2020 CCM tuleteeni Bernard Cammilius Membe "Nyundo" , Kamarade asiyehitaji kuongea saana kuonyesha kuwa ni kamanda makini aliyekamilika asiyeogopa kitu isipokuwa wananchi baaasi
Kuna nchi Moja Afrika Magharibi miaka ya nyuma Rais wake alikua Raia , alichaguliwa kwa Kura na sio mapinduzi kama ilivyokua kawaida ya nchi nyingi za Afrika Magharibi .
Alipoingia Madarakani akawa anatamani kuendesha nchi Kijeshi lakini alipata upinzani Mkubwa toka kwa wananchi hasa alipokua anawadhalilisha Raia na hata wanajeshi.
Walijitokeza wanaharakati na kumwambia kama anafikiri nchi kuendeshwa kijeshi ndio kuwaletea wananchi Maendeleo basi aachie nchi Jeshi ili Itawaliwe na wanajeshi waliofuzu Kwenye Medani za kivita na kimapambano na sio RAIA kuendesha nchi kijeshi na kutoa amri mpaka zile zinazotolewa ndani ya majeshi na maafisa wa kijeshi wenyewe.
Alikumbushwa pia kufuata Katiba ambayo inatenga majukumu ya Kijeshi na Shughuli za vyama na siasa ili isije ikatokea wale wanajeshi wanaoamini katika vyama tofauti nao kuibuka na kuonyesha uanachama au ukereketwa kwenye vyama vingine au hata kuanzisha Vyama.
2020 tutamsikiliza na kumpima Jasusi Mbobezi Bernad Membe.Tutampa kura kama ataonyesha umahiri na uwezo wa kutueleza jinsi atakavyoweza kutatua Changamoto zilizokuwepo na zile zijazo.
Atashughulikia vipi ufisadi ,wizi wa mali za umma, Ugaidi, Umaskini, Elimu duni, Ukosefu wa ajira, Demokrasia,Wizi wa Kura, Katiba mpya, Suala la utekaji,utesaji, chuki za kisiasa, kukua kwa kasi kwa ukabila na ukanda, wanasiasa hasa wa Chama chake kuhamasisha mauaji na kujeruhi wapinzani wao , kuingiza vyombo vya dola kwenye siasa.
Lakini pia atueleze kuwa atakijenga vipi Chama cha mapinduzi bila kutumia Dhulma ,rushwa,Risasi na mabomu,vitisho na kila aina ya hujuma.
Anyway 2020 ikifika tutasikia mengi.
Lakini pia tusimwamini sana Jasus Mbobezi kwa sababu inawezekana ni mbinu mojawapo ya kijasusi kuwaondoa wananchi kwenye muelekeo wa kuviunga mkono wapinzani baadae anaweza akakamilisha kazi yake kwa kusema nimeamua kuunga mkono Juhudi mana niliyokua nayapigania yote yametekelezwa.
Wekeni akiba pia mana CCM ni wale wale linapokuja suala la Chama.