Pongezi kwa Benard Cammilius Membe

Pongezi kwa Benard Cammilius Membe

View attachment 1169300


Kwanza nikiri kwamba wewe ni mtu shujaa sana, wale waliokuunderestimate hapo mwanzoni kutokana no move zako za kimyakimya zisizoacha traces sasa wanaumia kichwa na kushangazwa na jinsi unavyosukuma kete kwa utulivu.

Wao walikuwa wa kwanza kusema Huyu Membe yuko wapi, mbona hatumsikii?, Ulipojitokeza na kuanza kusikika walewale wakaanza kusema, Oooh wastaafu msiongeeongee!. Ajabu sana hii, Wazungu wanasema you are damn if you do and you are damn if you don't!

Mwezi uliopita ulisimama kiume kukemea matendo ya kinyama ya utekaji nchini, Kishindo na mwangwi wa kauli yako ulisikika vilivyo, hazikupita wiki mbili msaidizi wako akatekwa!. yote hii ni kujaribu kukprove wrong kwamba "tutakuonyesha kuwa sisi ni akina nani". Lakini wasichokijua ni kuwa wananchi hatupendi mambo ya Kiinterahamwe Interahamwe, Hatupendi ukatili, na mambo ya uonevu.

Lakini juzi hapa ndo umefunga kazi moja kwa moja, Waliovujisha sauti za mazungumzo yako walitegemea utanywea, utaogopa na kwa kufanya hivyo watakuwa wameua ndege wawili kwa jiwe moja, kwamba wamekuchafua mbele ya jamii lakini pia kukutisha, kukuogopesha. Lakini aaaah wapi ukaibuka ukasimama ukasema NDIYO HIYO SAUTI ILIYODUKULIWA NI YANGU SO WHAT?

Uzuri wa kauli hii ni kwamba sasa sisi wananchi tunasympathize na wewe zaidi kwa sababu umedukuliwa ukiwa na mazungumzo private, kauli ulizozingumza hata sisi raia wa kawaida huwa tunazizungumza daily na wakati mwingine huwa tunatoa kauli kali zaidi kuliko ulizotoa!. KAMA WANAJUA SANA KUDUKUA BASI WADUKUE WANANCHI MILIONI 10 AMBAO TUKIWA PRIVATE TUNAPIGA "NYUNDO" KWELIKWELI, LAKINI TUKIWA PUBLIC TUNASIFU JUHUDI!

Mheshimiwa, Umesaidia Jamii kuionyesha kuwa mambo ya udukuzi yana consequence zake yakitumika kiholelaholela, wapo wadukuzi professionals wakijua kuwa bongo Udukuzi "Dili" watakuja hapa na kudukua watu nyeti halafu wawablackmail kwa ajili ya concessions kibao!. HAWA WANAODUKUA NA KUONA SIFA KUZIACHIA WAJUE WANAKARIBISHA WAHALIFU WAKUBWA WANAOWEZA KUHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU!

Lakini Kikubwa Kauli yako ya "KIBABE" imetusaidia kuyaweka makampuni ya simu kwenye kikaango, leo yatajua kuwa japo yanatudukua lakini kuna consequence zake yakianza kuachiaachia maongezi yetu ya Faragha, Leo kama Voda watapoteza mteja hata mmoja nalo ni somo kuwa you can't be a pirate wa taarifa za watu na ku go away with it kirahisi

Kwa hiyo nimalizie kwa kusema, Pole sana kwa kudukuliwa, Kwa hakika Udukuzi uliofnaywa dhidi yako ni kinyume cha sheria za nchi. Maneno uliyoongea kwenye ule udukuzi ni ya kawaida sana, sisi wananchi trust me tunaongea makali zaidi ya hayo.

Lakini pia umetusaidia kujua kuwa kumbe wewe ni mtu wa watu, jinsi ulivyokuwa ukiongea kwa passion na kwa heshima na yule katibu kata inaonyesha kwamba wewe ni mtu wa watu mwenye kuheshimu watu wote mkubwa kwa mdogo na kwamba wewe siyo "ELITIST"

Sasa basi kama nilivyokuandikia barua ya wazi siku zilizopita, endelea kusimama kiume na kuonyesha msimamo usioyumba kwa mujibu wa Sheria za nchi na kanuni za Chama cha Mapinduzi. Wananchi wanataka Unafuu wa maisha dhidi ya hali hii ngumu sana waliyokuwa nayo, Watumishi wanataka stahiki zao kwa mujibu wa sheria ya wafanyakazi,Wakulima wa korosho wanataka kulipwa haki zao baada ya zao lao kuvurugwa na wastaafu wanataka walipwe fedha zao bila kusumbuliwa Lakini kikubwa wananchi wanataka hali ya hofu nchini itoke, watu waache kutekwatekwa, na vijana wapate ajira.

Kwa hiyo "BRAZA" MEMBE, Ni muhimu kuchukua Fomu, Who cares, Chukua fomu mambo mengine yaache yaende kwenye process, kama ipo ipo tu, kama haipo basi kwani shida iko wapi?

Mnavyozidi Kumjambisha ( Kumsifia / Kumpamba ) hivi ndiyo mnazidi Kumuharibia na Kumponza. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
2020 CCM tuleteeni Bernard Cammilius Membe "Nyundo" , Kamarade asiyehitaji kuongea saana kuonyesha kuwa ni kamanda makini aliyekamilika asiyeogopa kitu isipokuwa wananchi baaasi
Ukiona mtu anajifariji kwa mawazo ya ujinga wa aina hii..ni dalili akijaliwa kufika miaka 50 kuna chances kubwa za kurukwa akili!
 
Yaani leo ameacha kuwa Bulldozer amegeuka Jembe?
Basi kashuka kiwango sana

Tunaposema neno jembe kimjinimjini tafsiri yake ni zaidi ya bulldozer kifupi ni mchapakazi na watanzania wanahitaji mtu anayeweza kufanyia close monitoring kifupi mbwa kala mbwa..
 
Hizi Mbwembwe Mbona hatukuziona 2015??
 
Hakun
Hakuna cha maana alichofanya hata ktk taasisi yake ya zamani ya ukachelo zaidi ya majungu na fitina,maana ktk vioindi vyao ndipo tumepigwa Sana na wajanja na yeye kama kachelo mbobezi alifanya nini ktk ngazi yake? Ki ukweli hawezi kuwa Rai's wa Tanzania kamwe

Ukachelo
Vioindi
Rai's
Mkuu nenda shule kwanza ukimaliza uje ku comment huenda tukakusoma
 
2020 CCM tuleteeni Bernard Cammilius Membe "Nyundo" , Kamarade asiyehitaji kuongea saana kuonyesha kuwa ni kamanda makini aliyekamilika asiyeogopa kitu isipokuwa wananchi baaasi
Aliyewaroga ana dhambi sana!

Kwahiyo Lisu mmeshamusahau mara hii?
 
Hakun
Hakuna cha maana alichofanya hata ktk taasisi yake ya zamani ya ukachelo zaidi ya majungu na fitina,maana ktk vioindi vyao ndipo tumepigwa Sana na wajanja na yeye kama kachelo mbobezi alifanya nini ktk ngazi yake? Ki ukweli hawezi kuwa Rai's wa Tanzania kamwe
Mimi nakupendekeza wewe ugombee urais 2020. Naona una mengi ya kutufaa sana chief.
 
Ukachelo
Vioindi
Rai's
Mkuu nenda shule kwanza ukimaliza uje ku comment huenda tukakusoma
Shule nitakwenda mkubwa Ila Membe hawezi kuwa kiongozi wa nchi hii kwani hakuna cha maana alichofanya
 
Tanzania imejaa watu wanafki ni x1000 Yohana aendelee kushikilia madaraka.
 
Back
Top Bottom