukumu yake inavyotakiwa.

  Kauli hii ya Sitta imekuja siku chache baada ya Jumatatu wiki hii kunukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari akilalamika kuwa TAKUKURU inawadhalilisha wabunge inapowaita na kuwahoji bila kufuata utaratibu wala kanuni na jana alinukuliwa tena na baadhi ya vyombo vya habari akitoa mwongozo kwa wabunge kukubali kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU inapowaita kuwahoji.
  Awali alinukuliwa akieleza kuwa hatua iliyofikiwa na TAKUKURU kuwaita wabunge na kuwahoji ni uhdalilishaji na imekiuka utaratibu, kanuni na sheria za nchi dhidi ya Bunge kama taasisi inayojitegemea.
  Katika kauli hiyo, Sitta pia alieleza kuwa hajui kuwapo kwa jambo hilo kwa sababu hajataarifiwa na kwamba hajui kinachohojiwa na TAKUKURU kwa sababu taarifa hizo anazisoma katika vyombo vya habari.
  Alitoa tahadhari kwa taasisi nyingine za uchunguzi ikiwamo TAKUKURU kutoa taarifa ya maandishi ofisini kwake linapotokea jambo kama hilo ili Bunge liwe na taarifa na litoe utaratibu.
  Siku moja baada ya Spika kunukuliwa akitoa kauli hiyo, jana alinukuliwa akitoa kauli nyingine aliyokuwa ikipingana na ile ya kwanza.
  Gazeti moja la kila siku liliandika habari za ndani kutoka katika kikao cha wenyeviti wa kamati za Bunge, ambapo Spika Sitta alitoa mwongozo kwa wabunge kutoa ushirikiano kwa maofisa wa TAKUKURU wanaowaita kuwahoji.
  Hata hivyo alipozungumza na gazeti hili jana, Spika Sitta alisema msimamo wake halisi kuhusu suala hilo ni kupinga TAKUKURU kuwaita wabunge na kuwahoji bila yeye kutaarifiwa.
  "Ninayoyaongea sasa, ndiyo unapaswa kuyachukua kwa sababu ndio msimamo wa Spika. Kwanza mimi siijui barua hiyo. Pili, TAKUKURU wamekosea kulifanya suala hili la kawaida sana, wabunge si watu wa kuchezea, ni watu wakubwa na muhimu sana wanaopaswa kuhojiwa kwa heshima na viongozi wa juu wa vyombo vya usalama.
  "Na kabla ya kuhojiwa, ni lazima Spika ningetaarifiwa kwanza na kuandaa mazingira ya kuhojiwa kwao. Haiwezekani watu wa chini wasiojua maana ya mbunge kumhoji mbunge pasipo Spika kujua. Na kikawaida, takrima kwa ukarimu wa Kitanzania ni jambo la kawaida, ni ukarimu wa Kitanzania, hivyo hakuna posho mara mbili hapo. Ni ukarimu tu na wabunge wanaruhusiwa kuchukua," alisema Spika Sitta.
  Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Katibu wa Bunge, Kashililah kama ni wa shaka kiasi cha kuandika barua nyeti inayoomba msaada wa taasisi nyingine pasipo kumtaarifu, Spika Sitta alisema haamini kama Kashililah aliandika barua hiyo na kama aliandika, basi alilazimishwa na viongozi wa juu wa serikali.
  Katika hatua ya kushangaza, Spika alitoa kauli nyingine kuwa hata kama Kashililah aliandika barua hiyo, basi alikuwa anatekeleza majukumu yake ya kiutalawa hivyo anaweza asimtaarifu lakini TAKUKURU walipaswa kutochukua hatua zozote kulingana na barua hiyo kabla ya kumtaarifu.
  "Mambo ya utalawa sishiriki kila jambo, mhusika mkuu ni katibu na nadhani alilichukua kiutawala zaidi. Lakini TAKUKURU kabla ya kuanza kuifanyia kazi barua hiyo ni lazima wangenitaarifu kwanza Spika.
  "Hili jambo tumelijadili sana jana na juzi, tumebaini kuwa Katibu wa Bunge alitishwa sana. Watu wakubwa serikalini wamekaa vikao vingi tu, wamemtisha sana katibu kuwa ni lazima aandike barua hiyo, oh… eti ni maagizo ya rais, wakamlazimisha kuandika barua ile. Hili mimi siliafiki na tumefikisha malalamiko kwa waziri mkuu leo.
  "Bunge haliwezi kuendeshwa kwa vitisho, serikali iache kabisa kulitisha Bunge…. Bunge litakataa. Kama mbunge anatuhumiwa kuna Kamati ya Maadili ya Bunge, itashughulikia tuhuma hizo, si mambo haya yanavyofanyika sasa. Ni njama tu, lakini kamwe hatulegezi kamba, Bunge litaendelea na kazi yake pamoja na vitisho vyote," alisema Spika Sitta.
  Wakati Sitta akitoa kauli tatanishi kuhusu barua iliyoandikwa na Kashililah kwenda kwa Hoseah huku akisisitiza kutoifahamu, Tanzania Daima Jumatano imefanikiwa kuiona barua hiyo yenye kumbukumbu namba CEB.50/155/05/81 ikiwa na kichwa kinachosomeka: ‘Baadhi ya kamati za Bunge kuomba takrima serikalini na katika mashirika ya umma.'
  Sehemu ya barua hiyo inasomeka hivi: ‘Tafadhali rejea mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Bunge kuhusu suala tajwa hapo juu.
  ‘Nimepokea malalamiko kuhusu mwenendo usioridhisha wa kamati za Bunge kuomba takrima kutoka kwa watendaji wakuu serikalini na mashirika yake wanapohojiwa na kamati za Bunge.
