Polisi wenye silaha huwa wanafanya nini kwenye makutano ya barabara?

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,275
2,000
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?

Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.

Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.

Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.

Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
Nawafahamu hao, hata kwa kuwaona tu sura zao zinatishia amani. NAdhani ni mpango wa Serikali sikivi kuwatia hofu wananchi...
 
Vianelly Vian

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
338
195
Jamii forums hii siyo ile hii imejaa watoto na wanafunzi wengi asaiv nasikitika kushindwa kipata kile ninachohitaji kutoka humu
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,350
2,000
wapuuzie hao wanafunz! wanamaneno ya kijinga wamejaa mmu kaz kupm wamama peace of ---- ndo mana div 5 chungunzima
 
mzee Chibai

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
981
250
Jamii forums hii siyo ile hii imejaa watoto na wanafunzi wengi asaiv nasikitika kushindwa kipata kile ninachohitaji kutoka humu
Hujajibu hoja unaanza kulalamika sasa kama siyo ile unayoitaka wewe unasubiri nini humu?? Umelazimishwa?? Kila kitu huwa kina ubora wake na kwenye nyakati zake na kamwe hakiwezi kuwa bora miaka yote.. Ni upungufu tu wa akili kutotambua hilo

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
kaka cliff

Member
May 18, 2014
45
0
Hujajibu hoja unaanza kulalamika sasa kama siyo ile unayoitaka wewe unasubiri nini humu?? Umelazimishwa?? Kila kitu huwa kina ubora wake na kwenye nyakati zake na kamwe hakiwezi kuwa bora miaka yote.. Ni upungufu tu wa akili kutotambua hilo

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Inawezekana mada imemgusa kwa namna moja ama nyingine, pengine na ye ni askari ndio maana hasomi hoja akaielewa anaishia kulalamika tu
 
Danpol

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
4,590
2,000
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?

Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.

Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.

Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.

Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!

mazao ya dv 5 utayajua tu
 
High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,132
2,000
sasa unauliza humu kuna ofisi ya polisi suende huko kwao ukaulize kwani wameanza leo huna namba zao au uende kituoni ukaulize mimi najua kazi zao kukagua vitu sasa kama hupendi kukaguliwa wewe una matatizo na umedanganya kenya kuna point nyingi tu wanakagua mimi huko nimekaa miaka mitano mpaka namaliza shule usidanganye mkuu
 
nimeuliza humu maana najua kanda maaalum siku hizi ana i pad ana shida kwenye social networks.... igp wa kenya alipendekeza road block ziondolewe..... lakini you dont inspect a vehicle with a smg aissee tatizo hujui rights and responsibility of a citizen vs law enforcers
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,862
2,000
hao maskari unao waona kwenye ma junction ya barabara wana fanya ulinzi....wakipewa info kama kna tukio limetokea wao wanazuia....na wana kagua pia magari kama ya wizi au la
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,350
2,000
mbona kama Flora Msoffe umetoka nje ya mada vile mara mmu hata sijui ndo nini Mungu wangu mada inaongelea polisi wenye silaha kwenye makutano ya magari
nimemjb vianelly vian
mada inasema kuna utoto mwingi hapa jf wanafunz wamejaa hao askar wanakungoja wewe upite!
 
sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,297
2,000
Mkuu hao maaskari ni wa muhimu kuwepo katika maeneo hayo, ila labda wao wanatumia vibaya uwepo hao hapo. Lakini lengo la kuwepo hapo ni ulinzi kwa kuwa eneo hilo magari yanasimama kuna uwezekano wa uhalifu kutokea kama vile kuporwa gari au kitu cho chote cha thamani. Aidha, kama kunatukio limetokea sehemu wanapewa taarifa wanazuia vyombo vya usafiri na kuchukua hatua stahili. Kuna baadhi ya matukio huwa wanakamata wezi au majambazi, hata hivyo, kwa sababu ya kukosa maadili ndio maana waingilia maswala ya traffic polisi kama vile kukagua usalama ma magari ikiwa ni pamoja na kuchomoa funguo za Boada boda. Nilishangaa Rwanda wasimama kama miti kimya, hawaongei na mtu wala wenyewe kwa wenyewe, halafu wanakuwa na kitu kama radio yenye antanae ndefu imevaliwa kifuani, hata mvua inyeshe hawatoki. Hawa wa kwetu wanatembea tembea na kufukuzana na boda boda hawako makini na kazi ilyowaweka pale.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom