Polisi wazuia mikutano ya Mbunge wa Tarime kisa Waziri Mkuu ana ziara mkoani Mara siku zijazo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
JESHI la Polisi, Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara, limepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) kwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara mkoani Mara.

Mbunge huyo alipanga kufanya mikutano hiyo kuanzia jana hadi Januari 11 mwaka huu.

Katika barua iliyoandikwa na Mrakibu wa Polisi aliyejitambulisha kwa jina la I. Kimasa kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tarime kwenda kwa Matiko, mbunge huyo ameagizwa aahirishe mikutano yake hadi Waziri Mkuu Majaliwa atakapokamilisha ziara yake.

“Kutokana na sababu za kiusalama kuhusiana na ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, unashauriwa kuahirisha mikutano yako ya hadhara kwenye viwanja vyote ulivyotoa taarifa. Mikutano hiyo ifanyike baada ya ziara ya waziri mkuu,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo, Matiko akizungumza na MTANZANIA, alipinga hatua hiyo kwa madai kuwa inakwenda kinyume na sheria na haki za mbunge.

Katika maelezo yake, Matiko alisema amejijengea utaratibu, kwamba kila akimaliza kuhudhuria vikao vya Bunge, hurudi jimboni kukutana na wananchi wake na vikundi mbalimbali na kuwapa mrejesho kutokana na yale waliyomtuma bungeni.

“Nikiwa jimboni nina wajibu wa kuzunguka kwenye kata zangu na kuwaeleza wananchi wangu ni yapi nimeyafanya bungeni na kuchukua kero zao niende nazo bungeni na zingine tuweze kuzitatua katika ngazi ya halmashauri.

“Niliandika barua kwenda kwenye ofisi ya OCD Wilaya ya Tarime kuwajulisha kwamba niko jimboni na nitakuwa nafanya ziara na niliainisha mikutano mitatu.

“Cha ajabu wameniletea barua na kusema kuwa niahirishe mikutano hadi ziara ya waziri mkuu ipite."


Chanzo: Mtanzania

========

Pia kuna ujumbe mfupi wa SMS unasambaa ukisema

"Taarifa ya ujio wa m/kiti wa CCM Mkoa, imetokea dharula ya kikazi mjini TARIME ya kuwapokea madiwani wa chadema wanaoingia CCM, mpaka mtakapotaarifiwa na uongozi, upatapo ujumbe sambaza, CCM oyee"
 
NI KWA SABABU YA HII MSG INAYOSAMBAA, USISHANGAE SANA,
"Taarifa ya ujio wa m/kiti wa Ccm Mkoa, imetokea dharula ya kikazi mjini TARIME ya kuwapokea madiwani wa chadema wanaoingia ccm,mpaka mtakapotaarifiwa na uongozi,upatapo ujumbe sambaza, ccm oyee"
 
Wanahisi masikio na macho ya wakurya vitazibwa na speech za mbunge na hivyo kushindwa kumsikia na kumwona PM
 
Ujumbe huo unasambazwa na wenyeviti wa ccm kata kwa makada watiifu wa chama.
 
Hakuna jambo jipya hapo,bali ni mwendelezo wa siasa pasipo fikra pevu.
 
Ni kawaida Waziri Mkuu Siyo Kiongozi Wa kubezwa kwa Sababu za Kiusalama wako Sahihi.
 
Ni kawaida Waziri Mkuu Siyo Kiongozi Wa kubezwa kwa Sababu za Kiusalama wako Sahihi.
Kwa hiyo nchi yetu sio salama ? Ingekuwa siku moja sawa, lakini eti ana ziara "siku zijazo"! Uhuni uleule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom