Poor waandishi na magazeti ya Tanzania!!?

Wdl

Senior Member
Jun 2, 2017
185
174
Nani kusema wamekubali kulipa !? Au Jemedari amewaambia mumpigie debe, ngoma bado mbichi na siyo ajabu Tanzania ikatakiwa kuwalipa fidia.

Watalipa kwa base ipi labda !?

IMG-20170615-WA0009.jpg
 
Binafsi nimesikia kutoka taarifa ya habari ya TBC 1 jana 2 usiku.Na wamesema km ambavyo hilo gazeti limeandika.Lakini habari iliyopo hapa jamvini ni kuwa sio kweli.
 
Wasije wakawa wametutega tu maana ni wazoefu sio Bahati mbaya huko Venezuela wana nongwa yaendelea
 
Usilaumu bure media, this is the source
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017
Hivyo walichoripoti media ni walichoambiwa na mwenye mali, mmiliki mkuu!.

Paskali
 
Is this barrick issue adding a plate of ugali on your table? Who told you wazungu wanalipaga tu bila kujua wanalipia nni?
Hiyo press statement ya barrick umeisikia au unaongea tu inasema hvi wataunda commitee itakayokuja na win win situation.
Mwisho magazeti yetu yanaibisha wanandika vitu ambavyo havipo bure kabisa.
 
Tamko LA Barrick ni kuwa kuna timu ya mazungumzo itaundwa kupata win win situation, sasa kauli ya bwana mkubwa kuwa wamekubali kulipa sijui kaitoa wapi na magazeti yanaibeba tuu
Kwan palen ndio maneno pekee a yule Mkurugenz wa barrick uliyoyasikia,je wakichoongea na Rais huko ndani unayajua??
 
Tatizo sio magazeti. Tatizo la upotoshaji huu ni Sizonje ambaye kwake kiingereza ni shida. Yeye hakuelewa kilichosemwa na Prof. Thornton, hivyo akaamua kubahatisha tu kwamba "amesema kampuni yake italipa pesa zote zilizopotea" kumbe Prof kasema atahakikisha yanafanyika mazungumzo ya kupata maridhiano.
 
Soko huru hili haulazimishwi kununua, kuna magazeti mengi chukua lingine
Fikra zako zinapendekeza gazeti linaweza kuandika "rais mstaafu afa ghafla"
Japo ni uongo lakini unaruhusa kutolinunua ili kui avoid habari???
 
Back
Top Bottom