Polsi akataa hongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polsi akataa hongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chamkoroma, Oct 12, 2010.

 1. C

  Chamkoroma Senior Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWeli WAPO wachache sn watu wa aina hii.

  Kweli TZ tunao watu wachache ambao hawako tayari kuuona uozo na ugonjwa wa ufida unaendelea hawa wanaafaa mifano bora katika jamii.
  Frederick Katulanda, Mwanza
  JESHI la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano, huku wanne wakidaiwa kutoa rushwa ya Sh680,000 baada ya kukamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi inayodaiwa kuingizwa kutoka nchi jirani.

  Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alisema jana kwamba watuhumiwa hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti wilayani Magu jijini Mwanza wakiwa na kilo 520 za majani hayo yaliyopigwa marufuku nchini.
  Kamanda Sirro alisema baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walimshawishi Koplo Benson Karokola kuchukua rushwa ya Sh680,000 ili waondoke na kidhibiti chao, lakini askari huyo alikataa.

  Alisema katika tukio la kwanza Oktoba 8 mwaka huu saa 8:45 mchana, Koplo Kalokola alimkamata mtu mmoja (jina tunahifadhi) akiwa na kilo 20 za mirungi ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye dumu la mafuta ya kula la lita 20 eneo la Nata jijini Mwanza.
  “Baada ya kumkamata Bakari, alijitokeza mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Juma Poyo ambaye alimwomba askari huyo kumuachia Bakari na kumtaka apokea Sh280,000 kwa madai kwamba wao ni wauzaji wazoefu hivyo wakipelekwa polisi wataaibika,” alieleza Kamanda Sirro na kuongeza kuwa mtoa rushwa huyo alitiwa mbaroni.

  Alidai kuwa watuhumiwa wengine waliokamatwa Oktoba 9 mwaka huu kwa nyakati tofauti kati ya saa 3:00 hadi saa 4:00 asubuhi wilayani Magu wakiwa na kilo 500 za mirungi walizokuwa wakiziingiza nchini kutoka nchi jirani.
  Alifafanua kuwa mwanamke huyo alishushwa kwenye basi la kampuni ya Zacharia na mwingine kwenye basi la kampuni ya Batco Ltd.

  Baada ya kukamatwa, waliwaweka kwenye gari moja na kupelekwa jijini Mwanza lakini kabla ya kufika kituo cha polisi, mgtu mmoja (jina tunalo) alidandia gari na kumshawishi askari huyo kupokea Sh400,000 amwachie mtuhumiwa.
  “Naye pia aliwekwa chini ya ulinzi na askari huyo na wote kufikishwa kituoni pamoja na fedha hizo. Hivyo tunawashikia wanne kwa tuhuma za kukamtwa na mirungi na kutaka kutoa rushwa huku mwingine kwa tuhuma za kukutwa na mirungi,” alieleza Sirro.
  Kamanda Sirro alimpongeza Koplo Kalokola akimuelezea kuwa ni mfano wa kuigwa na kuwa jeshi hilo linaangalia utaratibu wa kumzawadia kutokana na uaminifu wake.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Well:

  Kinadharia inaonekana amekataa "hongo" : Kivitendo ni kwamba mtoa "hongo" hakuweza kufikia "hesabu" : Polisi nawafahamu sana : Hadi wakufikishe "Kituo" ni ama umekuwa "mbishi" au hesabu haijafika. NUKTA
   
 3. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safi sana, inabidi mambo kama haya TV zetu ziwe zinawaonyesha mashujaa kama hawa, siyo kusema "ukitaka kula kubali kuliwa kidogo" huyo ni kiranja mkuu huku akisema anapambana na rushwa. Crazy crazy crazy, hivi kwa nini tuendelee kupiga kampeni wakati tunajua CCM haina mtu safi? wala wagombea wengi ccm wa ubunge nao ni hovyo?

  Koplo kula tano zangu, nakosa cha kukupa lakini hakika umeonyesha mfano.
   
 4. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Amejitahidi. Mshahara wake ni sh ngapi?
   
 5. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Good Start. kukataa kwako Rushwa kuna Thamani
   
 6. S

  SNAKE HOUSE Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  Good show mkuu ....... mfano wako unafaa uigwe na manjagu wengine !
   
Loading...