Pongezi kwa jeshi la polisi hususani kitengo usalama barabarani

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Nimesafiri zaidi ya km 6,000 kwa gari mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka huu.Nimeshuhudia uwepo na umakini wa hali ya juu askari wa usalama barabarani.

Sikuweza kuona ajali yoyote,waendeshaji vyombo wapo makini kufuatia sheria.

Asanteni sana wadau wote, mabasi sasa si mabucha ya binadamu tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu Mkinunua magari yenu binafsi mrudi hapa kuendelea kuwasifia hao ma'traffic'.


Sent from my iPhone using ZXJamiiForums

Huo uzi polisi wameamua kucheka kwa kujitekenya wenyewe. Wa kuwapa pongezi nyie kama si wenyewe basi ni jiwe aliyewatuma kukusanya mapato.
 
Huo uzi polisi wameamua kucheka kwa kujitekenya wenyewe. Wa kuwapa pongezi nyie kama si wenyewe basi ni jiwe aliyewatuma kukusanya mapato.
Hili jambo ni jema sana, zamani ukisafiri kwa bus, kila mmoja anajikabidhi kwa Muumba kwa imani yake. Abaki lilikuwa njenje.Leo usafiri public ni Salama zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesafiri zaidi ya km 6,000 kwa gari mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka huu.Nimeshuhudia uwepo na umakini wa hali ya juu askari trafic. Sikuweza kuona ajali yeyote,waendeshaji vyombo wapo makini kufuatia sheria.
Asanteni sana wadau wote, mabua sasa si mabucha ya binadamu tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mh
 
Punda haendi bila ya Viboko
Bila ya Kibano Cha Polisi hali ingekuwa mbaya zaid

Jeshi la Polisi liongeze Tochi barabarani maana Muafrica Sheria bila ya adhabu kali Ni kazi bure
 
Mi nafurahi tu dereva wa basi akitaka kwenda kinyume na speed limit king'amuzi kinalia, dereva anakuwa mpoLee anapunguza. Safari inakuwa salama salimini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina cha kuwapongeza ila Mungu awabariki waendelee kusumbua wenye magari barabarani kwa kudai ile mambo yao wanaita ya kubrashia viatu.
 
Punda haendi bila ya Viboko
Bila ya Kibano Cha Polisi hali ingekuwa mbaya zaid

Jeshi la Polisi liongeze Tochi barabarani maana Muafrica Sheria bila ya adhabu kali Ni kazi bure

Pana uzi humu ulikuwa ukielezea waliopo kwenye daladala wanavyochukia waonavyo wengine wako kwenye magari madogo. Katika comments zilizokuwapo kuna zilizo watambua wenye madera kuwa na hasira zaidi.

Au mkuu wewe ni mmoja wa waliokuwa referred kuwa ni wale wenye madera?

Si ungemalizia kabisa kuwa tochi hizo ziwe zisizo ona magari yenu PT, STL, DFPA pia yale ya chama pendwa?
 
Kweli ajali zimepungua sana hasa kwa magari ya abiria. Lakini waendesha mabasi bado wanaendesha bila kuchukua tahadhali. Overtake zao nyingi bado zinaenda bila kujali kwamba barabara inaruhusu ama kuna usalama wa kufanya hivyo. Bado wanaonesha kutokuwa makini kidogo wakitumia hasa ukubwa wa bodi za magari yao kunyanyasa wa magari madogo
 
Back
Top Bottom