Polisi 'yamfilisi' Maradona, wakamata hereni,vidani vya thamani kubwa

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
ROME , Italia
POLISI wa Italia wamekamata hereni za kocha wa Argentina Diego Maradona.

Mamlaka ya mapato ya hapa ilimtembelea kocha katika hoteli Ijumaa na kuchukua hereni na vidani kama sehemu ya malipo kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Napoli ambaye alikuwa akidaiwa kodi.

Mamlaka hiyo ya Jimbo la Bolzano ilisema kuwa iliwaagiza polisi wake kumtaka Maradona akabidhi mali hizo zenye thamani ya dola 5,900. Shirika la Habari la Italia, ANSA lilisema kuwa Maradona alikuwa akidaiwa kodi ya dola milioni 54.

Polisi wa idara hiyo ya mapato katika mji huo wa kusini wa Tyrol walikataa kuzungumzia lolote kuhusu mali hizo za Maradona zilizochukuliwa kutoka kwake hoteli ya Grand Palace mjini Merano atarejeshwa au la.
Mtandao wa televisheni wa Italia umeeleza kuwa vito hivyo vinahusisha pia almasi.

Polisi hawakueleza kama Maradona alikuwa amevaa vidani hivyo au la, lakini walieleza kuwa anatakiwa kulipa kodi anayodaiwa.

Miaka mitatu nyuma, polisi walitaifisha saa mbili aina ya Rolex wakati Maradona alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari mjini Naples.

Maradona, 48, alikuwa nahodha wa Argentina kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986, ambayo waliibuka mabingwa. Aliichezea Napoli kuanzia mwaka 1984 hadi 1991.
 
hii kali, kwa hiyo ina maana kuwa kila Diego akitia mguu Italia atanyang'anywa kitu. Lakini ni vizuri kama wakisema ukweli kuwa wanaomdai ni mafia wa Italia, iko siku watakujachukua suruali yake au kuchukua nguo zake zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom