Poromoko la bei la Gari aina ya Nissan Dualis

Kila mtu ananunua Gari kwa mahitaji yake mwenyewe (wengine wanatafuta luxury nyie kwa ajili ya kubebea simenti/tofali) so usipangie watu wote wanunue Toyota wakati wao wanataka Luxury.
Hahahah sasa Nissan ni Luxury mkuu?
 
Habari wana jamvi!
Kuna hii gari pendwa katika jiji la dar es salaam, inayoshika kask sana kwa kununuliwa kama njugu.. wao wanaiita “dar sweetheart”.. si nyingine bi ni “Nissan Dualis”.

Nakumbuka kipindi zinaanza kuingia hapa bongo zilikua bei moto sana around milion 25. Lakini kwa sasa nimeshangaa kuona bei zake zimeshuka sana mpaka kuna baadhi ya agents wanakuagizia kutoka japan kwa 14.5m. Binafsi nimevutiwa na gari hii hasa kwa muonekano wake, Mungu akijaalia basi hili gari litakua kipaumbele kwangu.

Naomba wajuvi wa mambo watusaidie nini kimechangia poromoko la bei kwa kiasi hiki? je lina matatizo fulani ya kiufundi au sababu ni ipi haswa?
Gari ni Matunzo tu, Dualis ni kama Diamond -Platinumz alipokuwa Tandale na Diamond Platinumz anayeishi MADALE.
MATUNZO ndio yanatofautisha, wabongo tumezoea gereji za pembeni ya barabara, spea feki kwanini gari isife, ipe matunzo kama Zari anavyojipenda uone.
 
Wengine hatuijui tuwekee kapicha
1607028140711.png
kuna Duelis na Duet
 
Ni dualis, engine hazina shida, ulaji wa mafuta ni safi shida ya hii gari ni gari mayai haifai kuenda nayo rough road mara kwa mara. Na shida ni spare parts ni aghali mkuu itakufilisi..

Mara utasikia wish bone zimekufa ukiuliza bei ni mshahara wa mwalimu wa secondary,

Kwa ufupi chochote kitakachokufa kwenye nissan ujue ni bei aghali haswaaa...
Tuache dharau kwa waalimu!
 
Ni dualis, engine hazina shida, ulaji wa mafuta ni safi shida ya hii gari ni gari mayai haifai kuenda nayo rough road mara kwa mara. Na shida ni spare parts ni aghali mkuu itakufilisi..

Mara utasikia wish bone zimekufa ukiuliza bei ni mshahara wa mwalimu wa secondary,

Kwa ufupi chochote kitakachokufa kwenye nissan ujue ni bei aghali haswaaa...
Tuache dharau kwa waalimu!
 
Sasa na msimu huu wa mvua madimbwi kibao mimaji inajaa barabarani ndio uburuze Nissan Nyanya yako imagine lile li njia la mnazi mmoja linalonyoosha hadi mfugale kunajaaga mimaji pale mbele. Lazma utubu tu 😂😂😂

Juzi nimeburuza Toyota langu mle hadi nikalionea huruma japo halijakorofisha. Maji yalikuwa usawa wa bonet nikawaza je mtu wa Nissan, Benz, Bmw au Audi atatoboa kweli bila dashboard kumeremeta 😂😂😂
Acha maneno mbofumbofu kwa xtrail. Imetulea tukiwa na hela za mawazo. SUV kwa Bei ya Sedan
 
Back
Top Bottom