Pongezi kwa JF mpya na management team yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi kwa JF mpya na management team yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, May 28, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kabla sijaizoea JF mpya niliona kama taabu vile kuitumia lakini kwa sasa nimeona jinsi ilivyo nzuri kuliko ile ya mwanzo. Kwa sasa kuweka picha, ku-attach file n.k. ni rahisi na pia mwonekano wake ni mzuri kadri mtu unavyo itumia zaidi.

  Napenda basi niwapongeze wote wanaojitolea kutupa nafasi hii adimu ya kutoa mawazo yetu kwa jamii. Maxence, Invisible na wengine nisio wajua nawapongezeni sana na msikate tamaa kwani juhudi zenu kwa kuelimisha umma wa watanzania zinatambulika na Mungu awaongezee nguvu.

  Imekuwa vigumu kwangu binafsi kubadili status yangu hapa JF kwa sababu ya mahali nilipo lakini naahidi kufanya hivyo ndani ya muda mfupi ujao baada ya kukamilisha kazi zangu hapa nilipo.

  Nawashukuru pia JF members kwa constructive contributions na ideas zao hapa jamvini, nawaomba tuongeze nguvu sasa hasa tunakoelekea kwenye uchaguzi, Mungu awape nguvu.

  Naomba kila mwanaJF kwa nafasi yake ktk ofisi yake mahali alipo ajitahidi kufukunyua uozo wa watendaji wa serikali na mashirika yetu ya umma, hasa wale wanaotarajia kugombea nafasi mbali mbali na uozo huo uwekwe hapa ili jamii ijue. Tusiwe waoga kama ukipata uozo huo na unaogopa kuutundika hapa wasiliana na invisible ili aweze kuutundika hapa.

  Kwa leo ni hayo nawatakia ijumaa njema.
   
Loading...