Polisi waweka ulinzi mkali Dodoma

Polisi waweka ulinzi mkali Dodoma

richaabra

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
1,472
Reaction score
3,535
Dodoma. Haieleweki kama ni kutokana na tishio la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) au ni mabadiliko ya kawaida,mPolisi wameamua kuweka ulinzi mkali mjini hapa.

Jana, Kamati Kuu ya CCM ilifanya kikao kwenye jengo la makao yake makuu maarufu White House, ambalo lilikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye sare, askari kanzu, askari wa kikosi cha mbwa, hali iliyofanya mtu asiyehusika kupenyeza maeneo hayo kuwa ngumu tofauti na ilivyozoeleka.

Magari yaliyobeba askari polisi, vikosi vya mbwa na maofisa Usalama wa Taifa walionekana kutanda maeneo yote kuzunguka jengo hilo lililopo Barabara Kuu, katikati ya mji wa Dodoma. Mapema wiki hii, mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alitoa tahadhari kwa mtu yeyote anayetaka kufanya vurugu, akisema wamejiandaa vizuri kukabiliana nao.
 
Dodoma. Haieleweki kama ni kutokana na
tishio la Baraza la Vijana wa Chadema
(Bavicha) au ni mabadiliko ya kawaida,
Polisi wameamua kuweka ulinzi mkali
mjini hapa.
Jana, Kamati Kuu ya CCM ilifanya kikao
kwenye jengo la makao yake makuu
maarufu White House, ambalo lilikuwa
na ulinzi mkali wa polisi wenye sare,
askari kanzu, askari wa kikosi cha mbwa,
hali iliyofanya mtu asiyehusika
kupenyeza maeneo hayo kuwa ngumu
tofauti na ilivyozoeleka.
Magari yaliyobeba askari polisi, vikosi vya
mbwa na maofisa Usalama wa Taifa
walionekana kutanda maeneo yote
kuzunguka jengo hilo lililopo Barabara
Kuu, katikati ya mji wa Dodoma.
Mapema wiki hii, mkuu wa mkoa wa
Dodoma, Jordan Rugimbana alitoa
tahadhari kwa mtu yeyote anayetaka
kufanya vurugu, akisema wamejiandaa
vizuri kukabiliana nao.

Source.Mwananchi
 
Kawaida sehemu yenye viongoz wa juu lazima....... Cjui ndo mara yk ya kwanza kufika maeneo km hayo
 
Majuzi Marekani tumeona Republican na Democratic wakifanya mikutano yao bila na gari ya deraya wala Makundi ya mbwa wapolisi. ANC,ZANU, nk nk hawajawahi kufanya mikutano wakiwa wamezingirwa na maelfu ya askari idadi kama ya wajumbe.
Nini kimepelekea CCM kuvunja rekodi hii ya dunia?
 
Majuzi Marekani tumeona Republican na Democratic wakifanya mikutano yao bila nagari ya deraya wala Makundi ya mbwa wapolisi. ANC,ZANU, nk nk hawajawahi kufanya mikutano wakiwa wamezingirwa na maelfu ya askari idadi kama ya wajumbe.
Nini kimepelekea ccm kuvunja rekodi hii ya dunia?
pamoja na kupata lunch nimeshindwa kukuelewa..
 
Majuzi Marekani tumeona Republican na Democratic wakifanya mikutano yao bila nagari ya deraya wala Makundi ya mbwa wapolisi. ANC,ZANU, nk nk hawajawahi kufanya mikutano wakiwa wamezingirwa na maelfu ya askari idadi kama ya wajumbe.
Nini kimepelekea ccm kuvunja rekodi hii ya dunia?
Hivi sehemu ambayo yupo Rais wa nchi waziri mkuu, makamo wa Rais ulitegemea ilindwe kiukawa?
 
"BAVICHA hawatuwezi" kweli vijana wanajua kupata promo za Bure..UVCCM chali
 
Majuzi Marekani tumeona Republican na Democratic wakifanya mikutano yao bila nagari ya deraya wala Makundi ya mbwa wapolisi. ANC,ZANU, nk nk hawajawahi kufanya mikutano wakiwa wamezingirwa na maelfu ya askari idadi kama ya wajumbe.
Nini kimepelekea ccm kuvunja rekodi hii ya dunia?
Bila Polisi Magamba ni mepesi kama Unyoya
 
Hivi sehemu ambayo yupo Rais wa nchi waziri mkuu, makamo wa Rais ulitegemea ilindwe kiukawa?

Naona alitaka walindwee na hawa vibaka walinzi wa CHADEMA.Waangalie walinzi wa CHADEMA wakiwa wamevaa miwani yao ya kuchomea magrill ya chuma.Halafu angalia yule aliyekaa juu ya ukuta kujifanya mlinzi hata ukipuliza upepo tu anadondoka.Hawa ndio walinzi wa CHADEMA wacheck

Mbeya3.jpg
 
Back
Top Bottom