Polisi yamnasa 'kigogo' wa dawa za kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yamnasa 'kigogo' wa dawa za kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 21, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Polisi yamnasa 'kigogo' wa dawa za kulevya Send to a friend Thursday, 21 April 2011 08:55


  Na Mwandishi Wetu

  JESHI la Polisi Tanzania jana lilimtia mbaroni raia wa Iran, Asaad Azizi likimtuhumu kuwa kigogo wa biashara ya dawa za kulevya. Jeshi hilo limeeleza pia kuwa limefanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo baada ya kuwatoroka mara kadhaa kwenye mitego waliyokuwa wameandaa kumnasa.

  Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Polisi, Godfrey Nzowa aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Azizi alikamatwa juzi eneo la Namanga, mpakani mwa Tanzania na Kenya.

  Alisema alikamatwa akiwa katika harakati za kutoroka nchini na kwenda Kenya baada ya kubaini kuwa polisi walikuwa wakimfuatilia.
  "Wakati tunamkamata hakuwa na dawa za kulevya ila tumekuwa tukimsaka siku zote na mara zote anatutoroka," alisema Nzowa. Azizi anatuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine.
  “Huyu mtu ni mjanja sana, mara kwa mara amekuwa akiwatoroka polisi kila wanapoweka mtengo kwa ajili ya kumkamata,” alisema Kamanda Nzowa na kuongeza:

  “Tulishawahi kumpekua nyumbani kwake Dar es Salaam na tukamkuta na dawa za kulevya lakini alitoroka,” alidai.
  Kamanda Nzowa alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni raia wa Iran ingawa mwenyewe anadai kuwa ni Mtanzania.
  Alisema wanatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote baada ya kukamilika kwa upelelezi. Comments
  0 #3 nkoba 2011-04-21 09:57 Hili jina mbona linafanana na mtu anayeitwa Rostam Azizi ambaye naye asili yake ni Iran? Naamini jeshi la polisi litatumia uzoefu wake wa kitaalamu katika uchunguzi wa uhalifu kuhakikisha mtandao huo unavunjwa kabisa na wahusika serikali ihakikishe sheria inachukua mkondo wake. Ila uwazi unahitajika hapa ili wananchi tuwe na imani na jeshi la polisi. Mtuhabarishe mara kwa mara juu ya maendeleo ya kesi hii. Ahsante kamanda Nzowa kwa hatua hii.
  Quote

  0 #2 Ron 2011-04-21 09:28 Halafu baadaye kesi ikienda korti ushahidi usitosheleze na mtuhumiwa aachiwe huru na huo unga wenyewe tutaambiwa ni sembe, na wapi umepelekwa tumuulize Makamba! ama kweli huu mchezo wa kuigiza wa nguvu za soda hata sijui utaisha lini!
  Quote

  0 #1 laiza 2011-04-21 09:00 Hongera sana kamanda Nzowa, mimi naamini kabisa safari hii mlifanya intelijensia ya hali ya juu kiasi kwamba habari hazikuvuja kumfikia, maana zingemfikia msingempata. Kazeni buti na huyo Assad abanwe atutajie wenzake au wabia wake pamoja na wanaomkingia kifua. Itapendeza kama Mkuu utaweka mambo hadharani baada ya kumbana na akasema yote
  Quote  Refresh comments list

  Add comment
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi ile kesi ya mtoto wa Mengi kubambikizwa madawa ya kulevya iliishia wapi?

  Hivi wale waliokamatwa na "gunia" la madawa ya kulevya kesi yao imeshia wapi?

  Hivi hapa Tanzania kuna mtu alishahukumiwa kifungo kutokana na kukutwa na madawa ya kulevya - heroin/Ccocaine - achilia mbali bange?

  The way I see it - Kesi za madawa ya kulevya ni sawa sawa na kesi za EPA!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hana kesi ya kujibu huyu ni majungu tu haya...walaiwezaje kumakamata mwanzo na madawa halafu wasimstaki....polisi wetu bwana ovyo kabisa
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Nzowa ni waongo na mnafiki

  madawa ya kulevya yanapita mengi tu pale airport yakiwa na escort za polisi huo unafikisi vyema kuutngaza adharani
  atueleze kesi ya mtoto wa mengi imefikia wapi na yeye akiwa mtuhumiwa namba moja..na hayo madawa alikuwa anayatoa wapi..hivi umejiuliza yale madawa yanayokamwatwa yanapekwa wapi..unajua utajiri wa nzowa godfrey

  wacha kabisa kabisa kwanza ukifwatilia sana dili zao kama poliso nzowa anakuondoa fasta airport leo aseme akupata mgao ndio maana alikuwa akimtafuta atuambie kama si kweli issue ya mengi kwa nini wamekaa kimyaaaa....unajua wangapi wamebambikizwa na wako ndani mpaka sasa miaka 20?????? Ni mungu ndie atakaewalipa ila huo wa muiran unafiki tumeochoka atuletee ukweli wa kesi ya mtoto wa mengi
   
 5. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nahisi Aziz hakuwapa pesa wakati huu. Kesi zao huwa haziendelei. Anyway polisi hongera endeleeni na kwa wengine msiishie hapo
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Polisi wetu ni wanafiki kwani criminals wote wakubwa wanawalinda na ikibidi kuwavusha...hapo ujue kulitokea kutoelewana mgao
  kesi zao huwa hawafungwi hao
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,621
  Trophy Points: 280
  hana conection na rostam huyu kweli?
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hivi huu ukoo wa AZIZ kutoka iran mbona unatutesa sana?
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Tutafute ukoo wa bazazi
   
Loading...