DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Ki ukweli kabisa raisi mtaafu wa awamu ya nne ndg. J. Kikwete siasa za nchi yake anaziweza, ukikaa na ukikumbuka jinsi alivyoendesha nchi kwa miaka kumi utaelewa kuwa siasa ilikuwa damu kwake.
Tujikumbushe jinsi serikali yake ilivyopitia misukosuko mikubwa na jinsi alivyopambana nayo, mfn. Richmond, EPA, ESCROW, migomo ya watumishi kama walimu na madaktari, pengine mambo haya yalifanya yeye na chama chake kuja na mbinu mpya za kuimalisha chama kwani aliona upepo unavyoelekea.
Ni mara nyingi amesikika kuwa CCM ilikuwa kwenye hali tete kutokana na siasa za washindani hapo anasema pia asingekuwa katibu mkuu Kinana na Nape Nauye pengine chama kingeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita, pia amewahi sikika akisema waliona pia umuhimu wa kuwa na vijana wa chama mtandaoni (e-politics) ili kuendeleza mapambono ya kuimalisha chama.
Zaidi zaidi siku ya kukabidhi chama kwa mwenyekiti mpya, Kikwete aliongea jambo moja ambalo binafasi nililielewa kwa namana ya pekee ya kuwa " politics is the game of number" yaani kujumlisha, kutoa, kuzidisha au kugawanya idadi ya wafuasi, wapenzi, mashabiki na wanachama, mchezo ambao nahisi magufuli haujui ama anaupuuza, haihitaji uwe MNEC ili ujue kuwa kwa sasa matumaini ya wanachama na watanzania juu ya magufuli yameshuka sana yaani ndani na nje ya chama hali ni mbaya.
Ushauri kwa Magufuli (ingawa umesema mara kadhaa kuwa wewe ni jeshi la mtu mmoja), Mzee asikudanganye mtu wala usijidanganye huku site joto ni kali tafadhari sikiliza kero za wenyenchi unaweza ukafikiri kujenga tu flyovers ndo kusikiliza kero za wenyenchi hapana hali ya maisha huku litapwasi ni mbaya, chakula bei juu na pesa hakuna (hiyo kwangu ndo njaa yenyewe) halafu penda haki wafanyakazi hewa na swala la Bashite limekupunguzia alama na linaendelea kukutafuna.
Si vyema ukajibu kila hoja kwani style unavyojibu mara zote huibui sintofahamu kwa wenyenchi, kwa mfano, kama msimamo ndo huo juu ya makonda tena ulishajua hisia za wenyenchi kwenye mitandao ni vyema usingegusia.... Hata hivyo wale wageni hawakupaswa hata kusikia.... Sikuamini Jana baada ya kauli ile walewale niliowaona wanashangilia walipoona makonda kwenye luninga anataja watuhumiwa wa dawa za kulevya jana wamekasilika baada ya kusikia ile kauli, na huku ni kijijini litapwasi je huko mjini...au wewe kama jongoo unakufa na mti wako???
Mwisho, huo msemo wa Jk ushike sana ninawanafunzi wengi tu walishazungusha mtihani kwa overconfidence na Bashite inaonyesha alikuwa hivyo.