  ‘Hivyo ili kuepuka athari zaidi, ilionekana kuwa ni busara jambo hili likatazamwa kwa kina ili kuainisha chimbuko lake linaanzia wapi, nani wahusika wakuu, hatua gani zichukuliwe na kwa utaratibu upi. (Rejea nyongeza ya nane ya kanuni za Bunge za toleo la 2007 kuhusu mgawanyo wa kazi wa kila kamati).
  ‘Ni tegemeo langu kuwa suala hili utalipatia kipaumbele na kulitazama kwa ungalifu mkubwa, kwa kuzingatia aina ya makundi yanayohusika na nafasi yake katika jamii ya uongozi wa nchi, ili pamoja na kulitafutia ufumbuzi, bali pia kuwa makini katika kulishughulikia.'
  Barua hiyo pia imenakiliwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.
  Spika alipoulizwa kuhusu barua aliyoandikiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mei 26 mwaka huu ikimtaarifu kuwa amepokea malalamiko kuwa wabunge wanadai posho wanapotembelea ofisi za serikali, taasisi na mashirika ya umma, Spika Sitta alikana huku aking'aka na kuhoji kwa nini mwandishi anambana kwa maswali magumu.
  "Kwa nini una mambo magumu sana wewe, mwandishi gani huridhiki na maelezo unayopewa, kila ukijibiwa unaendelea kuhoji hoji tu, basi andika unavyotaka, mimi sijaona barua niliyoandikiwa na Waziri Mkuu ikielezea kuwapo kwa jambo hilo," alisema kwa ukali Spika Sitta.
  Wakati Spika Sitta akikana kuiona barua hiyo, Tanzania Daima Jumatano imefanikiwa kuiona barua hiyo yenye kumbukumbu namba PM/P/2/567/33, yenye kichwa kinachosomeka: ‘Malipo ya posho kwa wabunge wanapotembelea kikazi ofisi za serikali, taasisi na mashirika ya umma.'
  Sehemu ya barua hiyo inasomeka hivi: "Kwa muda mrefu sasa zimekuwapo taarifa mbalimbali kwamba baadhi ya kamati za Bunge zinapotembelea wizara, mikoa, taasisi za serikalki na mashirika ya umma, ama zinaomba au zinadai kulipwa posho mbalimbali. Posho hizo ni pamoja na posho za kujikimu, posho za kikao na takrima.
  "Nimepewa taarifa kuwa wizara ambazo maofisa wahasibu walitakiwa kufanya malipo hayo ni pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maji na Umwagiliaji, Afya na Ustawi wa Jamii, Maliasili na Utalii, Nishati na Madini, Kilimo, Chakula na Ushirika na Viwanda, Biashara na Masoko.
  "Nimeona ni busara nitoe taarifa hii kwako ili uweze kutumia njia zako za kiofisi kuwaasa waheshimiwa wabunge wachache wanaofanya hivyo waache, kwani mambo kama haya yanaweza kulipuka siku yoyote na yakalifedhehesha Bunge letu tukufu."
  Barua hiyo ambayo imesainiwa na waziri mkuu mwenyewe, imenakiliwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.
  Wakati huo huo, Spika Sitta jana alimtetea msaidizi wake, Christopher Ndallu, kuwa hahusiki na upotevu wa aina yoyote ya fedha za Bunge wala hajashindwa kurejesha masufuru kama ilivyoelezwa na Kamati ya Hesabu za Serikali.
  Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwa msadizi wake huyo, Spika Sitta alisema si kawaida yake kuzungumzia mambo ya kitoto kama hayo ya msaidizi wake kushindwa kurejesha masurufu kwa fedha anazochukua, lakini amelazimika kufanya hivyo kwa sababu jambo hilo linakuzwa.
  Alisema, kamati hiyo ina chuki binafsi, jambo linalodhihirishwa na uamuzi wake wa kuamua kuhoji matumuzi ya safari zake wakati akiwa nje ya nchi na msaidizi wake aliyetuhumiwa naye akiwa hayupo.
  "Mimi sichukui masufuru, hilo kwanza lieleweke. Lakini Spika ana mambo mengi sana, hivyo fedha inayozungumzwa ni ndogo mno. Ninahudumiwa na serikali kwa safari zangu za ndani na nje ya nchi, nyumbani kwangu na ofisini kwangu, sasa milioni 70 kweli zinaweza kuwa gumzo kwa hadhi ya Spika? "Mambo ya kurejesha masurufu yana matatizo makubwa, Ndallu ana kila kitu, anazo risiti zinazodaiwa hazionekani na ushahidi mwingine wote. Ni majungu tu, hii kamati ina chuki binafsi, ndiyo maana wameamua kuhoji hili mimi nikiwa sipo na Ndallu pia. "Nimeamua kuzungumza hili kwa sababu limekuzwa sana, lakini huwa siongelei mambo ya kitoto namna hii. Milioni 70 kwa hadhi ya Spika wapi na wapi, nahudumiwa na serikali safari zangu, walinzi wangu, wasaidizi wangu, nyumbani na ofisini kwangu, sasa hiyo pesa unayohoji, kweli haya yote kwa Spika! Mbona hawahoji kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Jaji mstaafu. Kwa nini Spika tu?" alisema Spika Sitta.
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  daggers are out.
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Bhaghosha na bhankema,

  To be honest if that's a whole story i belive we dont have the Governmet at all,

  Kumeibuka kamchezo fulani nchi yaongozwa kimtindo only IKULU ndio yajifanya sasa ina mamlaka ya kuiongoza nchi na kutoa order pale waamkapo asubuhi ati.

  Imenza na IPTL within six days tokea tamko litoke IKULU meli ilisha tua bandarini how kunini hapo IKULU??


  Kitika mihimili hii 3 Bunge Mahakama na Serikali, Where does IKULU comes with command??

  and What is IKULU by the way?? hao viongozi walipo ikulu wao kazi yao ni nini mudxa wote huo walikuwa wapi kumshauri rais mambo nyeti kama hayo iweje leo IKULU inatupa na kutoa kauli tata zisizo na mwanzo wa mwisho kinyemela???

  Order Imetoka Ikulu "Lakini Waziri Mkuu akaonyesha kutokubaliana na maamuzi hayo ya spika na kueleza kuwa uchunguzi huo wa Takukuru utaendelea kwa kuwa ofisi ya Rais Ikulu ndio ambayo imeagiza ufanyike" Jamani tuna serikali hapa sasa??

  Tukisema Wana Mtandao walijipanga kuingia IKULU 2005 na hawakujua kabisa ni nini wanachotakiwa kwenda kukifanya IKULU????

  Ama kweli TAKUKURU ni chombo cha kufuata Upepo kabisa hapa, hakijui katiba na nadhani hakina mustkabadhi wa kujiongoza chenyewe kwani chapokea Order toka kwa wakubwa nacho chafanya, Hapo ni kuwa serikali wame prove failure na nia aibu sana ati kwa chombo kama icho kushindwa kuwa na kanuni zake za kujiongoza, Ati leo chaenda wahoji wabunge jamani??? Hapa twawaonyesha nini wananchi na ndio wapiga kura wetu??

  Uchaguzi uchajao ipo haja na hoja ya makusudi kabisa kuwa toa viongozi wote walio kaaa madarakani muda mrefu esp wazeeeeee hili liko wazi kwani wamefirisika kima wazo kabisa, kwenda kuwa hoji wabunge mbona hawakuitangaza kwa vyombo vya habari kama walikuwa wamejipanga na wana uhakika kwa wanachokifanya???

  Naomba kuwepo na mgawanyo wa madaraka esp kwa nchi zetu za kiafrika Ukisha kuwa Mbunge hupaswi kuwa Waziri na ukiwa waziri usiwe mbunge period ndipo hapo Kanuni katiba na sheri zitakapo wabana.

  Am realy shocked by TAKUKURU jamani haibu mbona
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  Oct 28, 2009
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  waache wavutane lakini mwisho tunataka kieleweke, siyo kuvutana tu.
  lakini haya mambo ya posho nyingi nyingi yapo kila mahala (kwenye uongozi wetu) ingawa sometimes sio direct. Huwa inashangaza wakubwa wanaposafiri huwa wanachukua per diem lakini huko wanakoenda huwa kila kitu wanapata free, na sometimes hata shopping kwa ajili ya zawadi za nyumbani huwa wanafanyiwa; ni hela za serikali hizo hizo zinatumika ku-provide free services kwa wakubwa ambao walishavuta per diem zao walikotoka.
   
 14. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wote ni vigeugeu, ukisoma kwamakini habari hizo, na kama ukidigest habari nzima utagundua kwamba huyo Mwakyembe amenakiri kupokea hiyo 'posho' au 'bahasha' marabili (kinyume na sheria) ila anakataa kuhojiwa na vijana wa Dr. Hosea wa TAKUKURU. Nadhani angehojiwa na hiyo kamati ya bunge angekiri waziwazi kwani mambo yangeishia hukohuko kwenye kamati, lakini akihojiwa na TAKUKURU anaogopa atapelekwa mahakamani kwani amevunja sheria (japo yeye anajitetea ni utaratibu wa siku nyingi) Kuna usemi unasema 'Za mwizi harobaini' sas kama hawa wabunge walikua wanapewa bahasha marambili kwa kazi moja, leo arobaini yao imefika, pili asisahau msemo mwingine 'mkuki kwa nguruwe.... sasa ni zamu yako nenda ukajitetee (ujisafishe) kwenye hiyo interview ya TAKUKURU. Pia ieleweke kwamba hakuna mwananchi (au Mbunge) ambaye yupo juu ya sheria.. Sheria ni msumeno...

  NB: sinachuki binafsi na wabunge, hata huyo Mwakyembe simjui anafananaje... ni mawazo tu..
   
 15. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kama yaliyoandikwa kwenye magazeti ni kweli yamezungumzwa na wabunge basi inaonekana asilimia kubwa ya wabunge ambao wanajifanyaga kuwa ni vinara wa kuutokomeza Ufisadi nchini Tanzania nao pia ni Mafisadi, maneno yalioandikwa kuwa yamenukuliwa kutoka kwa Dr. Mwakyembe yamenishangaza sana na yanatia shaka sana uadilifu wake. Ni matumaini yangu kuwa wamemnukuu vibaya.
   
 16. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nadhani PM anakosea kutetea msimamo wake kwa kusema kuwa Rais ameagiza kwasababu Rais ni muhimili wa dola kama Bunge lilivyo kwa hiyo sidhani kama Rais ana mamlaka ya kuagiza wabunge wahojiwe na kama ndivyo basi hapo katiba imechemsha inatakiwa irekebishwe. Wabunge wanaweza kumwajibisha Rais kwa kupigia kura ya kutokuwa na imani naye, na Rais anaweza kuwawajibisha wabunge kwa kuvunja Bunge, Je? Bunge linaweza kuamuru Rais ahojiwe? kama hapana Vivyo hivyo Rais hawezi kuamuru wabunge wahojiwe.

  Alafu watu mkumbuke kuwa Rais ana kinga sawa sawa na Wabunge, huwezi kumtuma Kopolo kumhoji Rais, Mbunge napigiwa Saluti (sikumbuki mpaka cheo gani) kwa hiyo mtu anayenipigia saluti kwa mujibu wa Itifaki hawezi kunihoji. Kwa hiyo 6 yupo sahihi kwenye suala la kiprotocol.

