Polisi wavamia mtaa wa Njaro Temeke muda huu

mwamajinja mapunga

JF-Expert Member
Dec 23, 2014
1,077
1,500
Habari watu wa Mungu muda huu naandika huu uzi hapa limekuja karandika la polisi yaani Defender wakiwa wamevalia kishari sana wakiwa na sihala za Moto mtaa wa Njaro Temeke karibu na Kota za Polisi hapa za TAZARA kuna kauwanja hivii....

Nipo maeneo haya kuna fundi tumeleta lori hapa limesumbua control system kwa fundi Maarufu aitwaye China.

Nitawapa mrejesho kilichowaleta. Maana picha imepigwa kwa wizi sana na walikuwa mbali kidogo nime i zoom kidogo.

Asante najua wajuaji watakuja na maneno yao mara hoo unakimbia kimbia kuleta uzi shauri yako. Picha hapo chini 

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,506
2,000
Mkuu umewahi sana kuuleta huu Uzi humu Jf.
Kwanza,sijaelewa lengo la Uzi wako kwasababu zifuatazo.

Moja, polisi wamevamia kishari eneo, hapo hapo unasema wamevaa kishari,Lakini pia eneo walilofika ni kwenye uwanja tena ulio jirani na kota za polisi wenyewe.

Pili, wamekuja uwanjani, hawajaenda kwa MTU, kwanini usingefikiri tu kua wamekuja ktk mazoezi yao ya kawaida ktk uwanja Huo ?

Tatu, ungejiongeza tu kama GT ,kabla ya kuandika neno hili la kichochezi kua "wamevamia" ungeangalia kwanza mandhari husika uliyopo na walipofikia uone je Kuna vurugu lolote? Hata kama no fujo,je kwa muda ulokaa hapa garage ushapata tetesi ya vuguvugu lolote mtaa Huo?

Nne, naona cruiser tena IPO kituoni kabisa,sasa sijui ulitaka polisi wapaki au wafikie wapi pindi wanapotoka kwenye majukumu yao.

Nsamehe mkuu,ila sijaona logic bado labda nsubirie hizo updates
 

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,464
2,000
Habari watu wa Mungu muda huu naandika huu uzi hapa limekuja karandika la polisi yaani Defender wakiwa wamevalia kishari sana wakiwa na sihala za Moto mtaa wa Njaro Temeke karibu na Kota za Polisi hapa za T miAZARA kuna kauwanja hivii.... Nipo maeneo haya kuna fundi tumeleta lori hapa limesumbua control system kwa fundi Maarufu aitwaye China. Nitawapa mrejesho kilichowaleta. Maana picha imepigwa kwa wizi sana na walikuwa mbali kidogo nime i zoom kidogo. Asante najua wajuaji watakuja na maneno yao mara hoo unakimbia kimbia kuleta uzi shauri yako. Picha hapo chini
Wewe kweli huijui JF na hujui namna ya kuitumia kwa usahihi ,,yani unapost taarifa za ujio wa polisi mtaani kwenu halafu unajieleza na wewe ulipo???? Unayajua madhara yake lakini? Subiri ufuatwe hapo ulipo ubebwe kwa kosa la uhalifu mtandaoni

Soma mfano hapo chini ili ujue kosa lako:

Yawezekana polisi wamepata taarifa za tukio la uhalifu mitaa jiran na hapo wakaona ili tuvamie vizuri gari letu tulipaki mbali kidogo twende kwa miguu eneo la tukio , sasa wewe ndugu kwa kiherehere umevujisha habari kabla hawajafika huko maana yake tayari kama kuna mpango huo basi wahalifu wata ambizana na kukimbia mapema na wewe kuonekana mshiriki kwa kutoa taarifa za uwepo wa askari maeneo hayo bila utaratibu kitu kilicho sababuisha wahalifu wakimbie mapema .

Lakin kwa vile umesha elekeza upo hapo kwa fundi CHINA unarekebisha lori nadhan wewe utasaidia kianzio.

Maana ya matumizi ya mtandao sudhani kama nahii yakwako ni moja wapo!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom