:nimekataaSheikh Ponda Issa Ponda, mimi na muangalia kwa jicho la kipekee sana tofauti na vile alivyochorwa na vyombo vya habari na serikali kwa ujumla..nguvu yake ya ushawishi ni kubwa mno kuliko tunavyodhania tulivyo wengi. Labda nimtoe wasiwasi mjumbe mmoja alietangulia kusema,"Ponda sisimizi tu hawezi vieka vyombo vyote vya usalama busy kiasi hicho..." si vyombo vya usalama tu bali nchi yote kwa ujumla, tuache kejeli na dhihaka katika masuala mazito kama haya. Labda nikupeni mfano wa kariakoo; yale maandamano ya watu wanaoitwa wachache tu ndio yaliosababisha serikali kutumia nguvu kubwa kuyatuliza wakiwemo Mgambo wa jiji, polisi wa kawaida, polisi kanzu, kikosi cha kutuliza ghasia na hata tuliona JWT wakienda kuimarisha ulinzi labda unaweza kuona ni jinsi gani ana nguvu ya ushawishi japo yu mahabusu.
Sheikh Ponda, ni mwanaharakati wa kiislam na anaathiriwa na misingi ya imani na mafundisho yake katika maisha yake ya kila siku, ikiwemo kutembea, kuzungumza na hata anapoona vitu haviendi sawa anajukumu la kulikemea kama vile anavyoelekezwa na Misingi ya imani yake...hivyo mimi sioni kama kunahaja ya kumlaumu; Mathalani kiongozi yeyote wa imani ya Kikristo anapoongea na waumini wake ananamna anavyokua anaathiriwa na imani yake katika kukemea maovu kulingana na misingi ya imani yake kwamba Ukipigwa kofi kulia mgeuzie kushoto kama masihi alivyofundisha bi maana ukiona ovu muachie Mungu ndo anajua atahukumu vipi, Hali kadhalika kwa Sheikh Ponda anaelekezwa na kiigizo chema chake na waislam wote(Mtume (s.a.w)) ambae ni mwalimu wa walimu kwamba usikubali kudhulumiwa ama kudhulumu mana ni uovu, na unapoliona ovu basi litowe kwa mikono yako(Sheikh Ponda kwenye nchi isiyo na dini hana mamlaka hayo na nisingependa ifikie hapo mana hatutopata hata muda wa kupashana habari na kuelimishana kama ivi ila ana njia mbadala), ama kama ukishindwa likemee(Ndio maana kila siku unamsikia akikemea kwa nguvu zote maovu yote) na akishindwa kabisaaaaaaaaaaa basi achukie(ambapo ni udhaifu wa imani). Kwa nukta hiyo basi, hata akitoka huko gerezani bado ataendelea na msingi uleule wa imani yake na hakuna wa kumsimamisha isipokuwa ni Muumba anaemuamini, labda kwa faida mana huenda wengine hamkuwa mmezaliwa Sheikh Ponda alisha kaa nje ya nchi kwa vikwazo nayo ilikua ni kwa kazi yake hii hii na hata aliporudi hakuna aliemstopisha bado aliendelea kukemea maovu.
Labda nimalize kwa kusema kinachotakikana hapa nchini ni kutambua wapi mmetofautiana kiimani na kuheshimiana kiimani na si kuvumiliana mana unapovumilia kitu inafika mahali unaudhika ambapo huwezi vumilia tena. Sisi tuwe mabalozi huko mitaani mwetu juu ya kuheshimu misingi na matukufu ya imani nyingine ili mmomonyoko wa maadili ambao vijana wasasa wanao ukome. Pili, media zetu zijitahidi kusema kweli pale wanaporipoti habari na kujaribu ku-balance hizo habari ili isije ikawa ni chanzo cha vurugu. Tatu, serikali iache kupuuza malalamiko ya jammii hii ya waislam hapa tanzania ili ile Psychologia ya kushindwa walionayo waumini wengi wa jammii hii na kujiona wao kama 2nd class ikome. Naomba kuwakilisha x x x x:shut-mouth: