Porokwa kupambana na Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Porokwa kupambana na Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Feb 13, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Daniel Porokwa (37), ametangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

  Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ni Mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1995.

  Porokwa ametangaza nia hiyo jana nyumbani kwao katika Kijiji cha Monduli Juu.

  Viongozi wa kimila wa jamii ya Wamasai (Laigwanan) zaidi ya 30 kutoka wilaya za Monduli na Simanjiro walimuombea dua.

  “Ndugu zangu napenda kuwaarifu kuwa natarajia kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo la Monduli kupitia chama changu cha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakaofanyika baadaye mwezi Oktoba…kwa hiyo nawaomba wana Monduli na wenye nia njema na jimbo letu kuniunga mkono,” amesema Porokwa.

  Amesema, lengo la kujitosa kuwania nafasi hiyo ni kuleta changamoto katika nafasi ya uongozi na kumpokea Mbunge wa sasa ambaye kwa kiasi kikubwa amesukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo.

  “Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mheshimiwa Lowassa amefanya kazi kubwa sana kupigania maendeleo ya jimbo letu…lakini kwa kuwa katika Taifa letu tumejenga utamaduni wa kupokezana uongozi, basi nafikiri ni muda muafaka sasa kumpokea na kumsaidia mheshimiwa Lowassa,” amesema Porokwa.

  Amesema, muda wa kampeni uliopangwa na chama ukiwadia, atatangaza kaulimbiu yake atakayotumia katika kampeni zake na wanachama wa CCM watatumia nafasi yao kidemokrasia kuwapigia kura wagombea watakaokuwa wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

  Porokwa alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha kati ya mwaka 2003 hadi 2008, alimaliza muda wake na nafasi yake kuchukuliwa na Mwenyekiti wa sasa, James ole Millya.

  Porokwa ni mwana CCM wa kwanza kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, wengi wanatarajia kuwa Lowassa atagombea tena.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,625
  Likes Received: 23,787
  Trophy Points: 280
  Hata mimi ningeshauri EL asigombee, ajipumzikie kama ma ex pm wenzake kina Msuya, Sumaye, Warioba na Dr.Salim.

  Ni kweli Monduli, CCM imetimiza ilani yake kwa asilimia 100 na EL kafanya mengi. Wazee wakimasai walishaamua kumuengua EL baada ya kupata siri kuwa kumbe jamaa sio Mmasai ni Mmeru aliyepose kama Masai.

  Ile kesi ya Ole Sendeka na Ole-Milya ni battle ground ya EL na Porokwa. Mangi anamwaga fungu kwa Sendeka waing'oe ngome ya EL, huku RA akimwaga kwa Milya EL abaki. Monduli ni kipindi cha mavuno, maana vita vya mafahari huku wakimwaga fedha, nyika haziumii bali zinaneemeka.
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,139
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Mwanzoni nilikuwa sielewi....Asante sana mkuu kwa hili,
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kila mtu ana haki ya kugombea uogozi na pia kila mtanzania anayo haki hivyo kuna haja ya watanzania kuacha kama wanaona amechoka na kutompa kura
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Monduli labda Lowassa aamue kuacha kugombea mwenyewe. Lowassa na wafuasi wengi sana vijana na akina mama na hao ndiyo wapiga kura. Wazee mara nyingi mvua ikinyesha hawaendi na hata jua likiwa kali mno hawaendi. Ili kuwa mmasai siyo lazima kuzaliwa umasaini, siyo lazima uwe na baba mmasai au mama mmasai bali hata kama wewe ni mzungu na umekabili kufuata mila na desturi za kimasai utapewa heshima zote za kimasai na hautabaghuliwa kwa vyovyote vile. Ukiangalia Monduli wengi wa wakazi wake wamehamia na wengi wana orijin ya Meru, Rombo, Machame, na Kibosho na hata majina yao kwa kiasi fulani yanalandana. Kama EL akiamua kung'atuka ni vizuri zaidi kwake lakini nadhani hii itakuwa mapema sana kuisemea!!!
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Pasco,

  Ni vigumu sana Bwana Lowassa kuachia ngazi hasa tukizingatia kwamba bado ana hamu ya kutaka kukamata madaraka makubwa ya kisiasa[urais].Ubunge,UNEC na CC ni nafasi nzuri zitakazo mwezesha kutimiza ndoto zake.Bwana Lowassa anajua kuachia ubunge ni hatari sana kwake kisiasa kurejea kileleni.

  Bwana Parokwa anaungwa mkono na wamasai wengi ambao wanadhani Lowassa hastahili kuwa mwakilishi wao kwasababu asili yake ni Meru.Bwana Lowassa amekuwa akifanya juhudi kubwa tangu zamani kuhakikisha hakuna mmsai mwenye nguvu anachomoza kwenye anga za siasa Arusha.Walijaribu kina Lekule Laiser na Elisa Mollel kugombea uenyekiti wa mkoa na ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa waliishia kuzushiwa kesi na kuondolewa katika kugombea nafasi hizo.kilichofuatia ni Bwana Lowassa kumweka Bwana
  Onesmo Nangole kugombea uenyekiti na mmeru mwenzake Bwana Kaaya nafasi ya NEC.

