Polisi wawatisha viongozi wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wawatisha viongozi wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Jul 12, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,373
  Likes Received: 8,495
  Trophy Points: 280
  *Ni kwa viongozi kukataa kuhojiwa

  *Yasisitiza kuchunguza tuhuma zao

  *Yaonya haitakubali kuyumbishwa


  JESHI la Polisi limesema licha ya viongozi wa Chadema kukataa kuhojiwa, litaendelea kuchunguza tuhuma za chama hicho dhidi ya baadhi ya maofisa wa serikali na kuchukua hatua zaidi.
  Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema jeshi hilo haliwezi kuyumbishwa na mtu au kikundi cha watu katika kutekeleza majukumu yake na litafanya kazi kwa kufuata sheria na maadili.

  Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kukataa baadhi ya viongozi wake kuhojiwa ikisema haioni sababu ya kutii agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi.

  Dk. Nchimbi alitoa agizo hilo baada ya viongozi watatu wa Chadema, Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kudai baadhi ya maofisa usalama wa taifa wamekuwa wakiwafuatilia wakiwatishia kuwaua.

  “Jeshi la polisi ni chombo cha umma kinachowajibika kulinda watu na mali zao, pia tunatekeleza kazi zetu kwa haki, usawa na bila ubaguzi wowote. Hili la viongozi wa Chadema kukataa kuhojiwa haliingii akilini hata kidogo.

  “Kwa akili ya kawaida, chukulia mtu amevamiwa nyumbani kwake na majambazi akapiga kelele kuomba msaada na askari au watu wengine wakafika kumpatia msaada, kweli atashindwa kuwaelezea kilichompata?

  “Hawa Chadema kukataa kwao hakutuzuii sisi kufanya kazi na hatuwezi kuyumbishwa na kikundi au mtu yeyote bali tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na maadili.

  “…sitowaeleza sasa tunachokifanya ndani ya jeshi la polisi lakini baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutafanya uamuzi… isitoshe katika malalamiko yao waliwataja watu kwa majina,”alisema Senso.

  Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo zilidai kuwa hatua ya viongozi wa Chadema kukaidi kuhojiwa kunaweza kusababisha wakamatwe.

  Juzi Dk. Slaa alitangaza kwamba hakubaliani na agizo la Dk Nchimbi kutaka kuwahoji kwa kuwa akisema kuwa yeye na wenzake hawana tena imani na vyombo vya serikali ikiwamo polisi.

  Dk. Slaa alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wake lenyewe kuhusiana na madai yao na kutoa tamko na sio kuwahoji wao ambao ndio walalamikaji.

  Alisisitiza kwamba Chadema hakina imani na polisi kwa kuwa wamekuwa wakipuuza malalamiko wanayopelekwa na chama hicho.

  Chadema imekuwa ikiwasilisha madai yake mengi polisi yakiwamo ya wabunge wake kupigwa mkoani Mwanza lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, alisema.

  Dk. Slaa alisema kama Serikali isipokaa vizuri katika usalama wa raia wake na kutimiza wajibu na ahadi zake kwa Watanzania, taifa litakwenda pabaya.

  Naye Msaidizi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka ambaye ni mmoja wa maofisa usalama aliyetajwa kuhusika kuwatisha viongozi hao wa Chadema amekwisha kutoa kauli akidai kuwa malalamiko ya viongozi wa CHADEMA ni propaganda za siasa na zinapaswa kupuuzwa.
   
 2. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Polisi wajiangalie vizuri, kwani Watanzania wengi kwa sasa hawana imani na vyombo vya dola kutokana matukio yaliyowahi kutokea na yanayotokea sasa ni lazima wananchi wengi watakosa imani. Inaonekana vyombo vya dola na usalama wa Taifa viko kwa maslahi ya Chama tawala kitu ambacho ni hatari kwa amani ya Taifa letu. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awaondoe Watawala wenye nia kama hii.
   
 3. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hata wao wanaweza kuwa ni kundi la watu tu. Issue ni Tabia.
   
 4. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Niambie ni Mtanzania gani mwenye imani na jeshi la polisi?Ukiwa na tatizo umeenda kuto taarifa,unapigwa mzinga kwanza halafu ndio unaeleza tatizo.wanaweza wakampata mhalifu,wakala hela yake halafu wanakuja kukushauri uachane na hiyo kesi kwani haitafanikiwa.Huku ukiwaacha wamekula hela yako na ya mhalifu.
   
