Mkuu umewahi sana kuuleta huu Uzi humu Jf.
Kwanza,sijaelewa lengo la Uzi wako kwasababu zifuatazo.
Moja, polisi wamevamia kishari eneo, hapo hapo unasema wamevaa kishari,Lakini pia eneo walilofika ni kwenye uwanja tena ulio jirani na kota za polisi wenyewe.
Pili, wamekuja uwanjani, hawajaenda kwa MTU, kwanini usingefikiri tu kua wamekuja ktk mazoezi yao ya kawaida ktk uwanja Huo ?
Tatu, ungejiongeza tu kama GT ,kabla ya kuandika neno hili la kichochezi kua "wamevamia" ungeangalia kwanza mandhari husika uliyopo na walipofikia uone je Kuna vurugu lolote? Hata kama no fujo,je kwa muda ulokaa hapa garage ushapata tetesi ya vuguvugu lolote mtaa Huo?
Nne, naona cruiser tena IPO kituoni kabisa,sasa sijui ulitaka polisi wapaki au wafikie wapi pindi wanapotoka kwenye majukumu yao.
Nsamehe mkuu,ila sijaona logic bado labda nsubirie hizo updates