mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,073
Upo usemi wa wa wahenga usemao mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Wizara wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi ni moja kati ya wizara kubwa,nyeti na yenye kugusa maisha ya watanzania wengi sana.Ndiko kwenye barabara,vivuko,bandari,kampuni za simu {whatsapp},Mitandao etc etc.
Sijui anapumzika saa ngapi!Sijui anakaa na familia yako saa ngapi! Kama ndugu;jamaa na marafiki wanapata muda nae.Utendaji wa jinsi hii unatoa taswira ya uwajibikaji mahsusi unaopaswa kufanywa na viongozi wa kisiasa ukihusisha ufuatiliaji yakinifu wa sera/michakato/mikakati/mipango ya serikali spidi hii ya mfano huu wa Prof.
Mbarawa iwe chachu kwa wanasiasa wengine waliopewa dhamana katika awamu ya 5 ni rahisi kumsikia Mbalawa kwa siku moja akiwa katika mikoa miwili tofauti akifuatilia utekelezaji wa hili au lile mara yupo Kigoma, mara tabora, mara mwanza,mara kurasini,mara huku mara kule wapo wanaoweza kumbeza lakini upo msingi imara sana unajengeka.
Waziri Prof. Mbarawa kwa dhati kabisa anastahili pongezi lukuki kwa sababu ya kumwona akichapa kazi kupitia ufuatiliaji,usimamiaji,uendelezaji,utafutaji suruhu na utendaji wa hekima kila iitwapo leo kila anapopita ama kufanya ziara yenye taarifa ama kushtukiza.
Ushauri: Namshauri Prof. aongeze ukali katika utoaji wa maagizo au matamko yake la sivyo anaweza kujikuta jitihada zake nyingi za dhati hazizai matunda stahili na kwa wakati.Pia afahamu ya kuwa taasisi zilizo chini ya Wizara yake zina miradi na mapato ya mabilioni ya fedha za watanzania hivyo kwa kuwa kansa ya ufisadi imeshamiri upo uwezekano wa baadhi ya watendaji kuwa na viburi/kutotishika/kutoheshimu maagizo,maelekezo na miongozo. Mfano wa Taasisi hizi ni TANRODS,TEMESA,Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,Mamlaka ya Bandari,TCRA,RFB,TRL,RAHCO,etc.