Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
POMBE yaani kilevi ni hatari sana kwa ukuaji wa uchumi wako! Kwa mfano unakunywa POMBE ile inayo kaa kwenye CHUPA ya KIJANI, inaitwa castle lite (ya gharama) Utajenga nyumba kwa pesa za kibubu?? Huu ni mfano wa kawaida kabisa.
Yaani acha ile kunywa kwa ofa, yaani unakunywa KWELI KWELI ukimaliza kunywa UNALALA MBELE bila kulipa unaishi kwa madeni na kujificha kama kobe! Ha ha ha ha ha ha
POMBE husababisha watu kufukuzwa kazi hovyo hovyo, POMBE humfanya mtu Kukurupuka katika maamuzi, POMBE husababisha mtu kufanya mambo kwa kutafuta sifa! Ndiyo maana utakuta mtu anamaliza mshahara wake baa!
Ukiona mtumiaji wa POMBE anaiongoza vizuri familia yake basi shukuru MUNGU. Ukiona mtumiaji wa POMBE anabana matumizi pia mshukuru sana MUNGU maana wengi hutumia fedha zao vibaya.
Mtumiaji wa POMBE huwa ana mipango mingi mizuri sana hasa ya kukuza uchumi wake na wa familia yake lakini mipango yake haitimii kwa sababu ya Maamuzi ya Kukurupuka au kutaka sifa mbele za watu.
Mtumiaji wa POMBE hujiona yuko juu ya wote. Hujiona baunsa ni yeye, mbabe ni yeye, mwenye nguvu ni yeye! Akili ya mtumiaji wa POMBE humfanya ajione yuko sahihi kila wakati na hataki ushauri!
Kwani hujawahi kuona mtu kanywa POMBE kisha kaleta ugomvi?? Hujawahi kuona mtu kanywa POMBE kisha akataka hata kuvua nguo mbele za watu?? POMBE zikiisha kichwani anatafuta Mjumbe wa nyumba kumi kufanya SULUHU kwa watu alio gombana nao! Upuuzi mtupu!
Ukiona mtumiaji wa POMBE amefanikiwa sana, tazama walio mzunguka! Usimsifie mtumiaji wa POMBE aliye fanikiwa, wasifie wanao mshauri na hasa wanao mpinga kila wakati maana wanamfanya kushtuka kwamba umri haurudi nyuma, kuna uzee, ujana una mwisho na fedha ni maua!
Tufanye kazi, tuweke akiba, tuwe wazalendo kwa familia zetu, tutunze afya zetu pia. Huu ni ushauri wangu wa bure kwenu watumiaji na pia ni funzo kubwa kwa wale wanao onja onja au wanatamani kuanza kutumia POMBE.
NB: Msema kweli ni mpenzi wa MUNGU, hata maandiko matakatifu yanakataza POMBE, muulizeni Nuhu kilimkuta nini baada ya kutumia POMBE.
"Wenye akili pana wame elewa na wata acha kutumia POMBE".