 5. U

  Udaa JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Police thithiem sina imani nao.hata wao wanajijua jinsi wtz tusivyo na imani nao.
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Polisi yenyewe ni kakikundi kadogo ka watu!
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kama suala la kuwataja watu kwa majina ni ishu mbona Regnald Mengi aliwataja mpaka kwa majina Polisi waandamizi kuhusika katika mchezo mchafu wa kula hongo ili wambambikize kesi ya madawa ya kulevya mwanaye mbona kimyaaa!!

  Watanzania tuamke Tanzania hamna Polisi huru hiki chombo nahisi kinafanya kazi kwa maelekezo ya kikundi fulani cha wahuni, nitasimamia huu mfano wangu wa aliyoyasema Regnald Mengi mpaka naenda kaburini.
   
 8. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi yule Polisi ayeita rai Panya kule Arusha aliishia wapi?halichukuliwa hatua gani?Je yule askari inayesadikiwa kuwa ndiyo alikuwa muhusika mkuu katika ile kesi ya wafanyabiashara na Jaji akaagiza akamatwe mbona mpaka leo hatujasikia kitu?
   
 9. N

  Ndet Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawaunga mkono viongozi wa cdm kwa msimamo wao, kwasababu wabunge wao wa mwanza walijeruhiwa, lakini mpaka leo polisisiemu hawajasema kitu. kesi ya ngedele kumpelekea nyani utakuwa unachekesha.
   
 10. B

  Baba Hellen JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 764
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hawa polisi wenyewe ni sehemu ya tatizo alafu niaibu chombo kikubwa kamahiki kujidhalilisha mbele ya umma JAMANI UUUUUWI!!!! Nchi hii kila kitu kime EXPIRE
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ni vizuri Mwema na maafande wake wakajua kwamba Chama chochote kinaweza kukaa madarakani hivyo wasije wakamtukana mamba kabla hawajavuka mto.
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hawa Polisi vipi? au ndiyo wanazidi kutuaminisha kwamba JESHI la POLISI huwa wanajiunga VILAZA Dr. Ulimboka aliwataja kwa majina watu waliohusika kumteka na kumtesa tunaomba basi kwanza wakawahoji
  1. ACP Msangi
  2. Abeid Afisa wa Ikulu
  3. Pinda aliyesema Liwalo na liwe
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tuongeze vifaa gani ili intelejensia iweze kugundua mambo ya uhalifu na wahalifu badala ya maandamano na mikutano?
  au tochi ya intelejensia imeisha betri?
  au tuvunje intelejejsia na tuunde intelejensia nyingine?
  mbona imefanya kazi kwenye faru na mtalii?
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Polisi wetu ni wanasiasa tulishawazoea
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Wanatoa ahadi eti uchunguzi ukikamilika watatoa taarifa, at the same time, wamewatisha kina Slaa kuwa wanaweza kuwakamata.Sasa ina maana wakiwakamata ndo watasema?Ama wana mpango wa kung'oa watu meno na kucha?
   
 16. babujii

  babujii Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  ni kweli haiingiii akilini mtu kuvamiwa na majambazi na kukataa kuhojiwa na mamlaka zinazokubalika lakini ikiwa jambazi amekutegua kiuno halafu anakuja kukuchukua akupeleke hospitali,je! hii pia inaingia akilini una hakika gani kama ndo anataka akakuangamize ili kupoteza ushahidi? hapa panahitajika mtu tofauti na haya majambazi ili kutafuta undani wa tatizo lililopo. jamani tusiwe wanasiasa hata katika mambo ya kitaaluma. POLISI acheni hizo.
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama kuna kitu jeshi la polisi halifanyi ni hilo hapo juu, mara ngapi tunaona mapolisi wanahusishwa na ujambazi..embu watutokee hapa
   
 18. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Mi nadhani polisi wanapaswa kutueleza/ kutupa matokeo ya vipaza sauti chumbani kwa Slaa na tuhuma nyingine. Huu sio wakati wa kutoa majibu mepesi kwa lengo la kuuaminisha umma mambo yasiyokuwepo.

  POLISI YANYENI KAZI YENU ACHENI SIASA ZA KIBABAISHAJI. Msifikiri umahiri wa kazi unatokana na mavazi yenu, la hasha. Tuanataka umahiri.

  After all wananchi wa leo wana uelewa mkubwa sana.

  We need intelligible explanations to such serious issues.
   
 19. M

  Malova JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  POLI NYINYIEMU, mnaacha kutafuta ukweli wa tuhuma kwa kufanya uchungu mnataka kuwahoji walalamikaji. UPUUZI mtupu
   
Loading...