Pongezi kwa rpc mwanza

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Waungwana mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. Nimefuatilia maandamano ya leo kwa umakini mkubwa lakini hasa nikijaribu kudadisi nafasi ya jeshi la polisi katika kusababisha au kuzuia machafuko.
Niseme tu kwamba kwa jinsi nilivyomsikia Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Bw. Sirro akiongea na Radio France International (RFI) nimeamini kuwa ndani ya jeshi lililochafuka la polisi bado kuna watu waungwana. Ukiangalia picha jinsi polisi walivyokuwa makini hakika unakubali kuwa Polisi Mwanza wamejitahidi kuonyesha umakini wao tofauti na wale wa Arusha. Kumbuka shamrashamra zilianza tanu jana,Je angekuwa Andengenye hali ingekuwaje?
Big up RPC Simon Sirro
 
nami nampongeza RPC mwanza kwa kulinda maisha ya watanzania-kinyume na polisi arusha wauaji!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
nami nampongeza RPC mwanza kwa kulinda maisha ya watanzania-kinyume na polisi arusha wauaji!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kuna watu wanaotumia akili za kuzaliwa na wale wanaotumia za kuambiwa pekee, Polisi wa Arusha ni mfano wa wanaotumia akili za kuazima
 
Naungana na wote wanaoamini na kupongeza Ueledi aliouonyesha RPC wa Mwanza. Napenda kuwakumbusha wafuatiliaji wa siasa za Arusha kwamba dhambi ya kutotambua Ueledi na Uzalendo alioufanya Basilio Matei yule RPC Arusha wakati wa uchaguzi umepelekea kwenye 'miujiza' anayoifanya Andengenye(RPC wa Sasa). Anajaribu kufurahisha walioona kwamba mtangulizi wake alikosea. Matokeo yake hakuna ueledi au hata busara katika amri wanazopewa polisi wa Arusha. Naamini hata yeye anahangaika na kwa damu iliyomwagika hatapata Amani WALA KULETA ANANI.
 
hatutaogoma kutoa pongezi kamwe hata siku moja
sisi ni wawazi na si wanafiki, hata kama watamwondoa kama unavyosema
nao wataondoka tu
kwani unadhani wata-survive mabadiriko ya sasa?
Bora mkae kimya asije hamishwa bure
 
Jamani nyamazeni asije hamishiwa makao makuu kuwa bench officer kama aliyekua rpc wa arusha baada ya uchaguzi!
 
kitambo tu mwezi utaandama...being askari bila kufuzu kupiga kibongo bongo haikupi heshima uswahilini...ndio!
 
Hata kamanda Mbowe amemsifia, kamwambia wakimtimua aende CDM watampa kazi aendeleze mapambano kukomboa nchi.
 
RPC huyu ni mfano wa kuigwa! Hata akipeleekwa makao makuu kama matokeo ya kutenda iliyo haki, historia itamtetea sana; historia hiyo hiyo itawahukumu mafisadi watakao m-victimize RPC huyu kwa haki!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom