Pombe yapata Suluhu, Suluhu apata Mpango

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
25,360
38,869
Kiukweli ninakoshwa sana na hawa jirani zetu.katika gazeti lao Taifa letu alipokufa magufuli waliandika "Pombe yapata Suluhu " alipoteuliwa Mpango wakaandika " Suluhu apata mpango" .

Ukitafakari kwa kina Wahariri/waandishi wanatumia vizuri lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe ambao kiukweli unafikirisha na msomaji/wasomaji anaweza kutafakari na kufikia hitimisho kwa namna inayoweza kumridhisha msomaji.

Waandishi wa habari Tanzania mna la kujifunza kutoka Kenya. Ubunifu.
 
Mimi nilishangazwa sana na baadhi ya watanzania ambao walipandwa na hamaki, kisa ubunifu huo wa hali ya juu kutoka kwa wahariri wa Taifa Leo.
Hio ni 'word play' tu, jambo ambalo ni la kawaida sana hata kwenye 'captions' za taarifa za habari kwenye Tv nchini Kenya. Kusema "Tz yapata Suluhu baada ya Pombe" au "Suluhu apata Mpango Tz" sio matusi wala dharau.
Bali ni sanaa tu ya lugha na ubunifu wa kucheza na maneno, kwa lengo la kuwavutia wasomaji wa magazeti kupitia vichwa vya habari vinavyofikirisha na kusisimua mawazo yao.
Ebdl4RLWAAAxZVP
 
Kabisaa
 
Huyo prof naona mumempeleka kwa masuala ya sheria na katiba pamoja na anavyopenda kukariri zile historia zake za jinsi Tanzania iliikomboa Afrika na mlimpiga sijui Id Amin mara Comoros.....hehehe na alivyofuata dawa ya Corona Madagascar....
Anyway, labda atawapa matumaini ya katiba nzuri kama ya Kenya.
 
Mimi nilishangazwa sana na baadhi ya watanzania ambao walipandwa na hamaki, kisa ubunifu huo wa hali ya juu kutoka kwa wahariri wa Taifa Leo.
Hio ni 'word play' tu, jambo ambalo ni la kawaida sana hata kwenye 'captions' za taarifa za habari kwenye Tv nchini Kenya. Kusema "Tz yapata Suluhu baada ya Pombe" au "Suluhu apata Mpango Tz" sio matusi wala dharau.
Bali ni sanaa tu ya lugha na ubunifu wa kucheza na maneno, kwa lengo la kuwavutia wasomaji wa magazeti kupitia vichwa vya habari vinavyofikirisha na kusisimua mawazo yao.
Ebdl4RLWAAAxZVP

Hawa usipowazoea utapandisha mapigo ya damu bure, hukwazwa na vitu vidogo sana, yaani kama mke unayeishi naye inabidi uwe makini kwa kila neno linalokutoka maana anaweza akanuna mwezi uishe na haukumbuki nini ulikisema kikamvimbisha.
 
Kenya inakatiba nzuri no doubt. Lakin inafuatwa? Tanzani kwanza lazma ijiandae na iandae wana siasa wao kisaikolojia kwanza ndipo katiba nzuri ije. Haina maana kuwa na katiba nzuri kama ya kenya lakn isifuatwe kikamilifu. Uzuri wa katiba sio kumtukuna rais au kubadilisha matokea ya uchaguzi. Kuna zaidi ya hapo. Tanzania isikurupuke kwenda kwenye katiba itakayoishia kwenye makaratasi wakati utawala haujawa tayari. Subira huvuta heri alisema Jomo kenyyata.

Huwa nashindwa kuelewa msimamo wako, kuna siku wewe huandika kama mataga ila siku nyingine akili zinakukaa, kwa mfano hapa umeandika KIMATAGA.
 
Hawa usipowazoea utapandisha mapigo ya damu bure, hukwazwa na vitu vidogo sana, yaani kama mke unayeishi naye inabidi uwe makini kwa kila neno linalokutoka maana anaweza akanuna mwezi uishe na haukumbuki nini ulikisema kikamvimbisha.
Kwa hivyo ni wake zetu hawa, nimejifunza kitu.
 
Back
Top Bottom