Polisi, yuko wapi musa mbaruku wakala wa chadema igunga?

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,424
62,475
Nimeshtushwa na taarifa kuwa wakala CDM hajulikani alipo tangu uchaguzi uishe, Polisi hawana taarifa japo wamekiri kuwakamata vijana wa CDM na kuwahamishia magereza tofauti bila kuwapa taarifa ndg zao! Je uchaguzi umegeuka utekaji na uuaji wa watu? Je CDM nini mtafanya dhidi ya vijana walioko magerezani? CCM msitupeleke huko tafadhali!

Source: WAPO RADIO
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,424
62,475
Kitu kingine kilichonihuzunisha ni kwamba: Polisi hao wamekiri kuwa wamefanya makosa kuwakamata watu hao bila kutoa taarifa kwa ndugu zao; source: WAPO RADIO
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Ina maana hao vijana wamekosa wadhamini kweli mpaka waozee jela? Halafu mtoa mada acha unafiki wa kusema CDM msitupeleke huko mbona hujalilaumu jeshi la polisi kw kukamata watu hovyo hovyo Igunga na kuwasweka jela bila sababu za msingi? Nakujulisha kama ukiwa mchumi gharama za kuwaweka jela hao vijana ni kubwa kama wangekuwa wamepewa dhamana kwa serikali maskini kama hii iliyojaa madeni kila kona na inayoyegemea wafadhali kila sekta ili ijiendeshe!
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,424
62,475
Kitu kingine kilichonihuzunisha ni kwamba: Polisi hao wamekiri kuwa wamefanya makosa kuwakamata watu hao bila kutoa taarifa kwa ndugu zao; source: WAPO RADIO
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,424
62,475
Mzee wa Rula, nakuheshimu sana, hebu pitia nilichokiandika halafu nionyeshe mahali niliposema CDM msitupeleke huko! Mimi nimesema CCM maana wao ndio engineers wa haya yote, silipwi na wala sina interest na chama chochote cha siasa! napigania haki ya UHAI wa vijana hao, next time kuwa makini unapojibu kitu usiongozwe na ushabiki wa kisiasa Mpwa! Tuendelee kuheshimiana mkuu! Kama kuripoti hilo tukio ndio unafiki basi mimi ni mnafiki zaidi ya CCM
 

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,335
5,509
Mkuu,
ccm ni zaidi ya uwajuavyo!
Waliwapeleka green guard huko Igunga, wamewanyanyasa sana wananchi wa igunga sana huku wakiambiwa ni Mungiki walioletwa na cdm. Usishangae kusikia ameuawa!
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,424
62,475
Yeah ndio hivyo na hawa ndio watu tuliowapa maisha yetu
 

sir henry

Member
Sep 17, 2011
34
1
kila ukiisha Uchaguzi utayasikia haya kuna watoa maoni HASI na watoa maoni CHANYA. DAWA ni TUME HURU (ya UKWELI ) ya UCHAGUZI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom