Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,723
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu kwenye Nipashe ya leo. Ni makala ya pongezi kwa INEC kuanza kusawazisha uwanja tenge wa uchaguzi kwa wagombea 17 wa urais kwa kuwawezesha angalau angalau kufanania fanania kwa kuwapatia usafiri!, hivyo wataweza kufika popote ndani ya Tanzania hii. Vipi kuhusu kuiwezesha Media ili iweze kuwawezesha Watanzania kufanya an Informed Decision?, au uwezeshaji ni kwa wagombea tuu, media tujibebe wenyewe?. Tutashuhudia good media coverage kwa vyama dume vyenye ukwasi mkubwa, hala vyama makapuku... sijui!.
Makala ya leo ni pongezi kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuanza mdogo mdogo kusawazisha uwanja wa kuchezea mchezo wa siasa, ambao kwa muda mrefu, umekuwa ukilalamikiwa kuwa ni uwanja tenge!.
Uchaguzi wa Tanzania kwa muda mrefu umekuwa ukilalamikiwa, na kufananishwa na mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwaenye mpini, akiwaekezea washindani wake upande wa makali kuwili kuanza kuvutana.
Kuna chama kimoja ni chama dola, chama dume, kina dola kibindoni kwake, kina watu wenye ukwasi na rasilimali za kutosha, kinashindana na vyama makapuku wasio na kitu chochote, apeche alolo!.
Safari hii ni tofauti, INEC imefanya uteuzi wa wagombea 34 wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais kutoka vyama 17 vya siasa vilivyochukua fomu za uteuzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amefanya uteuzi huo baada ya wanachama waliopendekezwa kutimiza masharti ya Ibara ya 39(1), 41 na 47(4) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, zikisomwa pamoja na kifungu cha 34 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024.
Mhe. Jaji Mwambegele amesema kutokana na kutimiza masharti hayo, kwa mujibu wa kanuni ya 20(5) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewateua wagombea hao.
Baada ya uteuzi huo, Mhe. Jaji Mwambegele amewakabidhi wagombea hao seti moja ya fomu za uteuzi pamoja na nakala moja ya Tamko la Kuheshimu na Kutekeleza Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 kwa ajili ya kumbukumbu zao.
Mhe. Jaji Mwambegele amewapongeza wagombea hao kwa kuteuliwa na kuwatakia kampeni zenye mafanikio na kuwakabidhi wagombea wa Kiti cha Rais gari moja jipya aina ya Landcruiser GX VXR pamoja na dereva kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.
Kipenga kimepulizwa kampeni za uchaguzi zimeanza tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara wakati kipindi cha kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar itakuwa tarehe 28 Agosti, 2025 hadi 27 Oktoba, 2025 ili kupisha kura ya mapema na Tarehe 29 Oktoba, 2025 siku ya Jumatano itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura.
Kitendo cha INEC kutoa magari na madereva kwa wagombea wote wa kiti cha urais, ni hatua inayostahili kupongezwa kwa dhati, ni hatua ya kwanza ya kurekekebisha ule uwanja tenge, sasa hakuna tena mgombea urais atakayeshindwa kufika popote, ila kwa vile vyama vingine ni dholfu bin taabani, kwa mgombea wake aliyekuwa anakosa hata elfu hamsini ya kulipia fomu, ,mafuta ya gari aina ya Landcruiser GX VXR, kuzungukia nchi nzima!, bado ni mtihani!.
Sasa uchaguzi wa Tanzania, unaanza kufanana fanana na chaguzi za nchi za Scandnavia na Nordic, kwa kuhakikisha wagombea urais wote wanafanania. Baada ya Tume kuwapa magari, idara nyingine za serikali nazo zifanye kama ilivyofanya tume, sisi wa jicho la tatu, tunajua kuna mgombea anatumia magari ya serikali yenye number za kiraia, anajaziwa mafuta, na anawasadizi, ikiwemo ulinzi, media na logistics support.
Wagombea wote wa urais pia wapewe mafuta, wapewe ulinzi, kama mmoja ana ving’ora, wagombea wote wa urais pia wapewe vingo’ra, kama mmoja ana PA ya serikali na ana media ya serikali, wagombea wote pia wapewe PA na wapewe media support, ili Watanzania wote tuwasikie wagombea wote 17, ili siku ya uchaguzi, tufanye chaguo sahihi.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima ameahidi katika kipindi hiki cha uchaguzi, Tume itashirikiana na waandishi wa habari kupitia njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na televisheni, pamoja na kutoa taarifa rasmi kwa wakati unaofaa ili kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa habari za kweli na zisizo na upotoshaji.
Mkurugenzi wa Uchaguzi amesisitiza kuwa Tume itatoa taarifa sahihi na kwa wakati, na itatoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kila wanapohitaji ufafanuzi au msaada wowote wa kihabari.
Aidha, Ndugu Kailima ameeleza kuwa Tume itazindua mfumo wa kusajili vyombo vya habari kuanzia tarehe 1 hadi 30 Septemba 2025.
“Mfumo huu utasaidia vyombo vya habari kupata vibali na vitambulisho rasmi vya waandishi wake kwa ajili ya kufanikisha kazi zao wakati wa Uchaguzi Mkuu,” ameeleza.
Kufanyika kwa mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kumehitimisha mfululizo wa mikutano ya wadau ambayo ilianza tangu tarehe 27 Julai 2025, ambapo Tume ilikutana na viongozi wa vyama vya siasa, asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na watayarishaji wa maudhui ya mtandaoni
Kama Tume ilivyowezesha wagombea urais kwa kuwapa magari, sisi media nasi, ili tuweze, media pia inahitaji kuwezeshwa ili kuwapa fursa Watanzania, kuwasikia wagombea wate 17 wa urais. Bila kuwezeshwa, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na watayarishaji wa maudhui ya vipindi kwenye redio zetu, televisheni zetu na mtandaoni, hawewezi kuandaa maudhui ya maana bila ya uwezeshaji au kuwezeshwa.
Bila Tume kuwezesha media, mtashuhudia habari za mgombea mmoja zikitawala vyombo vyote vya habari, kwasababu ni wa chama chenye uwezo, wengine, mtaishia kuwasikia, wapo kama wapo, lakini hawapo na hamta wasikia!.
Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali