Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,115
- 79,527
PONGEZI KWA POLISI WA MOROGORO.
Na, Robert Heriel
Jana nimefurahishwa na kile nilichokiona pale Morogoro, Polisi wa Morogoro Mungu awabariki sana.
Jana Lissu alikuwa akikatiza maeneo ya Morogoro Mijini akielekea Iringa, kwa kazi ya kutafuta Wadhamini. Nilifurahishwa na namna polisi walivyoupokea msafara wa Lisu, kutoa maagizo ya namna watu watulie kwa ajili ya kumpa nafasi Lisu aongee, kisha kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa, hatimaye kumsindikiza mpaka alipotokomea kunako barabara ya Iringa.
Hivi ndivyo tunataka polisi wetu wawe, Polisi ni ndugu zetu, wapo kaka zetu, dada zetu, waume zetu, wajomba, Baba,nk. Polisi wanaowajibu wa kuhakikisha sisi tupo salama na mali zetu.
Polisi wapo kwa ajili yetu, kwa ajili ya wananchi wote, Polisi hawamilikiwa na dini fulani, kabila, au chama fulani. Polisi ni mali ya wananchi. Sisi ndio tunawapa mishahara, tunawapenda,
Sisi kama watanzania hatupendi kusikia Vyama pinzani vikilalamikia jeshi letu la polisi kuwa haliwatendei haki, kwa nini lisiwatendee haki ikiwa nao ni watanzania.
Polisi pamoja na kada zingine nafahamu wanajitambua, najua wanaipenda nchi yao, nafahamu wanajua kuwa vyama vya siasa ni kama club za simba na Yanga, Polisi hapaswi kuwa na chama, lakini hata kama anacho hapaswi kupendelea.
Polisi sio mali ya kiongozi wa serikali, polisi ni mali ya wananchi,
Viongozi wabaya huweza kuiharibu sifa ya polisi kwani huweza kuwatumia kwa maslahi yao binafsi na wala sio maslahi ya taifa. Viongozi wa kisiasa msiwatese ndugu zetu, msiwafanye waona kazi ya upolisi ni kazi ngumu, na ugumu wa kazi ni pale unapoambiwa utende jambo ambalo si la haki.
Kwa kweli katika moja ya mambo magumu yanayoweza kuwapata ndugu zetu polisi ni kuamrishwa kufanya jambo ambalo sio haki. Wanaumia, wanateseka, hakuna jambo baya kama kufanya kitu ambacho unaona kabisa sio halali.
Hakuna kitu kigumu na kibaya kama kupendelea.
Kazi ya Upolisi ni kazi ya heshima, lakini viongozi wabaya na polisi wasio waaminifu ndio huiharibu.
Polisi wa Morogoro ni mfano wa polisi wengi hapa Tanzania wanaojua kazi zao.
Polisi na kada zingine msikubali kutenda mambo yasiyo haki. Huko ni kutafuta laana kwenye kizazi chenu.
Waache wajinadi, wapeni uwanja sawa, kila mmoja afuata sheria, hakuna kupendelea mtu, atakayeshindwa ashindwe kihalali, sio kumnyima mtu nafasi, haipendezi.
Bado vyombo vya habari.
Inashangaza kutokuona habari za Tundu Lissu kwenye chombo cha taifa kama TBC, hivyo vyombo vingine tunajua ni binafsi hivyo hatuwezi kumpangia mtu na biashara yake kuonyesha mambo tunayotaka sisi wananchi, lakini TBC ni chombo cha UMMA, kinaendeshwa na Kodi za Watanzania.
Taikon ninashauri, watu watende haki, na kiongozi yeyote ambaye hataki kutenda haki huyo hatufai.
Taikon nawapongeza Polisi wote wa Morogoro.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300