illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,119
Hawa waheshimiwa kwenye makutano ya barabara huwa wanafanya kazi gani jamani utawakuta wamebeba mabunduki makubwa halafu wanasimamisha magari wanaanza lete leseni, na makorokoro kibao, ni nani anawapangia hilo jukumu?
Cha kusikitisha zaidi hawana uelewa wa kazi yao kwani huwa wana wasumbua mpaka watu wenye magari yenye namba za kidiplomasia "CD" kweli wanaharibu taswira ya taifa letu ni aibu mtu mwenye hadhi ya kibalozi kusimamishwa na askari mwenye cheo kidogo na mwenye silaha kisha kumsumbua kwa vyovyote vile, hii inaharibu uhusiano wa kimataifa, na wale wengine wanaovaa sare za ffu almaarufu kwa jina la tigo.
Kweli wanasikitisha sana wakati mitaani tunalia na panya rodi na mbwa mwitu wenyewe wana kimbizana na waendesha boda boda wanafikia mpaka hatua ya kupiga risasi juu mara wanapokimbiwa.
Wazo langu nimewahi kutembea taifa fulani la jirani kuna kitu kinaitwa gorilla patrol ambapo hawa askari wenye silaha za moto wanatembea kwa miguu watatu watatu mtaa kwa mtaa na kuna wengine wanazunguka na magari inakuwa rahisi kudhibiti uhalifu unapotokea.
Nataka niamini kuna wataalamu wa criminology katika taifa letu ila hili la smg kwenye traffic lights bado sijui lengo hasa ni nini!!