MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Daniel Porokwa (37), ametangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ni Mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1995.
Porokwa ametangaza nia hiyo jana nyumbani kwao katika Kijiji cha Monduli Juu.
Viongozi wa kimila wa jamii ya Wamasai (Laigwanan) zaidi ya 30 kutoka wilaya za Monduli na Simanjiro walimuombea dua.
Ndugu zangu napenda kuwaarifu kuwa natarajia kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo la Monduli kupitia chama changu cha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakaofanyika baadaye mwezi Oktoba kwa hiyo nawaomba wana Monduli na wenye nia njema na jimbo letu kuniunga mkono, amesema Porokwa.
Amesema, lengo la kujitosa kuwania nafasi hiyo ni kuleta changamoto katika nafasi ya uongozi na kumpokea Mbunge wa sasa ambaye kwa kiasi kikubwa amesukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo.
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mheshimiwa Lowassa amefanya kazi kubwa sana kupigania maendeleo ya jimbo letu lakini kwa kuwa katika Taifa letu tumejenga utamaduni wa kupokezana uongozi, basi nafikiri ni muda muafaka sasa kumpokea na kumsaidia mheshimiwa Lowassa, amesema Porokwa.
Amesema, muda wa kampeni uliopangwa na chama ukiwadia, atatangaza kaulimbiu yake atakayotumia katika kampeni zake na wanachama wa CCM watatumia nafasi yao kidemokrasia kuwapigia kura wagombea watakaokuwa wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.
Porokwa alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha kati ya mwaka 2003 hadi 2008, alimaliza muda wake na nafasi yake kuchukuliwa na Mwenyekiti wa sasa, James ole Millya.
Porokwa ni mwana CCM wa kwanza kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, wengi wanatarajia kuwa Lowassa atagombea tena.