lukelo sakafu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 2,938
- 517
Wakuu kuna hii pombe ya ULANZI kule Iringa kwa kweli inaharibu sana watoto hasa wanafunzi. Ukienda maeneo ya Isele, Image, Ifunda, Makete utajionea mwenyewe watoto wa kuanzia miaka 3 wakitembea uku wanapepesuka ovyo ovyo kuna wengine wanaamka na hang over. Wanafunzi wengine wanaenda shule uku wamelewa ULANZI tatizo ni kwamba ulanzi unaweza ugema ata ukiwa porini mchana kweupee kwa hawa watoto uenda porini na kunywa Ulanzi than wanaenda shuleni wamelewa wanapepesuka. ushauri serikali inatakiwa kudhibiti hii kitu hili watoto wasome wasipate division E.