Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Kurundukwa kama magunia kwenye mabasi ni ushenzi wa kiwango cha juu. Tutastaarabika lini. Tuache mazoea. Zamani watu walipiga mswaki kwa kutumia miti, je unapenda tuendelee na mazoea hayo ya zamani? Tuchukue hatua. Saa ya ukombozi ni sasa
 
Polisi wenyewe wanatufundisha gari/ basi haitakiwi kujaza abiria kwa kuwarundika kama magunia ya viazi. Endapo itatokea ajali maafa huwa makubwa zaidi kuliko endapo watu wangekaa level seat. Lakini polisi haohao hawachukui hatua hadi yatokee maafa. Kila siku tunashuhudia daladala zinavyojaza watu kwa kuwarundika. Tuache maisha ya mazoea
 
Ajali imetokea Temeke sehemu gani?! Au pale Machinjioni kazi imeanza upya?
 
Ndio maana wengine tulisema bora corona iendelee ili tuishi kistaarabu. Kunawa mikono, level seat, kuropokaropoka hovyo kulipungua n.k , n.k
Watanzania ustaarabu tutaendelea kuusikia kwa wenzetu. Tutasubiri sana
 
Hawa polisi huwa tunawalaumu bure tu wakati mwingine. Kama hoja yako ni watu kusimama, kwamba wangekuwa wamekaa wasingekufa, akili za wapi hizi? Hivi umeona hata picha za hiyo ajali? Hivi kweli pale kusimama kunazuia nini au bahati tu ndo inayokuokoa?

Sikushangai sana maana lawama ndo imeshakuwa mtindo wetu lakini wakati mwingine tutumie akkli kidogo, usimlaumu asiyestahili
 
Tatizo sio level siti bali ni ufukara wa watu wa dar, wengi ni walalahoi wakiweka nauli ya sh 1000 kelele mji mzima. Tembelea nchi jirani uone
Kweli niliona Kampala hiece wanaziita tax zinapakia level Siti Ila nauli Iko juu kidogo. Ikifika kwenye kituo konda anatangaza Siti tupu kama ziko 2 ina maana wataopanda ni wawili Tu.
 
Ndio maana wengine tulisema bora corona iendelee ili tuishi kistaarabu. Kunawa mikono, level seat, kuropokaropoka hovyo kulipungua n.k , n.k
Tatizo wasimamizi wa sheria hawataki kuchukua hatua. Huenda rushwa ndio chanzo kikuu cha kufumbia macho uvunjwaji wa sheria
 
Tunatakiwa kubadilika kama jinsi dunia inavyobadilika. Tuache kuendekeza mazoea
 
Tatizo sio level siti bali ni ufukara wa watu wa dar, wengi ni walalahoi wakiweka nauli ya sh 1000 kelele mji mzima. Tembelea nchi jirani uone

anayetoa 1200 ya nauli hashindwi kutoa 2000.

hiyo ni kanuni ya wastani tunaita.kelele huzaliwa pale konda anapojiamulia kutoza elfu moja mamlaka gazijui.

kuna utaratibu wa kugeuza na gari watu wanalipia 1000 kila siku na gari inasimamisha.
 
Tatizo linaanzia mbali daladala nyingi ambazo zimepitishwa sisi wenye urefu wa kawaida tukisimama inabidi kuinamisha vichwa
 
Kwa nini waseme dereva wa daladala ndo mwenye makosa bila kumwajibisha dereva wa lori kwa kushindwa kuendesha kwa kujihami kwenye junction. Inakuwaje huyo dereva wa lori ajiachie kisa taa nyekundu imemruhusu bila kuchukua tahadhari yoyote?
 
Utawalaumu askari lakini abiria wenyewe wabishi
Kwanini Gari limejaa wamepanda......
Wakati mwingine usalama uanzie kwetu wenyewe
Tuache unafiki

Ova
 
Utawalaumu askari lakini abiria wenyewe wabishi
Kwanini Gari limejaa wamepanda......
Wakati mwingine usalama uanzie kwetu wenyewe
Tuache unafiki

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kuna urasimu mkubwa wa kusajili njia za daladala pale Sumatra (LATRA). Wanakypangia wao njia (route). Sio njia unayotaka wewe. Matajiri wengine hukata tamaa kuongeza madaladala barabarani
 
Kwa nini waseme dereva wa daladala ndo mwenye makosa bila kumwajibisha dereva wa lori kwa kushindwa kuendesha kwa kujihami kwenye junction. Inakuwaje huyo dereva wa lori ajiachie kisa taa nyekundu imemruhusu bila kuchukua tahadhari yoyote?
Madereva wote wana hatia ktk suala hili
 
Abiria wakisimama kwa kurundikana kama magunia ya viazi endapo itatokea ajali madhara huwa ni makubwa zaidi tofauti na wakiwa level seat. Hata watengenezaji wa hayo magari wameweka kiwango cha idadi ya abiria wanaostahili kuwemo. Naamini waliotengeneza magari wana uelewa mkubwa wa magari zaidi ya sisi watumiaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…