Polisi wetu tuwabadilishe

13codes

Member
Dec 17, 2016
14
6
Habarini wanajamii,

Nina mpango wa kuandika kitabu kuhusu Jeshi la Polisi kwa ujumla wake, haya mawazo nilikua nayo tangia mwaka jana ila tangia juzi nafsi yangu inaniambia nifanye haraka.

Juzi nilijua nimepanda pikipiki jina marufu bodaboda sikua nimevaa element nilipanda kama abiria polisi walinikamata ila dereva wa pikipiki akachiwa nikapelekwa kituoni nikawekwa mahabusu muda wa masaa matano, ndipo waliponitoa wakanipiga faini ya elfu 30000.

Watanzania wenzangu kwenye kitabu nitakacho andika ni mambo gani muhimu ungependa yasikosekane kwenye hicho kitabu.

NB: Kua huru kusema chochote
 
habarin wanajamii
nina mpango wa kuandika kitabu kuhusu jeshi la polisi kwa ujumla wake,haya mawazo nilikua nayo tangia mwaka jana ila tangia juzi nafsi yangu inaniambia nifanye haraka .juzi nilijua nmepanda pikipiki jina marufu bodaboda sikua nimevaa element nlipanda kama abiria polisi walinikamata ila dereva wa pikipiki akachiwa nikapelekwa kituoni nikawekwa mahabusi muda wa masaa matano, ndipo waliponitoa wakanipiga faini ya elfu 30000.watanzania wenzangu kwenye kitabu nitakacho andika ni mambo gani muhimu ungependa yasikosekane kwenye hicho kitabu

NB:kua huru kusema chochote
Mimi ningekushauri usifanye haraka, kwani una mambo mengi ya kujifunza hasa hasa kuhusu uandishi.
1. Vituo na herufi kubwa
2. Kiswahili - nlipanda sio neno la Kiswahili, kwenye kitabu chako andika: NILIPANDA
3. Kiingereza - sio element, ni HELMET. Hebu nikupe mfano wa mwandishi kwa kutumia maneno haya haya uliyoyaandika hovyo:

Habarini wanajamii!

Nina mpango wa kuandika kitabu kuhusu Jeshi la Polisi kwa ujumla wake. Haya mawazo nilikuwa nayo tangia mwaka jana, lakini katika siku za karibuni, nafsi yangu imekuwa ikinisukuma nifanye haraka.

Juzi nilikuwa nimepanda usafiri wa piki piki almaarufu bodaboda. Kwa sababu ya kutopenda kwangu kuzingatia sheria za usalama barabarani, sikuvaa kofia ngumu, yaani helmet, jambo lililopelekea kukamatwa na askari wanaopenda kuona niko salama wakati wote. Askari hao weledi, waliniweka mahabusu ilhali wakimuachia huru dereva wa pikipiki kwa kuwa yeye alijali usalama wake na kuvaa kofia ngumu. Mimi ambaye nilikuwa na makosa, niliachiwa baada ya kutozwa faini ya shilingi 30,000 ili liwe fundisho na ukumbusho kwangu.

Watanzania wenzangu, kwenye kitabu nachotaka kuandika ambacho kimelenga kuchochea mabadiliko ya tabia na ufahamu juu ya sheria na taratibu za usalama barabarani, ninakusudia kupokea maoni na ushauri......
 
tangia ni kitu gani we mkosoaji?Andika :tangu.
Nimeamini hakuna mkamilifu chini ya jua.
 
Ni upuuzi mkuu kudhani kwamba sikupaswa kukosoa 'eti' kwa kuwa tu mimi si mkamilifu na ndio maana sikuwahi kusema mimi ni mkamilifu.

Asante kwa kunifunza kuwa hatuna neno tangia kwenye Kiswahili, bila usiishie kwangu, endelea kuelimisha uvaaji wa kofia ngumu na condom kwa jamii inayokuzunguka.

Wasalaam,
Mwana Mtoka Pabaya
 
Hivi helmet na condom zote zinakinga vichwa eti???
 
Back
Top Bottom