Polisi wetu jifunzeni kwa SSP Christopher Bageni

SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE!

By Melissa

Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu
Wajifunze nini kwa Bageni? Kuteka wafanya biashara au? Polisi waendelee kudhibiti wahalifu na mahasidi wa nchi basi.
 
Ni kweli lazima watu wajifunze kupitia hili. Mambo yanaenda yakibadilika.
Bagen na wenzie hawakuuwa kwa ajili ya chama, waliuwa watu waliotambulika hawakuwa na hatia ili wapore pesa. Walitumia kodi ya wananchi kuuwa wananchi wasio na hatia kwa uchu wa mali. Hata hivyo, kila mwenye akili lazima ashirikishe ubongo wake vizuri
 
Bageni ana habati mbaya. Ingelikuwa ni enzi hizi za Policcm wala asingefanywa kitu. IGP Mwema alijitahidi sana kuifanya Police kutumikia wananchi na siyo wanasiasa
Labda ulikuwa mtoto wakati ule. Kulikuwa HAKUNA polisi Bali walikuwa policemajambazi Bora Sasa hivi polisiccm.
 
Mkuu umenena vema "Kutii amri halali" ila ni kama wengi wanaishiaga "kutii amri" hawataki kujishughulisha na "uhalali" wa hiyo "amri".
 
Wewe inaonekana fimbo za walimu zilikuwa zinavunjikia sana kichwani mwako!
Maswala ya shule ungeachana nayo tuu maana hata sioni haja ya kujadili shule. Lakini kama jabo hilo linakufariji na taabu zako waweza kuendelea.
 
Siku mwenye haki akipewa mamlaka ya kuongoza nchi na akaunda Tume ya Majaji kufanya uchunguzi wa kina wa maiti zilizokuwa zinaokotwa kwenye viroba, hakika kuna watu wasio tarajiwa watajikuta pabaya sana kwani JINAI haifi! Damu za watu hao pamoja na za kina Saanane, Azori, Aquilina, Mawazo nk nk bado zinalilia HAKI na Mungu sio Athumani, ipo siku HAKI hiyo itapatikana tu!
Huwa sielewa MTU ana kuwa na furaha na AMANI gani baada ya kuua mtu!
 
Jiwe alikuwa wapi kutia mkono wake kwenye kesi hii kumwepusha polisi huyu na kifo?

Haoni kuwa hukumu hii itawatia hofu polisi wake kutii "AMRI" nyingi batili ktk uchaguzi huu?

Ooh, asante Yesu Kristo Bwana na mwokozi wetu kwa kuwa mkono wako wenye nguvu unaokoa watu wako tulioonewa miaka mingi ya kuwa utumwani Misri..

Ama kweli, sasa ninaelewa kuwa kunbe;
.......THE DESTINY OF PEOPLE CAN BE DELAYED BUT CAN NEVER BE CHANGED......
 
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE!

Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu
Huu ujumbe unaenda kwa wote. Hata wale wanaoambiwa wasizisikilize mamlaka zilizowekwa kihalali kisha wakashughulikiwa uwakuta wao na familia zao tu.
 
Kuelewa ni Hadi uwe na akili , ila saluti upunguza uwezo wa kufikiri
 
Siku mwenye haki akipewa mamlaka ya kuongoza nchi na akaunda Tume ya Majaji kufanya uchunguzi wa kina wa maiti zilizokuwa zinaokotwa kwenye viroba, hakika kuna watu wasio tarajiwa watajikuta pabaya sana kwani JINAI haifi! Damu za watu hao pamoja na za kina Saanane, Azori, Aquilina, Mawazo nk nk bado zinalilia HAKI na Mungu sio Athumani, ipo siku HAKI hiyo itapatikana tu!
Hivi huwa najiuliza mtu anayetekeleza maagizo ya ya kipumbavu bila hata kusita anapataga wapi ujasiri wa kufanya uonevu wa kiwango cha GB100 huu.

By the way,thuluma za namna hii Mungu huwa anaziangalia kwa jicho la pekee.hata hao waliochomoka hawako salama,watapata hukumu kivingine
 
Ujumbe mzuri. Askari amefundishwa kutii amri halali, mambo mengine unaona kabisa ni uhalifu alafu unatekeleza. Ipo siku yanarudi kinyume na utabakia peke yako.

Siku hizi naona kuna watu wanatumia ulinzi shirikishi kusumbua watu mitaani kama ilivyotokea kwa studio za mtayarishaji maarufu wa muziki. Sasa waliowatuma watakwepa alafu nyie msiotumia akili zenu mtabakia na msala wenu.

..inategemea.

..ukipiga wafuasi wa upinzani hakuna hatua zinazochukuliwa.
 
Back
Top Bottom