Friday Malafyale
JF-Expert Member
- Jan 18, 2017
- 1,811
- 2,916
Niko hapa maeneo ya Ubungo Plaza nikiwa nimejiandaa vema kuhudhuria tukio la uzinduzi wa kitabu cha ndugu uyetu Alphonce Lusako ghafla naona magari ya polisi matatu lingine likiwa limepaki kwa mbali.
Hapa nilipo imenibidi nijifanye mpita njia maana wamemkamata Mkuregenzi wa kituo cha utetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Ndg, Onesmo Ole Ngurumwa pamoja na ndugu Baraka, wamechukuliwa hapa Blue Pearl na Police.
Wanaelekea kuhojiwa na OCD Kituo cha polisi Magomeni.
========
Kitabu kilichotaka kuzinduliwa kinaitwa Sauti ya Watetezi wa Haki Vyuoni.
Onesmo Olengurumwa ameachiwa kwa dhamana jioni ya leo.