  Tuachambue hoja za kisheria zinazogongana hapa, naona watu wengi tunaongelea feeling, Ndio maana watu wanalia kuwa katiba imekaa vibaya ibadirishwe, na hapa tunaona wazi mgongano wa kikatoba, ambapo waziri mkuu anadhani kuwa bosi wake Rais yupo juu ya chombo cha kutunga sheria(Sik!). Mihimili ya Dola Serikali (Rais) Mahakama (Jaji Mkuu) na Bunge (Spika) hawa watu walipaswa wawe na nguvu sawa kwenye uwiano wa mzani ili demkrasia ya kweli iweze kuprevail kwenye nchi.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,597
  Trophy Points: 280
  Papa fisadi fisadi RA amelipwa $172 million kifisadi kupitia kupitia ufisadi alioufanya kupitia swahiba waka Lowassa na Lowassa akamwanga unga. Papa fisadi Rostam anahusika na wizi wa $40 million kipitia Kagoda lakini hadi hii leo hajahojiwa kuhusiana na tuhuma zote hizo. Na wewe mpiga debe wa mafisadi au fisadi hupigi debe kwamba Papa fisadi RA aburuzwe mahakamani lakini umeweza kupiga debe kwamba Wabunge waliochukua masufuru mara mbili waburuzwe mahakamani na kuplay down ufisadi uliofanywa na Fisadi Vijisenti Chenge. Hebu tuambie ni mabilioni mangapi hao Wabunge waliochukua masurufu mara mbili walinufaika nayo?

  Ama kweli mvunja nchi ni Mwananchi! Bado kuna watu wanaowapigia debe akina Lowassa, Papa fisadi Rostam na mafisadi wengine bila kuona athari kubwa iliyofanywa na ufisadi wao!
   
 18. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hivi akiulizwa hiyo ndege imetua wapi Kyela, atasema nini? Mambo mengine ni aibu tupu!
   
 19. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya mabadiliko ya haraka katika katiba ya nchi hii. Watu wanatumia mapungufu katika katiba kutetea uozo wao. Kama kila mtu akidai yeye ni mhimili fulani kwa hiyo siwezi kufanywa hili au lile basi tumeshajenga matabaka ya watu ambao wako juu ya sheria. Kauli za hawa wabunge na bosi wao zinatia shaka kuhusiana na suala zima la kupambana na ufisadi. Wamefika hatua ya kuhalalisha mazoea ya kupokea posho za ziada na kudai hata kama wamelipwa ni haki yao "kukarimiwa" kwani huo ndo ukarimu wa watanzania kwa mgeni. Hawa ndio watu tuliowakabidhi jukumu la kutunga sheria na kupitisha miswada badala yake wao ndio wanavunja sheria kwa visingizio kuwa hayo ni masuala madogo tu.

  Kwa kifupi hatuna serikali, hatuna bunge na nadiriki kusema hatuna tulichobakiza. Kauli ya mheshimiwa mmoja kuwa asilimia kubwa ya watanzania akili zimedumaa naanza kuona ukweli wake......wataendelea kutuburuza na kutufanya mazezeta kwani wanaamini kuwa wao walau wana kaunafuu kwenye udumavu wa akili ukilinganisha na sisi wengine ndio maana wanatuongoza na sisi tunafuata kama mabehewa tukilalamika chini chini bila kuchukua hatua madhubuti. Ifike mahali tuseme HAPANA, TUMECHOKA NA HUU UPUUZI MNAOTUFANYIA. Tukifanya hivyo watajua kuwa uzezeta wetu umenza kupungua......
   
 20. t

  tk JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona sikuelewi? Hivi kuna ufisadi mkubwa na mdogo. Una maana ufisadi mdogo unakubalika na ufisadi mkubwa haukubaliki? Kama mtu unamtoa dosari mwenzio lazima wewe mwenyewe uwe huna dosari. Hawa jamaa tayari wamekwisha onyesha wazi kuwa wako capable ya kufanya ufisadi kutokana na nafasi wanayoipata. Kama wangepata nafasi kama ya hao unaowasema Rostam, Lowassa na Chenge huenda wangefanya ufisadi mara mbili yao.
   
Loading...