  Kuna wakati wananchi wa Monduli walitaka mtoto wa marehemu E Sokoine agombee lakini aliishia kupelekwa ubalozini,Bwana Lowassa ni mjanja sana kiasi kwamba mara nyingi karata zake anazicheza vyema.

  Parokwa anaweza kumsumbua sana Lowassa ikiwa anapata sapoti ya Mzee Mengi,ikumbukwe Lowassa mara zote anahakikisha hapati mpinzani kwenye jimbo lake hii itakakuwa mtihana mkubwa sana ikiwa Parokwa ataendelea na msimamo wa kugombea ubunge Monduli.
   
 7. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,704
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama atamuweza.Lowassa ndio amesha safishwa.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 10,073
  Likes Received: 3,388
  Trophy Points: 280

  Mzee Pasco, tunakuamini sana kwa michango yako humu. Lakini hii ya 100 % nina mashaka nayo mkuu!!!
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Porokwa anaweza kumuangusha Lowassa kwasababu wamasai kwa utamaduni wao sio Mafisadi, ni watu wachapa kazi na wanajiheshimu, kuiba mali za watu wengine sio utamaduni wao; Sekoine kabla ya EL alikuwa kiongozi muadilifu lakini sasa EL amethibitika kuwa ni fisadi na mwizi kwahiyo wamasai hawapendezeshwi na sifa hizo na ndio maana hata hoja za kuwa EL sio mmasai zinapata nguvu!! Kwa mtaji huu Porokwa anaweza kuua tembo kwa ubua!!
   
 10. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sishawishiki kuwa wamasai huko vijijini wanajua kama kuna kitu kama hicho.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280

  Hiyo ndio itakuwa kazi ya Porokwa kuwaelimisha juu ya ufisadi wa EL; na kazi hii nadhani amekwishaianza na ndio maana hao wazee wa kimasai wamempa baraka zao!! Kazi ipo wajameni.
   
 12. B

  BUBBA Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri wakati mwingine kukumbuka historia na kutambua nafasi za watu hasa kwenye uongozi wa kijamii na tusiishie kupiga kelele na kuwa wapayukaji kwenye jukwaa hili muhimu. Kwa watu wa Monduli na jamii ya wamasai Mhe Lowassa ni mtu wa muhimu kwao hata kama watanzania wote hawatomtambua,uthibitisho wa hilo ni kwa kumpatia cheo cha Uleiguanan na tena kumchagua kuwa mkuu wa "luiguanans" in East Africa,pili utekelezaji wake wa ilani ambao hata Porokwa anaukubali. Upande wa Porokwa,alipewa nafasi ya kuongoza Umoja wa vijana Arusha wa CCM kama Mwenyekiti kwa muda wa miaka mitano hakuna lolote alilofanya zaidi ya kuruhusu katibu wake ndugu Mfaume Kizigo kujiuzia nyumba ya umoja wa vijana,huu nao ni ufisadi wa hali ya juu. Pengine angeulizwa alishindwa kusimamia kanuni ya umoja wa vijana leo hii anataka kusimamia Ilani ya chama,Katiba ya chama na Katiba ya Nchi kama Mbunge ataweza kweli? Kama kweli wana Monduli wamemchoka Mhe Lowassa nadhani wanahitaji kiongozi makini zaidi ya Porokwa.
   
 13. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Porokwa hafai wala hataweza kumng'oa Edward. Yeye mwenyewe akiwa mwalimu wa shule anazo kashfa za udokozi wa mapesa. Na yeye anajua hamwezi. Kwa sababu ni mtu anayependa pesa bila shaka anataka kumtikisa Edward ili anunuliwe na amwachie. Na hilo ndilo atakalofanya. EL is very powerful. Hate him or Love him. Lowasa is there to stay na mwaka 2015 atarudi kama Rais a la Jacob Zuma.
   
 14. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,482
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180  mmhh! watu bwana...yaani jamaa awe Rais!! Mchonga atafufuka walahi.....mimi simooooo....
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyo pokorokwa anataka siasa ya kupokezana?

  wanapokezana kitu gani?

  yaani kama ana sababu ya kipuuzi ya namna hii basi hafai coz hataki kusema ukweli;

  Bora angesema ana lengo la kuwaondoa wale wote wenye kashfa ya ufisadi
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Porokwa anapoteza muda wake tu ni bora angefanya kitu kingine..anajua hashindi
   
 17. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,506
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Gembe habari za siku nyingi!!!
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,415
  Likes Received: 2,056
  Trophy Points: 280
  Ni nzuri ila aangalie utasikia mara kapata ajali barabarani Mwache ashindane na huyo fisadi!
   
 19. K

  Kibori Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kugombea au kutogombea ni haki ya msingi na uamuzi wa kila mtu apendaye, msikatishe watu tamaa, wanajua wanachokifanya mpaka kutangaza nia zao....swala la atashinda au la ni wantanzania au wanamonduli ndio wenye majibu . After all hakuna hata mtu mmoja ambaye mwenye kujua dhahiri kama atashinda au la lakini pamoja na hayo wanaendelea kugombea na wataendelea kugombea tena sana tu .
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  andika hii meseji kwenye diary yako siku kura za maoni zinatangazwa ntaku PM mkuu.Porokwa nina uhakika atapatta namba za kiatu katika kura za maoni...EL hamuwezi hamuwezi hata afanyeje
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...