Polisi wenye silaha huwa wanafanya nini kwenye makutano ya barabara?

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,117
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?

Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.

Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.

Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.

Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!
 
Nawafahamu hao, hata kwa kuwaona tu sura zao zinatishia amani. NAdhani ni mpango wa Serikali sikivi kuwatia hofu wananchi...
 
wapuuzie hao wanafunz! wanamaneno ya kijinga wamejaa mmu kaz kupm wamama peace of ---- ndo mana div 5 chungunzima
 
Hujajibu hoja unaanza kulalamika sasa kama siyo ile unayoitaka wewe unasubiri nini humu?? Umelazimishwa?? Kila kitu huwa kina ubora wake na kwenye nyakati zake na kamwe hakiwezi kuwa bora miaka yote.. Ni upungufu tu wa akili kutotambua hilo


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Inawezekana mada imemgusa kwa namna moja ama nyingine, pengine na ye ni askari ndio maana hasomi hoja akaielewa anaishia kulalamika tu
 
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?

Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.

Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.

Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.

Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!

mazao ya dv 5 utayajua tu
 
sasa unauliza humu kuna ofisi ya polisi suende huko kwao ukaulize kwani wameanza leo huna namba zao au uende kituoni ukaulize mimi najua kazi zao kukagua vitu sasa kama hupendi kukaguliwa wewe una matatizo na umedanganya kenya kuna point nyingi tu wanakagua mimi huko nimekaa miaka mitano mpaka namaliza shule usidanganye mkuu
 
sasa unauliza humu kuna ofisi ya polisi suende huko kwao ukaulize kwani wameanza leo huna namba zao au uende kituoni ukaulize mimi najua kazi zao kukagua vitu sasa kama hupendi kukaguliwa wewe una matatizo na umedanganya kenya kuna point nyingi tu wanakagua mimi huko nimekaa miaka mitano mpaka namaliza shule usidanganye mkuu


nimeuliza humu maana najua kanda maaalum siku hizi ana i pad ana shida kwenye social networks.... igp wa kenya alipendekeza road block ziondolewe..... lakini you dont inspect a vehicle with a smg aissee tatizo hujui rights and responsibility of a citizen vs law enforcers
 
hao maskari unao waona kwenye ma junction ya barabara wana fanya ulinzi....wakipewa info kama kna tukio limetokea wao wanazuia....na wana kagua pia magari kama ya wizi au la
 
Mkuu hao maaskari ni wa muhimu kuwepo katika maeneo hayo, ila labda wao wanatumia vibaya uwepo hao hapo. Lakini lengo la kuwepo hapo ni ulinzi kwa kuwa eneo hilo magari yanasimama kuna uwezekano wa uhalifu kutokea kama vile kuporwa gari au kitu cho chote cha thamani.

Aidha, kama kunatukio limetokea sehemu wanapewa taarifa wanazuia vyombo vya usafiri na kuchukua hatua stahili. Kuna baadhi ya matukio huwa wanakamata wezi au majambazi, hata hivyo, kwa sababu ya kukosa maadili ndio maana waingilia maswala ya traffic polisi kama vile kukagua usalama ma magari ikiwa ni pamoja na kuchomoa funguo za Boada boda.

Nilishangaa Rwanda wasimama kama miti kimya, hawaongei na mtu wala wenyewe kwa wenyewe, halafu wanakuwa na kitu kama radio yenye antanae ndefu imevaliwa kifuani, hata mvua inyeshe hawatoki. Hawa wa kwetu wanatembea tembea na kufukuzana na boda boda hawako makini na kazi ilyowaweka pale.
 
Kamwe huwezi jua mambo ya ulinzi kama si mlinzi.

Na yeyote asiyeheshimu taaluma za wengine hata yake haijui. Tukumbuke ujambazi siku hizi unafanyikia hasa kwenye mataa kama pale moroko,tazara,aiport,ubungo,namanga je bado hujaona umuhimu wa uwepo wa wale askari kwenye mataa? Tukumbe taarifa zinaonesha siku ambazo ambazo hapakuwepo askari pale mataa ndizo kulitokea ujambazi.

Pia rafiki yangu mtoa post hii kumbuka kuwa kumsimamisha balozi katika barabara si kosa kwani anaweza kupewa maelekezo kwa usalama wake
 
Msisahau kuwa vifo vingi hapa taz vinasababishwa na ajali pia wale polisi wanaofanya hizo kazi wanaitwa general duty au polisi wa kazi zote hivyo kukagua leseni au kufanya kazi yeyote ya polisi ni wajibu wake ila kama atavuka mipaka ya sheria ya nchi atakuwa amekanyaga katiba lakini pia tukumbuke polisi yeyote wa kitengo chochote anaruhusiwa kudhibiti uhalifu wowote unaokatazwa na sheria za nch.

