Pongezi zangu kwako dr. Slaa,viongozi wengine muige

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
7,687
Reaction score
2,240
Jana nilikutana na dr slaa Pale Mlimani city nadhani alikuja kwa ajili ya Bank issues katika ATM za CRDB tawi la Mlimani City. Nilichokipenda kutoka kwake ni pale alipokuja na kujiunga na foleni ndefu iliyokuwa inaitaji pia huduma hiyo na hata pale wasamalia wema walipomtaka apite awe wa kwanza alikataa na kutoa tabasamu kuuubwa akiashiria kuwa zamu yake ikifika ataingia na kupata huduma.

NAKUPONGEZA KWA KUKATAA UTUKUFU ULIOPEWA NA WATANZANIA WENYE ROHO YA UPENDO KWA VIONGOZI WAO. Kioja kilichonishangaza, kunisikitisha na kunishtua ni dr Slaa kuwa na Bodigard mmoja ambaye hata silaha hajashika ila akiwa nyuma ya dr Slaa kashikilia gazeti anasoma. Hii ni hatari sana nikiamini kuwa dr Slaa kama mwanasiasa amejitengenezea maadui wengi ambao wanaweza kutumia mwanya huo kumdhuru. Ni vyema dr Slaa na CHADEMA mkalifanyia kazi hilo.

Nadhani mnakumbuka siku moja kupitia akaunti ya Independent spy ililetwa taarifa kuwa dr Slaa alikuwa anafuatiliwa na gari katika msafara wake wakati wa harakati zake za kichama.

Sasa watu wenye akili hawatokuwa tayari kurisk maisha yao wakati kuna chansi nzuri tu za kuweza kumdhuru. Bodigard mwenyewe anaonekana dhaifu sana. Ni ushauri tu.
 
Hukumuuliza hizo fedha alizokuwa anatoa km zina uhusiano wowote na fungu la ruzuku ambalo wachache wanamega na kutumbua badala yakuzielekeza kwenye ujenzi wa chama?
 
alikuwa hana haraka na hiyo pesa.naalifanya hivyo ili waliopo hapo wasijue nae niwalewale.
 
Uyo bodyguard namfaam, ana mkanda mweusi, pia kasomea taikondo.
 
CCM kweli ni janga hakuna aliyeko CCM akawa na akili njema hata kido angalieni huyo mtu anayejiita CCM ni ovyo kabisa
 
DR. ni mtu wa watu, hata hivyo siraha siyo lazima ionekana na si lazima kila mtu ajue kwamba yule alikuwa ni mlinzi wake, pia kusoma gazeti si hoja kwamba jamaa hajui kazi yake, inawezekana hiyo ikawa mbinu za kimedani.

Sasa ku-test zali wewe ungeenda karibu na DR. na kujaribu kumpush pembeni ili ujiridhishe kwamba jamaa alikuwa anasoma gazeti na hakuwa na siraha yoyote.

Nafikiri kwenye suala la ulinzi CDM wapo makini - lakini kumbuka kwa sisi tuliozaliwa mara ya pili tunaamini kwamba mlinzi mkuu na tunayemwamini wote ni mwenyezi mungu, huu ulinzi wa duniani watu wakitaka kukutoa roho wanakutoa tu muda wowote ule.

Mkabidhi maisha yako mwenyezi mungu na uwe tayari kwa safari ya mbinguni wakati wowote.
 
Jana nilikutana na dr slaa Pale Mlimani city nadhani alikuja kwa ajili ya Bank issues katika ATM za CRDB tawi la Mlimani City. Nilichokipenda kutoka kwake ni pale alipokuja na kujiunga na foleni ndefu iliyokuwa inaitaji pia huduma hiyo na hata pale wasamalia wema walipomtaka apite awe wa kwanza alikataa na kutoa tabasamu kuuubwa akiashiria kuwa zamu yake ikifika ataingia na kupata huduma.

NAKUPONGEZA KWA KUKATAA UTUKUFU ULIOPEWA NA WATANZANIA WENYE ROHO YA UPENDO KWA VIONGOZI WAO. Kioja kilichonishangaza, kunisikitisha na kunishtua ni dr Slaa kuwa na Bodigard mmoja ambaye hata silaha hajashika ila akiwa nyuma ya dr Slaa kashikilia gazeti anasoma. Hii ni hatari sana nikiamini kuwa dr Slaa kama mwanasiasa amejitengenezea maadui wengi ambao wanaweza kutumia mwanya huo kumdhuru. Ni vyema dr Slaa na CHADEMA mkalifanyia kazi hilo.

Nadhani mnakumbuka siku moja kupitia akaunti ya Independent spy ililetwa taarifa kuwa dr Slaa alikuwa anafuatiliwa na gari katika msafara wake wakati wa harakati zake za kichama.

Sasa watu wenye akili hawatokuwa tayari kurisk maisha yao wakati kuna chansi nzuri tu za kuweza kumdhuru. Bodigard mwenyewe anaonekana dhaifu sana. Ni ushauri tu.

Ukisha kuwa kiongozi makini na mwanifu ni lazima uwe na madui wengi hasa wa kutoka CCM ambao wengi wao hawana sifa za uaminifu.
 
DR. ni mtu wa watu, hata hivyo siraha siyo lazima ionekana na si lazima kila mtu ajue kwamba yule alikuwa ni mlinzi wake, pia kusoma gazeti si hoja kwamba jamaa hajui kazi yake, inawezekana hiyo ikawa mbinu za kimedani.

Sasa ku-test zali wewe ungeenda karibu na DR. na kujaribu kumpush pembeni ili uone kama hizo zoezi lako lingefanikiwa.

Nafikiri kwenye suala la ulinzi CDM wapo makini - lakini kumbuka kwa sisi tuliozaliwa mara ya pili tunaamini kwamba mlinzi mkuu na tunayemwamini wote ni mwenyezi mungu, huu ulinzi wa duniani watu wakitaka kukutoa roho wanakutoa tu muda wowote ule.

Mkabidhi maisha yako mwenyezi mungu na uwe tayari kwa safari ya mbinguni wakati wowote.

Haha!. Sisi tuliozaliwa mara ya pili.......

Nimeipenda hii Mkuu
 
Wewe unaugua

Hakuna mtu mnafiki kama wewe humu JF.Ulipokuwa unajiita kamanda ulitaka uaminiwe humu alafu baadae ujifanye unajitoa Chadema ili kuvunja moyo wapiganaji wa mtandaoni na wananchi.
Haya mnafiki ishi unafikini unapostahili alafu ufungue ID nyingine ya kuendelea kujifanya kamanda kumbe mjanja mjanja wa mitandaoni tu.
 
Nimempiga picha na kamchina kangu naona network inazingua nitawawekea mumuone dr Slaa na ile stayle yake ya kuweka mikono tumboni kama anataka kufunga swala.
 
Dhaifu Bodigard.....mdharau mwiba mguu huota tende...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom