illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,119
Hujajibu hoja unaanza kulalamika sasa kama siyo ile unayoitaka wewe unasubiri nini humu?? Umelazimishwa?? Kila kitu huwa kina ubora wake na kwenye nyakati zake na kamwe hakiwezi kuwa bora miaka yote.. Ni upungufu tu wa akili kutotambua hilo
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?
Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.
Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.
Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.
Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!
sasa unauliza humu kuna ofisi ya polisi suende huko kwao ukaulize kwani wameanza leo huna namba zao au uende kituoni ukaulize mimi najua kazi zao kukagua vitu sasa kama hupendi kukaguliwa wewe una matatizo na umedanganya kenya kuna point nyingi tu wanakagua mimi huko nimekaa miaka mitano mpaka namaliza shule usidanganye mkuu
Mkuu hao maaskari ni wa muhimu kuwepo katika maeneo hayo, ila labda wao wanatumia vibaya uwepo hao hapo. Lakini lengo la kuwepo hapo ni ulinzi kwa kuwa eneo hilo magari yanasimama kuna uwezekano wa uhalifu kutokea kama vile kuporwa gari au kitu cho chote cha thamani. Aidha, kama kunatukio limetokea sehemu wanapewa taarifa wanazuia vyombo vya usafiri na kuchukua hatua stahili. Kuna baadhi ya matukio huwa wanakamata wezi au majambazi, hata hivyo, kwa sababu ya kukosa maadili ndio maana waingilia maswala ya traffic polisi kama vile kukagua usalama ma magari ikiwa ni pamoja na kuchomoa funguo za Boada boda. Nilishangaa Rwanda wasimama kama miti kimya, hawaongei na mtu wala wenyewe kwa wenyewe, halafu wanakuwa na kitu kama radio yenye antanae ndefu imevaliwa kifuani, hata mvua inyeshe hawatoki. Hawa wa kwetu wanatembea tembea na kufukuzana na boda boda hawako makini na kazi ilyowaweka pale.