Pia nathubutu kukiri nimezunguka afrika mashariki yote ni tanzania pekee ndiyo wanaojali na kuheshimu haki za bin
 
Mkuu hao maaskari ni wa muhimu kuwepo katika maeneo hayo, ila labda wao wanatumia vibaya uwepo hao hapo. Lakini lengo la kuwepo hapo ni ulinzi kwa kuwa eneo hilo magari yanasimama kuna uwezekano wa uhalifu kutokea kama vile kuporwa gari au kitu cho chote cha thamani. Aidha, kama kunatukio limetokea sehemu wanapewa taarifa wanazuia vyombo vya usafiri na kuchukua hatua stahili. Kuna baadhi ya matukio huwa wanakamata wezi au majambazi, hata hivyo, kwa sababu ya kukosa maadili ndio maana waingilia maswala ya traffic polisi kama vile kukagua usalama ma magari ikiwa ni pamoja na kuchomoa funguo za Boada boda. Nilishangaa Rwanda wasimama kama miti kimya, hawaongei na mtu wala wenyewe kwa wenyewe, halafu wanakuwa na kitu kama radio yenye antanae ndefu imevaliwa kifuani, hata mvua inyeshe hawatoki. Hawa wa kwetu wanatembea tembea na kufukuzana na boda boda hawako makini na kazi ilyowaweka pale.

Ni kweli mkuu, ni muhimu wao kuwepo hapo kwa kazi husika, na si vinginevyo!
 
Wale ni rapid n quick response yaani kama unaweza hata kujaribu kuwaza wewe mwenyewe, "Kwa mfano nakuambia tupange racket ya kufanya Ujambazi labda Exim Bank Namanga nipe njia rahisi ya kukimbilia kumbuka tupo na gari? Na sehemu utakazo waza ni ngumu kupitika nikwa sababu ipi?".

Kiukweli mimi binafsi naongea toka Moyoni tupo wengine yumkini tu maskini wa kutupwa lakini kuna wengine wanaumia kwa ajiri ya usalama wetu. Sehemu nzuri za kuvuruga mipango ni njia panda labda kwa mawazo yako binafsi ya haraka uliwaza ni vyema wakae wapi? Haya mfano mwingine labda tuseme wangekaa vituoni mwao. Haya tukio limetokea Victoria la wizi au ujambazi wewe kwa mawazo yako ya haraka labda polisi watoke Oysterbay kituoni kukabiliana na tukio ? Je wakikuta foleni imeshona watatokaje?

Lakini kwa hali ilivyo saizi ni kwamba Morroco Junction Ujambazi gari XXXX aina XXX na Shell Junction taarifa hivyo hivyo Mwenge Junction, Darajani, Magomeni mataa zote hizo ni taarifa zinasambazwa na wengine wanaingia msako kazi inakuwa rahisi .

Suala la magari kusimamishwa elewa inakuja hapa labda ujambazi wa jana gari aina XXX lilitumika na halijaonekana likitoka maeneo hayo ya Vizuizi kwa hiyo gari lolote lenye kufanana na gari XXX hata kama halina number XXX kwa kuwa plate no. Kazi rahisi kubadili kwa hiyo magari yote yatakayotoka zone hiyo yatakaguliwa kwa kufananana na Gari XXX. Na muda mwingine labda viongozi wanapita na sehemu za makutano ndio nzuri kwa rackets hata kulipua na kufanya maovu njiapanda ndio mpango, nipe tasks yoyote ya uharifu harafu nikupe Illustration ya racket.
 
Kukaa njia panda na silaha ni sahihi kabisa ila wanakosea pale wanapoanza kusimamisha magari kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida. Nazani ni kwa ajili ya njaa tu.

Mimi wameshawahi kunikamata pale magomeni, wakaniambia nimepita na taa nyekundu, kitu ambacho kilikua sio kweli, walitaka kuingia ndani ya gari na mabunduki yao nikawakatalia, wakaomba hela nikawatolea nje tukaongozana mpaka kituoni, ikabidi tu nilipe faini ili niendelee na mishemishe zangu.

Njaa inasababisha waache kufanya kazi iliyokusudiwa na wanageuka kero kwa watumiaji wa barabara'
 
Unaongelea nini mtoa mada? Yaani mtu ambaye ana namba za kidiplomasia asisimamishwe kwani yeye sheria inamexclude?

Tembelea nchi kama German uone askari wake kama hawana silaha wakati wakiwa kwenye kazi za kitraffic.

Utofauti ni kwamba wanatumia bastola badala ya haya masilaha yetu makubwa yanayotisha watu wakiyaona.

Naunga mkono hoja usumbufu ila si kubagua nani asimamishwe nani asisimamishwe.
 
Mifumo ya doria nchini kwetu ni mibovu na askari wetu wana kaa makini kutafuta mianya ya rushwa kwa sababu ya njaa zao na kujikuta wamewasimamisha hadi wawakilishi wa mataifa mengine nchini kwetu, btw tuige mifano ya doria za Rwanda, Burundi, Uganda, Angola, Msumbiji itasaidia sana kwani hawa wenye silaha huongozana muda wote na hasa mitaa ya kariakoo wangekua wengi kuzunguka maeneo yale, lkn ukaguzi wkt wa kuingia kwenye taasisi zetu hasa za fedha kwa mfano mabenki ni mbovu sana
 
Hatujakataa wao kukaa barabarani tatizo ni rushwa wanazoanza kuomba hadi kwa mabalozi kwa kukagua eti taa cjui nini na nin? Na unadhani ni matukio mangapi ya kihalifu yametekelezwa na watu kuondoka? Halafu Polisi wengine wengi wapewe pikipik zenye namba za kiraia na wazunguke maeneo ya Jiji ili kufuma baadhi ya uhalifu kirahisi sana lkn pia kitengo chao cha upelelezi kinaonekana kimelala sasa kwan matukio yamezidi nashauri wajikite zaid kupeleleza kabla ya matukio na sio kusubiri baada ya matukio ndo waanze kukukuruka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom