Pombe ni nini? Nimechoka mimi

Pombe ni nini? Nimechoka mimi

ndo maana nasemaa sijawahi onja na sitaonja ng'o! nani anataka shida waii!!
 
Sijui niiweke hii news sehemu gani kule habari mchanganyiko naona kama sio penyewe kule chit chat sipaeLewi kule intelijensia kumejaa wanoko tu siredi itafungwa kule jokes na nin sijui sio paHala pake.
Anyway mada yenyewe ni hivi.

JE ni kitu gani ushawahi kufanya ukiwa umepiga tungi then baadae ukaona umefanya kitu cha kiboya?

Kwangu nshafanya haya.

1. Nishaenda chooni kukojoa baada ya haja nikawa nanawa sasa bahati mbaya nkadumbukiza sabuni choooni....
Kilichofuata niliingiza mkono chooni na kuiibua sabuni huku ikiwa na haramuuuu nkaiosha sabuni kwanza then na mimi nkaendelea kujiosha nayo....daah kila nikikumbuka ni kinya.

2. Nishavua viatu kuingia chooni na baada ya hapo nikalala nje.

JE wewe nini kilikukumba ? Hebu tupia kituko chako cha kweli hapa.

Long weekend.....

Tobaaa. Hiyo ya chooni noooma! Asante sana kwa kunichekesha hapa nusura nianguke lwa kicheko
 
Back
Top Bottom