RPC Mwanza, Ahmed Msangi awaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaohamisha maandamano haramu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Jeshi la Polisi Jijini Mwanza limeaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.

RPC Msangi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na Polisi mbalimbali walipokuwa wakifanya mazoezi ya viungo katika uwanja wa Mabatini

RPC Ahmed Msangi amesema kuna umuhimu wa kufanya mazoezi sana ili uwe na pumzi na muscles zikaze ili at least pale unapotaka kufanya shughuli zinazotumia nguvu na tuweze kufanya shughuli vizuri kwa ufanisi.

Nafikiri wote sasa hivi mnafahamu kuna hii mitandao ya kijamii kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu, na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa, na kiukweli umepigwa marufuku.

Sasa hili linasambazwa kwenye mitandao ya kijamii maana kuna hili la kushawishiana, la pili wote sisi askari inabidi tuwe na masikio marefu na pua zifanye kazi vizuri na akili.

Kuna watu wanafanya fanya hayo kushawishiana. Tufanye upelelezi, tuchunguze. Yeyote atayefanya hayo kushawishi tukimng'amua tuweze kumkamata. Tumkamate na tuweze kumhoji wana sababu gani, wana nia gani wanataka kufanya vitu vya kushawishiana kufanya vitu vya namna hiyo.

----
Viongozi mbalimbali walizuia 'maandamano haramu'. Zaidi soma...

Februari 26, 2018. IGP Simon Sirro alisema Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Mnamo Februari 28, 2018. Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo alisema Kuna viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi, hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Machi 9, 2018 Rais Magufuli amesema Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma watakwenda kuwasimulia vizuri

Machi 9, 2018. Jeshi la Polisi pia kupitia Mkuu wa Operation na mafunzo, CP Nsato Marijani wakati alipokutana na vyombo vya habari amekionya kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram
 
Hizi kesi huko mahakamani sijui zitakuwaje kwa watakaoshitakiwa na wakapata mawakili wazuri wa kuwatetea.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jeshi la Polisi Jijini Mwanza limeaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.

RPC Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuna umuhimu wa kufanya mazoezi sana ili uwe na pumzi na muscles zikaze ili at least pale unapotaka kufanya shughuli zinazotumia nguvu na tuweze kufanya shughuli vizuri kwa ufanisi.
Huyu atakue
 
nani anaamasisha maandamano kati ya police na raia...

by the way maandamano ni ya ccm wenyewe angeanza kuwakata makada...

sana sana sasahivi atakuwa anafurahia budget ya kuzuia maandamano ambazo wameanza kugawa kila mkoa

Wanasahau nguvu ya umma haijawai mwacha mtu salama ....
 
Mwambieni huyu katiba inaruhusu Watanzania kuandamana siku na mahali popote pale bila kutoa taarifa kwa yeyote. Akajifunze haki na uhuru wa Watanzania kama unavyoelezewa ndani ya katiba.
Mambo sasa alisema kuandamana instagram ruksa sasa tunahamadishana huko tatizo nini? Mtaani tutaenda kuandamana kuunga mkono mapinduzi ya zanzibar ya kumwondoa sultan tu. Haya ya Mange mwisho wake kwente tecno tena tumelala kama kamanda wa dodoma alivyoagiza
 
Hizi kesi huko mahakamani sijui zitakuwaje kwa watakaoshitakiwa na wakapata mawakili wazuri wa kuwatetea.
Yerico anadai ana mawakili wazuri mpaka leo kesi inamuhenyesha,
Wale waliovunjwa miguu bado wanaoza ndani
Nondo ameshaharibu career yake,mtaishia kuchuuzana tu humu wale wasio na akili watakamatwa kama panya
 
Kamanda Msangi,nimejulishwa kuwa polisi wa usalama barabarani hutengeneza foleni muda wa asubuhi ili wakamate gari zinazotanua!!
 
Jeshi la Polisi Jijini Mwanza limeaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.

RPC Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuna umuhimu wa kufanya mazoezi sana ili uwe na pumzi na muscles zikaze ili at least pale unapotaka kufanya shughuli zinazotumia nguvu na tuweze kufanya shughuli vizuri kwa ufanisi.

Nafikiri wote sasa hivi mnafahamu kuna hii mitandao ya kijamii kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu, na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa, na kiukweli umepigwa marufuku.

Sasa hili linasambazwa kwenye mitandao ya kijamii maana kuna hili la kushawishiana, la pili wote sisi askari inabidi tuwe na masikio marefu na pua zifanye kazi vizuri na akili.

Kuna watu wanafanya fanya hayo kushawishiana, tufanye upelelezi, tuchunguze. Yeyote atayefanya hayo kushawishi tukimng'amua tuweze kumkamata. Tumkamate na tuweze kumhoji wana sababu gani, wana nia gani wanataka kufanya vitu vya kushawishiana kufanya vitu vya namna hiyo.
Msangi maandamano yako palepale hata upige yowe vipi nakushauri kaa kimya zoezi hili likiisha usije kupoteza kazi
 
Ni ukweli katiba inaturuhusu tufanye maandamano na tutafanya kwa mujibu wa katiba yetu acheni kusigina katiba yetu huu ni ubabe
 
wajameni.hata kama katiba inasema.lakini kuna by laws mbalimbali katika.ku tacilitate.hilo..haipo tu kiholela eti unaamka.asubuhi unaenda kuandamana..angalieni.msije jutia.kuzaliwa..acheni mambo.ya kijinga ambayo hayawasaidii.hata kuwaongezea shilingi kwenye.akiba yenu。labda kama mnalipwa kwa kazi hiyo..kama mnalipwa basi nendeni mkavunjwe miguu mbaki vilema..ndio faida yenyewe tu mtakayobaki nayo.sawa !!
 
DEMOPHOBIA..............huu moto huzimiki kwa vitisho
tukutane 26/04/2018
 
Ushauri wangu ni kwa wakuu wote wa mikoa ambao walikuwa maafisa wa jeshi/walipitia JWTZ,acheni mara mroja kukiuka KIAPO chenu,,,laana ya kwenda kinyume na kiapo cha utii na kuitetea katiba KITAWAMALIZA.
 
Jeshi la Polisi Jijini Mwanza limeaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.

RPC Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuna umuhimu wa kufanya mazoezi sana ili uwe na pumzi na muscles zikaze ili at least pale unapotaka kufanya shughuli zinazotumia nguvu na tuweze kufanya shughuli vizuri kwa ufanisi.

Nafikiri wote sasa hivi mnafahamu kuna hii mitandao ya kijamii kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu, na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa, na kiukweli umepigwa marufuku.

Sasa hili linasambazwa kwenye mitandao ya kijamii maana kuna hili la kushawishiana, la pili wote sisi askari inabidi tuwe na masikio marefu na pua zifanye kazi vizuri na akili.

Kuna watu wanafanya fanya hayo kushawishiana, tufanye upelelezi, tuchunguze. Yeyote atayefanya hayo kushawishi tukimng'amua tuweze kumkamata. Tumkamate na tuweze kumhoji wana sababu gani, wana nia gani wanataka kufanya vitu vya kushawishiana kufanya vitu vya namna hiyo.
Kwanza kamanda ajue kuandamana sio uhalifu wala kosa katiba imeruhusu na kuandamana ni kutembea ukiwa na ujumbe ila mara nyingi vurugu huanzishwa na polisi kuanza kupiga watu wanaotembea
 
Back
Top Bottom